Samia Suluhu iunde CCM Upya

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Watanzania wa umri wangu kurudi nyuma, wote kwa wakati fulani tuliwahi kuwa wanachama wa CCM, iwe kwa kutaka au bila hiari, kwa kujiunga au kuungishwa, kwa kuelewa au bila ya kuelewa.

Nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi, nilikuwa kiongozi wa chipukizi wa Wilaya na Mkoa. Ni wakati huo ndiyo nilipata nafasi ya kushikana mkono na Mwalimu Nyerere kwa mara ya kwanza. Wala hatukujua chochote kuhusiana na mfumo wa vyama vingi au utofauti kati ya serikali na CCM. CCM ilikuwa ndiyo serikali, wakati fulani ndiyo mahakama. Kuna wakati uliwasikia watu wakisema, naona unanionea, nitakupeleka CCM (kushtaki).

Nilipomaliza kidato cha sita, na division one yangu yangu ya PCM, nilienda JKT. Huko kulikuwa na posho ya kila mwezi. Posho ya mwezi mmoja ilikatwa, bila ya hiari, tukaambiwa ni kulipia kadi ya chama (CCM). Huulizwi bali unapewa tu kadi. Na wakati huo mkuu wa kikosi (CO) alikuwa ndiye mwenyekiti wa tawi la chama kikosini. Hachaguliwi, bali anakuwa mwenyekiti kwa nafasi yake ya kuwa CO. Siku ambayo CO aliitisha mkutano wa tawi, na yeye akiwa kama mwenyekiti wa tawi, tulifurahia sana maana yeye mwenyewe angeanza kwa kutamka, leo jeshi lipo pembeni, tunazungumza kama wanachama. Ndiyo siku ambayo unaruhusiwa kuzungumza chochote bila ya hofu ya kupigwa drill. Kipindi hicho kinakoma pale unapoambiwa, Jeshi linarudia kwenye nafasi yake. Baada ya historia hii fupi, nije kwenye hoja:

Kuna wakati CCM iliaminiwa, ilipendwa na ilionekana ni tumaini. Hali hiyo iliendelea kupotea taratibu, na msumari wa mwisho mbaya kabisa ulipigiliwa wakati wa uongozi wa Mwenyekiti Hayati Magufuli.

Kipindi cha Magufuli:

1) Demokrasia ndani ya CCM ilitupwa. Siasa za hoja na ushawishi zilifutwa, na CCM ilitekwa na watu wachache, na kuifanya CCM kuwa kikundi kilichotofautiana kidogo sana na makundi ya kigaidi. Greenguards ikawa ndiyo kinu cha kutengenezea wahalifu. Humo ndimo walimotokea akina Sabaya, Makonda, Gumo, Hapi, na the like, ambao matendo yao, sote tunayajua.

2) Maamuzi yaliondolewa kutoka kwenye vikao (kama mwalimu Nyerere alivyosisitiza), na kupelekwa kwa Mwenyekiti na watu wake wachache. Mfano mzuri ni kura za maoni 2020 ambapo robo tatu ya wagombea wote waliopitishwa na wajumbe, majina yao yalikatwa. Kimsingi, wagombea wote wa CCM waliteuliwa na watu wachache badala ya kupitishwa na wajumbe kama katiba ya chama inavyotamka.

3) CCM taratibu ilipelekwa kuwa taasisi ya dola, ikitegemea zaidi nguvu za polisi na vyombo vingine vya ulinzi. Kati ya taasisi za serikali ambazo wananchi wengi hawaridhishwi na utendaji wake (hata Rais aliwahi kuonya matendo ya polisi ya kubambikia watu kesi, watuhumiwa kuuawa kwenye mahabusu za polisi, etc) ni jeshi la Polisi. Kitendo hicho kinafanya chuki dhidi ya polisi kuwa pia chuki dhidi ya CCM. Ni lazima CCM ijinasue, itoke kwenye mgongo wa Polisi.

CCM kwa sasa, siyo chama chenye hoja wala ushawishi, kinaishi kwa kutegemea mgongo wa Polisi. Hali hii inaipeleka CCM kwenye kifo cha jumla. Kama Rais Samia anaipenda CCM, ni lazima aiunde CCM upya. Aifanye CCM kuwa chama cha siasa, na siyo genge la wahuni, au sehemu ya kundi la watu wasiojulikana. Asipofanya hivyo, ni suala la wakati, lazima CCM itakuja kufa (simaanishi kushindwa kwenye uchaguzi, jambo ambalo ni la kawaida kwa chama cha siasa, bali kufa na kupotea baada ya kupoteza dola).
 
