Samwel Sitta asisitiza: Dkt. Mwakyembe kalishwa sumu, asema kuna polisi majambazi

sumu ndo dawa pekee ya wafitini na wambea safi sana ulomwezeza mwakyembe sumu
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameendelea kusisitiza kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, unatokana na kulishwa sumu.

Kauli yake imekuja baada ya Jeshi la Polisi nchini kueleza kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri huyo hausababishwi na kula chakula chenye sumu; kauli iliyomuibua Dk. Mwakyembe na kudai Jeshi hilo halikumtendea haki akisema si lazima unyeshwe sumu ili ikudhuru.

Sitta amesema, hoja ya Jeshi la Polisi kueleza kuwa suala hilo linahitaji ushahidi ni kuupotosha umma ili usielewe nini kinachomsumbua Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya.

Akizungumza katika uzinduzi wa Asasi ya Kiraia ya Vijana wa Kanisa Katoliki mkoani Tabora (VITAL) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Askofu Mkuu Marco Mihayo, Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo mkoani hapa, alisema yeye kama Waziri hawezi kusema uongo kuhusu jambo hilo.

Alisema Jeshi la Polisi limekuwa likipotosha umma kukanusha kwamba Dk. Mwakyembe hajalishwa sumu ingawa Naibu Waziri huyo ana ushahidi wa kutosha kuhusu jambo hilo.

"Mimi nitapigana hadi siku ya mwisho kutetea wanyonge na ninashangaa kuelezwa kwamba mimi nimeshitakiwa na Polisi kwamba nimepotosha umma kusema kwamba Dk. Mwakyembe amelishwa sumu. Na kwa taarifa yako Baba Askofu nimeelezwa jalada langu limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ili nishitakiwe," alisema Sitta.

Alilishutumu Jeshi la Polisi kutokana na tabia ya kuhujumu watu na kusisitiza kuwa tabia hizo ni za kijambazi zinazoweza kuhatarisha hali ya usalama na maisha ya watu wanaozuliwa mashitaka kama hayo yanayomkabili.

Akizungumza ufisadi, alisema amekuwa mstari wa mbele kupinga suala hilo kwa nguvu zote na atahakikisha anapigana kufa au kupona kupambana na watu wanaojilimbikizia mali kwa kutumia madaraka yao.

Alisema jambo hilo halikubaliki na kwamba kwa sababu yupo hai, ataendelea kupambana nalo hadi hapo litakapoleta tija na hatimaye kuwawezesha wananchi wanufaike na rasilimali za nchi yao.

Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, lilieleza kuwa kwa taarifa ilizopewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Hospitali ya Apollo nchini India, ni kwamba ugonjwa wa Dk. Mwakyembe haukutokana na kulishwa kitu chenye sumu.


Source:
Habari leo
Hivi mwakyembe alilishwa sumu na nani?, sio wale jamaa wa richmond baada ya kuwaumbua bungeni na report yake
 
Back
Top Bottom