GE2025 Samia: Tutatoa ruzuku ya Pembejeo bure na kutafuta masoko ya korosho ili kuongeza tija kwa wakulima

GE2025 Samia: Tutatoa ruzuku ya Pembejeo bure na kutafuta masoko ya korosho ili kuongeza tija kwa wakulima

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa endapo atapata ridhaa ya wananchi, serikali yake itaendelea kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima ili kuendeleza sekta ya kilimo nchini.

Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo leo Septemba 25, 2025 wakati akinadi sera zake kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Mchinga, mkoani Lindi, ambapo amesisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha wakulima wa zao la korosho wanapata mbolea na pembejeo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.

Aidha, amesema serikali yake itaendelea kutafuta masoko ya korosho ili kuongeza tija kwa wakulima.

 
Ukiwa mgeni nchi hii unaweza ukadhani yeye siyo raisi naye ana usaka urais, na unaweza kudhani korosho ni zao jipya Tanganyika.

Hahaha alafu kuna watu wanasikiliza na kushangilia.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Imefikia hatua yaan kila anachokizungumza naona anadanganya hivi ni mimi peke yangu au tupo wengi tunaowaza hivi??
 
Back
Top Bottom