Magufuli mwehu Sana eti Chama cha Majambazi kilibadilika na kuitwa CCM ya Magufuli.
Jamaaa liliwa brain wash watu.
Sisim inatakiwa ifanyiwe overhaul na ikibidi ibadilishwe na Jina.
Jiwe alikinajisi Sana hicho chama
 
Asante Kwa madini yenye historian na uzoefu wa maisha, namna hii wangekuwa wasikivu wengine wasingekuwa nyuma ya nondo Leo hii.
 
Wabunge wa Arusha wamewakilisha vizuri

Wabunge wa Kilimanjaro, walikosa agenda ya Pamoja ya kumwambia Rais..kuna biashara zao la kahawa, pembejeo za kuliko kupanda, Parachichi, yaani uchumi kwa ujumla

Professor Mkenda Mbunge wa Rombo, amejikita zaidi kwenye uwaziri...Mbunge wa Rombo..haangalii kero za wanarombo.

Mbunge wa Rombo, amekumbatia matajiri kama Mramba.... Mashamba yaliyovunwa miti, matajiri wanagawana. Wajane na wamama , vijana wanandikishwa majina Kila mwaka, hawapewi hata Eka Moja

Matajiri wanahodhi hayo mashamba, Eka 5 mpaka 30. Hapo iangaliwe pia na Rushwa, PCCB IKO KIMYA

Professor Mkenda, hujui hayo mambo? Basi husikilizi kero za wajane Tarakea..tena sehemu uliyozaliwa
 
Watanzania wa umri wangu kurudi nyuma, wote kwa wakati fulani tuliwahi kuwa wanachama wa CCM, iwe kwa kutaka au bila hiari, kwa kujiunga au kuungishwa, kwa kuelewa au bila ya kuelewa.

Nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi, nilikuwa kiongozi wa chipukizi wa Wilaya na Mkoa. Ni wakati huo ndiyo nilipata nafasi ya kushikana mkono na Mwalimu Nyerere kwa mara ya kwanza. Wala hatukujua chochote kuhusiana na mfumo wa vyama vingi au utofauti kati ya serikali na CCM. CCM ilikuwa ndiyo serikali, wakati fulani ndiyo mahakama. Kuna wakati uliwasikia watu wakisema, naona unanionea, nitakupeleka CCM (kushtaki).

Nilipomaliza kidato cha sita, na division one yangu yangu ya PCM, nilienda JKT. Huko kulikuwa na posho ya kila mwezi. Posho ya mwezi mmoja ilikatwa, bila ya hiari, tukaambiwa ni kulipia kadi ya chama (CCM). Huulizwi bali unapewa tu kadi. Na wakati huo mkuu wa kikosi (CO) alikuwa ndiye mwenyekiti wa tawi la chama kikosini. Hachaguliwi, bali anakuwa mwenyekiti kwa nafasi yake ya kuwa CO. Siku ambayo CO aliitisha mkutano wa tawi, na yeye akiwa kama mwenyekiti wa tawi, tulifurahia sana maana yeye mwenyewe angeanza kwa kutamka, leo jeshi lipo pembeni, tunazungumza kama wanachama. Ndiyo siku ambayo unaruhusiwa kuzungumza chochote bila ya hofu ya kupigwa drill. Kipindi hicho kinakoma pale unapoambiwa, Jeshi linarudia kwenye nafasi yake. Baada ya historia hii fupi, nije kwenye hoja:

Kuna wakati CCM iliaminiwa, ilipendwa na ilionekana ni tumaini. Hali hiyo iliendelea kupotea taratibu, na msumari wa mwisho mbaya kabisa ulipigiliwa wakati wa uongozi wa Mwenyekiti Hayati Magufuli.

Kipindi cha Magufuli:

1) Demokrasia ndani ya CCM ilitupwa. Siasa za hoja na ushawishi zilifutwa, na CCM ilitekwa na watu wachache, na kuifanya CCM kuwa kikundi kilichotofautiana kidogo sana na makundi ya kigaidi. Greenguards ikawa ndiyo kinu cha kutengenezea wahalifu. Humo ndimo walimotokea akina Sabaya, Makonda, Gumo, Hapi, na the like, ambao matendo yao, sote tunayajua.

