MTENDAHAKI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,013
- 1,448
Mimi ni kati ya wanao, wanazi wako (Kuliko mdogo wangu P Makonda). Nikupongeze kwa ushupavu uliouonyesha kwenye kampeni mpaka sasa.
Pamoja na yote haya nakuomba ufanye jambo hili, "Zungumza na wanawake akiwemo mama yangu"!Waambie namna ambavyo utahakikisha 50/50 inapatikana, waeleze wewe ni kielelezo, waambie umechoka kuona wanalal chini hospitali na unajulijua tatizo hilo na huogopi kulisema waziwazi na wewe ndiye mwarobaini wao, waambie miaka hamsini ya Tanzania kutokuwa na mama katika ngazi ya juu imekoma.
Waambie mama ni usafi wa nyumba na moyo wa familia na kwa mara ya kwanza nchi hii ina midundo dhahiri ya uhai kutokana na msukumo thabiti wa damu kutoka kwenye moyo.
Makonda alikupachika jina zuri lililoungwa mkono na mzee pinda na bila shaka sasa naamini tuna ulinzi wa uhakika wa familia. Waambie wake zetu ujumbe utatufikia tu, waambie wasikosee kuchagua watatueleza na sie waambie kila jambo lina sababu na sasa wewe ni sababu ya mabadiliko.
Naamini nimesikika najua hupiti humu lakini kuna watu watakuletea ujumbe wangu. Mimi kura yangu inajulikana ni kwa Magufuli ili nisihofie watoto wangu kukosa matibabu ya uhakika, ili mke wangu ajifungue salama, ili bibi zangu watibiwe bure ili nikae kwenye nchi ya amani na utulivu.