Saranga waanza kupata majisafi ya dawasa

Saranga waanza kupata majisafi ya dawasa

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
1553328550801.png



WAKAZI wa Kata ya Saranga wilayani Ubungo mkoani Dar es Salaam, wamesherehekea kilele cha Wiki ya Maji kwa furaha, baada ya kuanza kupata majisa ya bomba, ambayo hawajawahi kupata tangu Uhuru mwaka 1961. Mkuu wa wilaya hiyo, Kisare Makori, ndiye aliyezindua mradi huo wa maji, uliojengwa na Mamlaka ya Majisa na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa).

Wakazi hao wa Saranga wanaunganishwa kwenye huduma ya kupata majisa kwa mkopo; na hakuna kuchangishwa. Wataanza kulipia bili, baada ya maji kuanza kutoka kwenye mabomba yao. Dawasa ndiyo inayochimba mtaro kwa gharama zake na wananchi hawatakiwi kuchangia gharama za kuchimba mtaro. Mkurugenzi wa Miradi wa Dawasa, Lydia Ndibalema, alieleza kuwa Dawasa imetekeleza mradi huo, kwa sababu Saranga ni moja ya maeneo ambayo kwa miaka mingi, lilikuwa na tatizo kubwa la majisa ya bomba.

Pia, maji ya visima vingi katika eneo hilo, hayakuwa na ubora. Alisema programu ya kuyapatia maji maeneo yasiyokuwa na maji ya bomba, inatekelezwa katika maeneo mengi ya jiji. Kwa wilaya Ubungo maeneo hayo ni pamoja na Malambamawili na Msakuzi, ambayo miradi yake ya maji, itakamilishwa wiki ijayo. Diwani wa Kata ya Saranga, Haruni Mdoe alisema kata yake ina wakazi 120,000 wanaoishi katika mitaa ya Ukombozi, Saranga, Upendo, Matangini, Stop Over, Michungwani, Kimara B na Busara.

Meneja wa Kitengo cha Ubora Dawasa, Christian Christopher, alisema mabomba wanayolaza Saranga yatadumu kwa muda mrefu na kwamba wanafuatilia ubora wa maji kwenye mabomba wanayolaza na mitaro inayochimbwa.

Alisema lengo la Dawasa ni kuwa ikapo mwaka 2020, asilimia 95 ya wakazi wa jiji hilo wawe wanapata majisa. Mkuu wa Wilaya, Makori alisema tukio hilo kubwa na la kihistoria, kwa sababu eneo hilo halijawahi kuwa na maji ya bomba tangu Uhuru. Alisema mradi huo ni matunda ya kazi kubwa, inayofanywa na serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli, ambayo siyo serikali ya maneno maneno, bali ya vitendo na kuongeza kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, serikali iliahidi itaondoa kero ya maji katika eneo hilo ; na sasa imetekeleza.

Makori alisema baada ya mtaa wa Saranga, Dawasa itasambaza maji katika mitaa ya Upendo na Ukombozi, isiyokuwa na huduma hiyo. Mwenyekiti wa CCM Kata ya Saranga, Irene Daffa alisema hatua ya kata yao kupata majisa ya bomba ni kama muujiza kwao, kwani hawajawahi kupata huduma hiyo tangu nchi ilipopata Uhuru, miaka zaidi ya 50 iliyopita.

Alisema kero ya maji ilikuwa inatesa zaidi wanawake, ambao walilazimika kuoga maji yanayowaletea fangasi na ukurutu. “Maumbile ya wanawake yanahitaji staha sana, lakini kutokana na shida ya maji tulikuwa tunalazimika kuoga maji yanayotuletea fangasi na ukurutu”, alisema Daffa huku akishangiliwa na wanawake wenzake.
 
Back
Top Bottom