2) Maamuzi yaliondolewa kutoka kwenye vikao (kama mwalimu Nyerere alivyosisitiza), na kupelekwa kwa Mwenyekiti na watu wake wachache. Mfano mzuri ni kura za maoni 2020 ambapo robo tatu ya wagombea wote waliopitishwa na wajumbe, majina yao yalikatwa. Kimsingi, wagombea wote wa CCM waliteuliwa na watu wachache badala ya kupitishwa na wajumbe kama katiba ya chama inavyotamka.

3) CCM taratibu ilipelekwa kuwa taasisi ya dola, ikitegemea zaidi nguvu za polisi na vyombo vingine vya ulinzi. Kati ya taasisi za serikali ambazo wananchi wengi hawaridhishwi na utendaji wake (hata Rais aliwahi kuonya matendo ya polisi ya kubambikia watu kesi, watuhumiwa kuuawa kwenye mahabusu za polisi, etc) ni jeshi la Polisi. Kitendo hicho kinafanya chuki dhidi ya polisi kuwa pia chuki dhidi ya CCM. Ni lazima CCM ijinasue, itoke kwenye mgongo wa Polisi.

CCM kwa sasa, siyo chama chenye hoja wala ushawishi, kinaishi kwa kutegemea mgongo wa Polisi. Hali hii inaipeleka CCM kwenye kifo cha jumla. Kama Rais Samia anaipenda CCM, ni lazima aiunde CCM upya. Aifanye CCM kuwa chama cha siasa, na siyo genge la wahuni, au sehemu ya kundi la watu wasiojulikana. Asipofanya hivyo, ni suala la wakati, lazima CCM itakuja kufa (simaanishi kushindwa kwenye uchaguzi, jambo ambalo ni la kawaida kwa chama cha siasa, bali kufa na kupotea baada ya kupoteza dola).
 
Attachments

  • FB321251-28F3-4ECA-AC78-D88496015849.jpeg
    FB321251-28F3-4ECA-AC78-D88496015849.jpeg
    72.5 KB · Views: 1
Ccm hii hii iliyokuwa imejifia kabla ya kuhuishwa na Hayati Magufuli, au nyingine? Ccm hii hii ambayo ilikuwa kichaka cha biashara ya unga na ufisadi wa kutisha enzi za Kikwete na Kinana?
Nakuapia, as far as Kikwete na kinana bado wako hai na wana influence kwenye chama, ccm haiwezi kurekebishwa au kuundika upya. Labda kama ni kuharibika zaidi. Mwenyekiti Samia mtamlaumu bure tu.
 
Watanzania wa umri wangu kurudi nyuma, wote kwa wakati fulani tuliwahi kuwa wanachama wa CCM, iwe kwa kutaka au bila hiari, kwa kujiunga au kuungishwa, kwa kuelewa au bila ya kuelewa.

Nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi, nilikuwa kiongozi wa chipukizi wa Wilaya na Mkoa. Ni wakati huo ndiyo nilipata nafasi ya kushikana mkono na Mwalimu Nyerere kwa mara ya kwanza. Wala hatukujua chochote kuhusiana na mfumo wa vyama vingi au utofauti kati ya serikali na CCM. CCM ilikuwa ndiyo serikali, wakati fulani ndiyo mahakama. Kuna wakati uliwasikia watu wakisema, naona unanionea, nitakupeleka CCM (kushtaki).

Nilipomaliza kidato cha sita, na division one yangu yangu ya PCM, nilienda JKT. Huko kulikuwa na posho ya kila mwezi. Posho ya mwezi mmoja ilikatwa, bila ya hiari, tukaambiwa ni kulipia kadi ya chama (CCM). Huulizwi bali unapewa tu kadi. Na wakati huo mkuu wa kikosi (CO) alikuwa ndiye mwenyekiti wa tawi la chama kikosini. Hachaguliwi, bali anakuwa mwenyekiti kwa nafasi yake ya kuwa CO. Siku ambayo CO aliitisha mkutano wa tawi, na yeye akiwa kama mwenyekiti wa tawi, tulifurahia sana maana yeye mwenyewe angeanza kwa kutamka, leo jeshi lipo pembeni, tunazungumza kama wanachama. Ndiyo siku ambayo unaruhusiwa kuzungumza chochote bila ya hofu ya kupigwa drill. Kipindi hicho kinakoma pale unapoambiwa, Jeshi linarudia kwenye nafasi yake. Baada ya historia hii fupi, nije kwenye hoja:

