Samsung Galaxy S4 Kufungua Kurasa Kwa Macho

Samsung Galaxy S4 Kufungua Kurasa Kwa Macho

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
​
Ikiwa imebaki kama wiki moja kabla ya uzinduzi wa Samsung Galaxy SIV, kuna taarifa kwamba simu hiyo itawawezesha watumiaji kufungua kurasa kwa kutumia macho, hili sio la kushangaza kwani Samsung Galaxy SIII tayari ina sensa inayoweza kutambua kwamba mtuamiaji anatazama skrini na hivyo skirni kutojizima. Uwezo huo wa Galaxy S3 unajulikana kama "smart stay".

Huu ni muendelezo wa haki miliki iliyochukuliwa na Samsung mwezi wa januari mwaka huu, haki miliki hiyo ambayo inajulikana kama "Eye Scroll" ambayo ni haki miliki nambari 011510674 imechukuliwa na kusajiliwa kwa Samsung huko bara la Ulaya. Pia haki miliki hiyo imesajiliwa huko Marekani kama "Samsung Eye Scroll". Vile vile Samsung imepata haki miliki inayojulikana kama "Samsung Eye Pause" ambayo haikuelezewa inatumika vipi.

Ufunguaji wa kurasa huo sio tu kutoka kurasa moja kwenda nyingine bali pia kusogeza kurasa juu unaposoma na kufikia mwisho wa sehemu ya ukurasa inayoonekana skrini. Habari hizi zimeripotiwa na mwandishi wa New York Times anayejulikana kama Brian Chen.

Afisa Mkuu wa Uzalishaji wa Samsung Bwana Kevin Packingham alipoulizwa kuhusu uweo wa simu hiyo kufungua kurasa kwa macho alisema hayuko tayari kuzungumza chochote kwa sasa ingawa amesema simu hiyo itakuwa ni ya aina yake.

Ushindani mkubwa katika Simu za Android umekuwa ukielekea kwenye software ambapo hivi karibuni High Tech Computers (HTC) walitoa Simu yao HTC One ikiwa na HTC Sense 5 na Blink Feed huku kampuni mbali mbali zikitumia "skin" katika OS hiyo katika jaribio la kujitofautisha na Android ya kawaida (Stock Android).

Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia

 
Mmmh! Yetu macho. Usiwe ukawa unatupiga changa.
 
samsung wanazingua, yani hata S3 haijachokwa sokoni wanaleta mpya.
 
afu mbaya zaidi simu zinakua na specification tofauti uki-compare na iphone wao wanabadili majina na sio specification.
 
Kweli Samsung wanatuchezea. Mimi nina Galaxy III hata sijaichoka ni mpya na upya wake saa wanataka tena niiache? Kwa hakika hisi technologia zinatakiwa zifungwe speed governor kidogo.
 
Kuuliza sio ujinga hivi galaxy 3 na 2 ipi ipo juu maana tulikuwa tunabishana na watu tukakosa conclussion
 
afu mbaya zaidi simu zinakua na specification tofauti uki-compare na iphone wao wanabadili majina na sio specification.
mama mbona unawalaumu samsung....apple mbona alitoa i phone 4,4s na 5..????
halafu kama umeshawah kusoma theory inaitwa Moore's law ungeelewa kwanin smartphone zinatoka kila mwaka
 
duh yaani nilikuwa nachanga ninunue s3 inakuja s4? ngoja niisubirie tu sina jinsi isee na ndio itakuwa ya mwisho sitanunua tena wanatizungua sana
 
Wanatupeleka wapi! Yana unepekua, kurasa za cm kwa macho! Balaa aisee
 
Samsung ni watovu wa nidhamu, hivi juzi wameonyesha skrini mpya zinazopinda sasa wamekuja na control ya macho. Dunia kweli inazunguka.
 
Back
Top Bottom