Samsung wajifunze kwa Apple

Samsung wajifunze kwa Apple

100 others

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2017
Posts
8,765
Reaction score
30,677
Samsung kuna kitu inapaswa wajifunze kutoka kwa wapinzani wao apple inc,nasema hivi kwa sababu haya ni maoni yangu binafsi na mtazamo wangu juu ya kampuni kubwa kama hili kuwa kila siku wanafanya mambo ya kukurupuka.

Samsung imekuwa ni kampuni inayoweka vikolombwezo viiingi kwenye simu hali ya kuwa havina hata umuhimu wowote ule bali ni ujanja wa kumkamata mteja,nitarudi nyuma kidogo tukumbushane na tuje sasa ili kuona ni lini Samsung atajifunza?

Yafuatayo ni mambo ambayo Samsung anapaswa kujifunza.
-Waache kuweka hardware/software features kwenye simu zao amabazo ni useless.
-Waache kuweka feature kabla ya kuzifanyia re-search ya kutosha(Kukurupuka)

Useless features.
Tazama face unlock kwenye Samsung galaxy s3/note 3 n.k.
Japo ni simu ya zamani lakini kampuni kubwa kama hii inapaswa kuona mbali zaidi,haina ubishi Samsung galaxy s3 ilifanya mapinduzi makubwa ilipotoka june 2012.
Moja ya feature iliyokuwa nayo hii simu ni pamoja na face unlock,nashindwa kuelewa kwa nini samsung waliweka hii feature,accuracy yake ni mbovu sana nadhani iliwekwa kuwatoa ushamba watu ili kuwapiga pesa vizuri.
maxresdefault.jpg

Face unlock Samsung kwanza waliiweka nadhani hata hawakuifanyia re-search,hii feature kwenye Samsung ilikuwa inaweza kuwa tricked na picha ya kwenye karatasi.
Samsung ilikuwa kwenye competition na apple iPhone lakini sikuona hiko kitu kwa iPhone mpaka tulipokuja kushuhudia kwenye face id yenye security na kutumiwa kwenye payments.
Ni moja ya feature ya kipuuzi ambayo Samsung waliziweka.

Features zingine ni kama smart scroll ile inayo track eye balls zako ukiwa unasoma na smart stay ile inayo pause video ukitazama pembeni.
Sijashuhudia hizi feature kwenye iphone kutokana na kutokua na umuhimu,hata kama tukiuliza watu 100 wenye note 3 tuwaulize wangapi wanatumia smart scroll 10 hawatofika.

Heart beat rate sensor kwenye Samsung galaxy note 4
Samsung hawakuchoka kuweka mapambo kwenye simu zao na sasa ni heart beat sensor ambayo nimeitumia binafsi na haina accuracy,sasa sijui wanaweka kwa nini?
Kuna watu niliona mtandaoni wana complain heart rate sensor inasoma mpaka 150 bpm,hivi ukifikia hii stage utakuwa hata unaona kweli?
Mimi binafsi nilitest unaweza kusoma 67 sasa hivi baada ya dakika ukiweka inasema 104 baadae tena inarudi 65.
this is complete a joke.
Sensor ipo kwenye apple watch ambayo acccuracy yake ni 97%, ambapo hata iphone x haina heart rate sensor.
p1060377.jpg

Kulipuka kwa Samsung galaxy note 7
Samsung kwa mara ya kwanza walisema kuwa ilikuwa ni shoti kwenye circuit na battery lakini baada ya watafiti kufanya hili jaribio kwa hivi vifaa kwa kutumia safe batteries bado simu ilikuwa inachemka sana hivyo kupelekea galaxy note 7 kukatazwa rasmi katika matumizi.
Tatizo lilikuwa kwenye power management features,hii ni simu ya kwanza kabisa kwa Samsung iliyokuwa na USB-C na ilikuwa ina charge only 35 minutes na tayari imejaa,pia ilikuwa na charge ya kawaida kama convertor.
Tatizo lilikuwa ni tokana na uzembe kama vile kuweka 3500mah battery kwenye simu yenye 7.9mm thin, pia kulikuwa na manufacturing problems,nadhani hapo unaona battery ilivyobanwa,yote hii ilikuwa ni kuipa maisha marefu simu katika matumizi ya battery.

