GE2025 Samia: Tanzania tutaijenga wanawake na wanaume, acheni ubaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza suala la mshikamano na umoja miongoni mwa watanzania pamoja na kuachana na imani, tamaduni na mila zenye kuwakandamiza wanawake na kuamini kuwa hawafai katika Uongozi.

Dkt. Samia ametoa rai hiyo leo Ijumaa Oktoba 10, 2025 Wilayani Serengeti Mkoani Mara kwenye Viwanja vya Mwenge wakati wa Mkutano wake wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, akionesha kusikitishwa na baadhi ya watu walioanza maneno ya ubaguzi dhidi ya wagombea Ubunge wanawake wa Majimbo ya Mkoa huo, wakidai kuwa hawawezi kuongozwa na wanawake.

"Mimi ninayesema hapa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya miaka minne nimefanya makubwa sana sasa ingekuwa mwanamke hawezi nisingeweza kuyafanya, Mungu alituumba wote na akili sawa, akatupa na uwezo wa kufikiri, ukiwa mwanamke unafikiri, ukiwa mwanaume unafikiri, tena mwanamke mwaminifu zaidi na mtendaji zaidi kwasababu ya uoga kuliko mwanaume." Amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia amesisitiza kuwa kwenye maendeleo hakuna jinsia na kwamba Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla itajengwa na watu wote, akisema la muhimu ni Utanzania wa kila mmoja na kushikamana kama ambavyo waasisi wa Taifa la Tanzania walivyohimiza muda wote kutaka jamii kushikamana.

Dkt. Samia katika maelzo yake amewaomba pia wananchi wa Serengeti kuwachagua wagombea Ubunge, Udiwani na Yeye mwenyewe katika nafasi ya Urais wa Tanzania, akikumbusha kuwa kwake binafsi wapo wengi waliokuwa wakimbeza wakati anaingia madarakani mwaka 2021 kutokana na jinsia yake na miaka minne baadaye simulizi zimekuwa tofauti, za sasa zikijaa mafanikio na matumaini makubwa kwake kutokana na umahiri na uchapakazi aliouonesha katika kipindi chake cha awamu ya sita.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…