Samsung Galaxy s7 edge

Nyamwage

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
757
Reaction score
1,866
Hamjambo wakubwa nilikua natoka zangu pemba kikazi kuja Dar home nikashuka Unguja kama saa saba mchana ikabidi nikatembee Pela unguja ili nivute muda ifike saa kumi nipande boti nije Dar nikakutana na maduka yanauza simu za Samsung na iPhone.

Lakini muuzaji aliniambia kua zile simu ni used lakini nilivutiwa nazo hatimae nikanunua Samsung Galaxy s7edge kwa shilingi 280,000 simu naiona iko vizuri sana chaji inajitaidi kukaa lakini kuna jamaa yangu hapa naona ananipa tumbo joto kua nijiandae kulia baadae kua hizi simu used huwa zinazingua.

Hebu wataalam wa masuala haya ya simu niwekeni wazi hizi simu hua zina majanga gani huko mbeleni japo kuwa nilishainunua tayali ili nijiandae kisaikolojia na yajayo.
 
Hiyo simu uliyonunua ndo umefungulia huu uzi.?? kama inaingia Jf usiogope kaa chini piga zako nne endelea kusoma Thread za kula kimasihara.
 
I naweza kuwa nzuri ama mbaya Hakuna guarantee, hio ndio tabia ya vitu used na sio simu tu hata magari, bajaji, laptop, fridge etc.

Cha muhimu usinunue kitu bila warranty, ili ukiipata tatizo ujue PA kurudi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…