Uzembe huu ulipelekea over heating na simu kuripuka ovyo hivyo kuwa hatari zaidi kwa watumiaji.

Pink line
Tuache mambo ya zamani,je Samsung wamejifunza nini nyuma?
Nadhani mmeshuhudia baadhi ya simu hasa s7/s6 edge zikiwa na pink line kwa pembeni mara nyingi upande wa kulia,mara ya kwanza niliona simu ya rafiki yangu nikadhani labda aliiangusha lakini nilizidi kuona watu wa karibu yangu tena kama wa 3 nao simu zao zipo hivyo ikabidi ni fanye re search ndogo kwenye mtandao,sasa huko nilikuta watu wengi wakilalamika hasa kwenye forums za samsung nao simu zao zipo hivyo wala hawajawahi kuziangusha wala kukalia simu bahati mbaya.
Pink line of pixels down edge screen - Android Forums at AndroidCentral.com
Kulikuwa kuna njia tofauti tofauti za ku fix na mara nyingi ilikuwa ni hardware problems,watu wengine ilibidi wazitume Samsung ili kusudi warekebishiwe.
aHR0cDovL21lZGlhLmJlc3RvZm1pY3JvLmNvbS81L1kvNjQ2OTE4L29yaWdpbmFsL215Y2Utc2Ftc3VuZy1nYWxheHktczctZWRnZS1waW5rLWxpbmUtZGlzcGxheS5qcGc=

Binafsi sijafuatilia tatizo linasababishwa na nini lakini hili limetokea ghafla baada ya Samsung kuingia kwenye vioo vya edge,nahisi hawakufanya pia re-search ya kutosha na walikurupuka kama kawaida yao.

Binafsi siku Samsung wakijua kutengeneza simu nitatumia lakini bado wana safari ndefu hasa kushindana na kampuni kama iPhone.
Nimenunua note 7 2016 imelipuka 2017 nanunua edge inaleta pink line utanishauri nini?niendelee kutumia Samsung?

Samsung pink line.PNG

Kuna vitu vingi sana bado sijavizungumza mungu akipenda nitaendelea...............
 
Ko upande wa apple hujaona drawback yoyote?
Kwa upande wangu, Apple wanamiss katika utengenezaji wa Fingerprints. Simu za apple ambazo zipo mikononi mwa watu zinatumika, 50% zimekufa fingerprint.

Huwa nakaa na simu mwaka au zaidi ikibidi na sijawahi kutana na hilo tatizo. Fuatilia unazosema zimekufa touch id utagundua ni zile walizofanyia screen replacements. Zaidi ni vile vya mtaani kwa vioo vya bei nafuu na mafundi wasio na weledi na kazi hiyo.
 
Hizi mistakes unazoona kwenye Samsung usishangae sana hua zinatokea hata kwa apple na companies nyingine, au umeshasahau iPhone 4 ilitoka antenna haifanyi kazi, 6s ilitoka ikiwa inapinda, 8 ikatoka na pink screen.

Huwezi epuka defects kwenye manufacturing, laiti ungejua process yake ilivyo usingekaa uka-criticize. Kutengeneza simu ni kazi ngumu mno, naongea kama mtu niliyefanya kazi kwenye hizi companies kutengeneza components za simu. Face unlock ya apple ni revolutionary ndiyo na better kuliko Samsung ila kuna product nyingi ambazo Samsung nayo ni better, mfano mzuri OLED panels zao hazina mpinzani.
 
Km sikusoma vibaya forums, basi miaka miwili au mitatu mfululizo SAMSUNG huwa anaongoza kwa quality ya simu. Am I wrong?
 