Kuna wakati CCM iliaminiwa, ilipendwa na ilionekana ni tumaini. Hali hiyo iliendelea kupotea taratibu, na msumari wa mwisho mbaya kabisa ulipigiliwa wakati wa uongozi wa Mwenyekiti Hayati Magufuli.

Kipindi cha Magufuli:

1) Demokrasia ndani ya CCM ilitupwa. Siasa za hoja na ushawishi zilifutwa, na CCM ilitekwa na watu wachache, na kuifanya CCM kuwa kikundi kilichotofautiana kidogo sana na makundi ya kigaidi. Greenguards ikawa ndiyo kinu cha kutengenezea wahalifu. Humo ndimo walimotokea akina Sabaya, Makonda, Gumo, Hapi, na the like, ambao matendo yao, sote tunayajua.

2) Maamuzi yaliondolewa kutoka kwenye vikao (kama mwalimu Nyerere alivyosisitiza), na kupelekwa kwa Mwenyekiti na watu wake wachache. Mfano mzuri ni kura za maoni 2020 ambapo robo tatu ya wagombea wote waliopitishwa na wajumbe, majina yao yalikatwa. Kimsingi, wagombea wote wa CCM waliteuliwa na watu wachache badala ya kupitishwa na wajumbe kama katiba ya chama inavyotamka.

3) CCM taratibu ilipelekwa kuwa taasisi ya dola, ikitegemea zaidi nguvu za polisi na vyombo vingine vya ulinzi. Kati ya taasisi za serikali ambazo wananchi wengi hawaridhishwi na utendaji wake (hata Rais aliwahi kuonya matendo ya polisi ya kubambikia watu kesi, watuhumiwa kuuawa kwenye mahabusu za polisi, etc) ni jeshi la Polisi. Kitendo hicho kinafanya chuki dhidi ya polisi kuwa pia chuki dhidi ya CCM. Ni lazima CCM ijinasue, itoke kwenye mgongo wa Polisi.

CCM kwa sasa, siyo chama chenye hoja wala ushawishi, kinaishi kwa kutegemea mgongo wa Polisi. Hali hii inaipeleka CCM kwenye kifo cha jumla. Kama Rais Samia anaipenda CCM, ni lazima aiunde CCM upya. Aifanye CCM kuwa chama cha siasa, na siyo genge la wahuni, au sehemu ya kundi la watu wasiojulikana. Asipofanya hivyo, ni suala la wakati, lazima CCM itakuja kufa (simaanishi kushindwa kwenye uchaguzi, jambo ambalo ni la kawaida kwa chama cha siasa, bali kufa na kupotea baada ya kupoteza dola).
Unataka alogwe ?
 
Hapo kwa CCM kuanguka chini ya Magufuli,umetupiga kamba.CCM ilianza kufia mikononi mwa Kikwete hasa kipindi kile Makamba akiwa Katibu Mkuu kuelekea 2010 ambapo tulishuhudia Kikwete Family ikiendesha kampeni za uchaguzi Mkuu wa Rais.Awamu ya nne ata ukivaa shati au T-shirt ya CCM mtaani unazomewa!
Heshima ya CCM ilianza kurejea taratibu baada ya Kinana kurejeshwa kuwa Katibu Mkuu na Mangula kuteuliwa Makamu Mwenyekiti wa CCM 2012.
Kuanzia 2015 chini ya Magufuli na Bashiru,heshima ya CCM ilirejea kwa kiwango kikubwa sana mpaka 2021,ila kwa sasa naona CCM is returning back to square 1.
I stand to be corrected!
 
Watanzania wa umri wangu kurudi nyuma, wote kwa wakati fulani tuliwahi kuwa wanachama wa CCM, iwe kwa kutaka au bila hiari, kwa kujiunga au kuungishwa, kwa kuelewa au bila ya kuelewa.

Nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi, nilikuwa kiongozi wa chipukizi wa Wilaya na Mkoa. Ni wakati huo ndiyo nilipata nafasi ya kushikana mkono na Mwalimu Nyerere kwa mara ya kwanza. Wala hatukujua chochote kuhusiana na mfumo wa vyama vingi au utofauti kati ya serikali na CCM. CCM ilikuwa ndiyo serikali, wakati fulani ndiyo mahakama. Kuna wakati uliwasikia watu wakisema, naona unanionea, nitakupeleka CCM (kushtaki).

Nilipomaliza kidato cha sita, na division one yangu yangu ya PCM, nilienda JKT. Huko kulikuwa na posho ya kila mwezi. Posho ya mwezi mmoja ilikatwa, bila ya hiari, tukaambiwa ni kulipia kadi ya chama (CCM). Huulizwi bali unapewa tu kadi. Na wakati huo mkuu wa kikosi (CO) alikuwa ndiye mwenyekiti wa tawi la chama kikosini. Hachaguliwi, bali anakuwa mwenyekiti kwa nafasi yake ya kuwa CO. Siku ambayo CO aliitisha mkutano wa tawi, na yeye akiwa kama mwenyekiti wa tawi, tulifurahia sana maana yeye mwenyewe angeanza kwa kutamka, leo jeshi lipo pembeni, tunazungumza kama wanachama. Ndiyo siku ambayo unaruhusiwa kuzungumza chochote bila ya hofu ya kupigwa drill. Kipindi hicho kinakoma pale unapoambiwa, Jeshi linarudia kwenye nafasi yake. Baada ya historia hii fupi, nije kwenye hoja:

Kuna wakati CCM iliaminiwa, ilipendwa na ilionekana ni tumaini. Hali hiyo iliendelea kupotea taratibu, na msumari wa mwisho mbaya kabisa ulipigiliwa wakati wa uongozi wa Mwenyekiti Hayati Magufuli.

Kipindi cha Magufuli:

1) Demokrasia ndani ya CCM ilitupwa. Siasa za hoja na ushawishi zilifutwa, na CCM ilitekwa na watu wachache, na kuifanya CCM kuwa kikundi kilichotofautiana kidogo sana na makundi ya kigaidi. Greenguards ikawa ndiyo kinu cha kutengenezea wahalifu. Humo ndimo walimotokea akina Sabaya, Makonda, Gumo, Hapi, na the like, ambao matendo yao, sote tunayajua.

2) Maamuzi yaliondolewa kutoka kwenye vikao (kama mwalimu Nyerere alivyosisitiza), na kupelekwa kwa Mwenyekiti na watu wake wachache. Mfano mzuri ni kura za maoni 2020 ambapo robo tatu ya wagombea wote waliopitishwa na wajumbe, majina yao yalikatwa. Kimsingi, wagombea wote wa CCM waliteuliwa na watu wachache badala ya kupitishwa na wajumbe kama katiba ya chama inavyotamka.

3) CCM taratibu ilipelekwa kuwa taasisi ya dola, ikitegemea zaidi nguvu za polisi na vyombo vingine vya ulinzi. Kati ya taasisi za serikali ambazo wananchi wengi hawaridhishwi na utendaji wake (hata Rais aliwahi kuonya matendo ya polisi ya kubambikia watu kesi, watuhumiwa kuuawa kwenye mahabusu za polisi, etc) ni jeshi la Polisi. Kitendo hicho kinafanya chuki dhidi ya polisi kuwa pia chuki dhidi ya CCM. Ni lazima CCM ijinasue, itoke kwenye mgongo wa Polisi.

CCM kwa sasa, siyo chama chenye hoja wala ushawishi, kinaishi kwa kutegemea mgongo wa Polisi. Hali hii inaipeleka CCM kwenye kifo cha jumla. Kama Rais Samia anaipenda CCM, ni lazima aiunde CCM upya. Aifanye CCM kuwa chama cha siasa, na siyo genge la wahuni, au sehemu ya kundi la watu wasiojulikana. Asipofanya hivyo, ni suala la wakati, lazima CCM itakuja kufa (simaanishi kushindwa kwenye uchaguzi, jambo ambalo ni la kawaida kwa chama cha siasa, bali kufa na kupotea baada ya kupoteza dola).
CCM IKO IMARA SANA SANA.
 
Back
Top Bottom