Sanchezi: Najuta kwenda Man u

hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,642
19,018
Sanchez: Nilitaka kuondoka Man Utd na kurudi Arsenal baada ya kufanya mazoezi siku ya kwanza.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez amekiri kuwa alitaka kuondoka Manchester United na kurudi Arsenal baada ya kufanya mazoezi siku yake ya kwanza tu na Mashetani Wekundu.

"Baada ya kufanya mazoezi yangu ya kwanza kabisa niligundua vitu vingi, nilirudi nyumbani na kuiomba familia yangu na meneja wangu ikiwa naweza kuvunja mkataba na kurudi Arsenal, hapakuwa sehemu sahihi, lakini nilikuwa tayari nimesaini," amesema Sanchez.

Akizungumzia wakati wake huko Manchester kupitia video iliyopostiwa kwenye Instagram yake, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anadai alifahamu haraka sana kwamba hatafurahiya maisha yake ndani ya klabu na aligundua kukosekana kwa umoja ndani ya kikosi cha United kilichokuwa kikinolewa na Jose Mourinho.

"Baada ya mazoezi ya siku ya kwanza tu niligundua vitu vingi, nilirudi nyumbani na kuuliza familia yangu na meneja wangu ikiwa siwezi kuvunja mkataba na kurudi Arsenal, kitu hakikunitoshea, lakini nilikuwa tayari nimesaini," Sanchez alisema.

"Miezi ilipita na niliendelea kuhisi hivyo hivyo. Hatukuwa na umoja kama timu kwa wakati huo.

"Waandishi pia walizungumza bila kujua na iliniumiza. Wachezaji wa zamani pia walizungumza na hawakujua ni nini kilikuwa kinaendelea ndani ya klabu. Na waliniumiza.

"Mchezaji pia anategemea mazingira ya ndani ya klabu, tunahitaji kuwa kama familia moja. Hatukuwa hivyo, na ilionekana hadi uwanjani. Ikiwa mtu alikosea, walinilaumu mimi.

"Ninajilaumu mwenyewe na nilipaswa kucheza vizuri zaidi. Lakini nilikuwa nikilaumiwa kila wakati, hata ikiwa nilicheza kwa dakika chache."

Itakumbukwa Sanchez alicheza game 45 kwa Mashetani Wekundu, akifunga mabao matano tu na kutoa assits tisa, takwimu ambazo zilikuwa chini sana ukilinganisha na mabao 80 aliyofunga kwenye michezo 166 na Gunners.
 
Tangu fergusson aondoke man u imekuwa utopolo united
 
Back
Top Bottom