KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,569
- 21,081
Sanamu la mkewe Donald Trump latoweka
Chanzo cha picha,Getty Images
"Melania" alionekana katika ukingo wa mto Sava huko Slovenia mnamo Julai 202, miezi minne kabla ya Melania Trump kuondoka katika ikulu ya Marekani kufuatia kumalizika hatamu ya mumewe Donald Trump.
Sasa miezi minne baada ya Melanija Knavs kurudi katika makao ya White House kufuatia kurudi madarakani kwa Trump, sanamu lake kubwa lililokuwepo katika ukingo wa mto huo wa Sava limetoweka kutoka mji wa Sevnica alikozaliwa huko nchini Slovenia.
Kilichosalia kwenye sanamu huyo mkubwa wa shaba ni miguu na kigutu cha mti chenye urefu wa mita mbili ambapo sanamu hiyo ilikuwa ikisimama.
Hii sio mara ya kwanza kwa tukio la aina hii la kumpa Melania Trump heshima lililoishia na mwisho mbaya huko Sevnica. Sanamu ya kwanza ilizinduliwa mnamo Julai 2019.
Ilichongwa kutokana na mbao moja na fundi wa eneo hilo Ales "Maxi" Zupevc. Ilikaa kwa mwaka mmoja kabla ya mtu asiyejulikana kuamua kuitekeza moto sanamu hiyo.
Kwa bahati nzuri msanii wa Marekani Brad Downey, aliyemuagiza Maxi kutengeza sanamu hiyo ya mbao, tayari alikuwa ameshatengeza mfano wa sanamu hiyo ambayo iliundwa upya kwa shaba na kuzinduliwa katika eneo lilo hilo.
Downey alieleza kuwa sanamu hiyo mpya iliundwa kuwa thabiti kwa kutumia shaba ambayo haiwezi kuharibiwa.
Lakini inavyoonekana imeweza kukatwa miguuni na kuibiwa. Polisi katika eneo hilo wanauchukulia mkasa huo wa kutoweka kwa "Melania" kama "wizi" na wameidhinisha uchunguzi