Lengo la kubadilisha noti ya shilingi 500 kuifanya sarafu ilikuwa ni kutokana na noti hizo kuchakaa mapema kutokana na mzunguko mkubwa. Sasa kama hii sarafu ya 500 ambayo tunategemea pia itakuwa na mzunguko mkubwa imetengenezwa kwa viwango duni kama ulivyoandika basi itachakaa mapema zaidi ya ile noti ya 500. Sasa hapo BOT watakuwa wamefanya nini cha maana?
Nasubiria majibu ya vituko toka BOT. Usishangae ukaambiwa kuwa kupiga kutu kwa hiyo sarafu mpya ya jero ni moja ya alama ya ubora kwani nakumbuka wakati BOT walipobadili noti na watu kulalamika kuwa noti mpya zilikuwa zinachakaa mapema na zinatoa rangi na kuchafua walleti na mifuko yao Gavana alisema kuwa kutoka rangi kwa hizo noti ni moja ya alama ya ubora!