tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuimarisha sekta za maji na nishati endapo atapewa ridhaa kuendelea kuongoza nchi.
Chanzo: ITV
"Kwa upande wa maji tumefanya lakini bado tunajua kuna maeneo ambayo maji hayajafika, tutaendelea na miradi yetu miji 28 na uchimbaji wa visima, lakini kubwa zaidi ni ule mradi mkubwa wa kutoka Ziwa Victoria maji yapite Singida yaende mpaka Dodoma.
Mradi ule utakwenda kumaliza shida zote, sasa fedha tutatoa wapi mimi na yeye tutajua, tuliahidi tunakwenda kuweka umeme Vijiji vyote, tumemaliza na sasa tunaunganisha kwenye vitongoji, tumepeleka umeme mpaka kwa wachimbaji ili wapate urahisi wa kuchimba na uchumi ukue haraka haraka, kwa hiyo tutaendelea na kazi ya kupeleka nishati ya umeme kwa wananchi wa Tanzania."