Ko upande wa apple hujaona drawback yoyote?
Kwa upande wangu, Apple wanamiss katika utengenezaji wa Fingerprints. Simu za apple ambazo zipo mikononi mwa watu zinatumika, 50% zimekufa fingerprint.

Mkuu acha uongo, hizo ni zile fake fake au zimefanyiwa screen replacement, mim niko n iphone 6 mwak wa pili sasa na hakuna hilo tatizo, pia simu yenyewe nilinunua used na mtoto kila siku anapambana nayo kuiangusha mpaka home button inacheza cheza lakini fingerprint bado iko poa kabia.
 
Hizi mistakes unazoona kwenye Samsung usishangae sana hua zinatokea hata kwa apple na companies nyingine, au umeshasahau iPhone 4 ilitoka antenna haifanyi kazi, 6s ilitoka ikiwa inapinda, 8 ikatoka na pink screen.

Huwezi epuka defects kwenye manufacturing, laiti ungejua process yake ilivyo usingekaa uka-criticize. Kutengeneza simu ni kazi ngumu mno, naongea kama mtu niliyefanya kazi kwenye hizi companies kutengeneza components za simu. Face unlock ya apple ni revolutionary ndiyo na better kuliko Samsung ila kuna product nyingi ambazo Samsung nayo ni better, mfano mzuri OLED panels zao hazina mpinzani.

Umejibu hoja vizuri sana, big up mkuu. Pamoja na yote lakini Iphone is my brand and my Iphone is my Iphone
 
Umejibu hoja vizuri sana, big up mkuu. Pamoja na yote lakini Iphone is my brand and my Iphone is my Iphone
Mkuu we tumia tu iPhone sio big deal, hata mimi natumia products zote za apple kuanzia simu hadi macbooks kwa sababu ya continuity na privacy kubwa, lakini haimaanishi hao wengine hawapo innovative. Hasa kwenye hardware side apple wako nyuma sana kuliko kampuni nyingine, software tu ndiyo inawabeba, apple ecosystem ipo very well intergrated kiasi kwamba ukiizoea ni ngumu sana kutoka.
 
Kulipuka kwa note 7 inaweza kutokea kwa manufacturer yeyote, pili heart rate sensor kwako inaweza ikawa haina faida lakini kumbuka kuna watu wenye matatizo ya moyo kwao inafaida sana na mtu anaweza akanunua simu kwasababu ya hicho kitu tu.
 
Kha! Sasa waje wafanyeje kwani wameitwa. Ulitaka tuongee ya ccm na cdm, hilijukwaa la tech na hicho ndicho kilichoongelewa shida ikowapi hapo?
Nimesema kuna shida kwani?
Mtoa mada kasema wajifunze, sasa hao sumsung walioambiwa wajifunze hawapaswi kuuona huu ujumbe?
 
Mkuu we tumia tu iPhone sio big deal, hata mimi natumia products zote za apple kuanzia simu hadi macbooks kwa sababu ya continuity na privacy kubwa, lakini haimaanishi hao wengine hawapo innovative. Hasa kwenye hardware side apple wako nyuma sana kuliko kampuni nyingine, software tu ndiyo inawabeba, apple ecosystem ipo very well intergrated kiasi kwamba ukiizoea ni ngumu sana kutoka.

Kweli kutoka kwa apple ni kazi sana, zamani nilikuwa nabadili sana simu ( tecno sijawahi) ila toka nilipoanza kutumia iphone sijawahi hama mpaka leo
 
Yaaani apple funboys nanyinyi mmeanza kuwa na majungu.

Yaani unakuja hapa kutaja simu za miaka minne/mitano nyuma kweli!!!

Tech inabadilika na kuboreka kila siku,ndio maana hata apple kwa sasa wamekuza screen na kuweka dual sim,ingawa mliponda sana.
 
Kweli kutoka kwa apple ni kazi sana, zamani nilikuwa nabadili sana simu ( tecno sijawahi) ila toka nilipoanza kutumia iphone sijawahi hama mpaka leo

Badili hata hiyo ya apple bas kama zingine hutaki.
 
Back
Top Bottom