Samia: Mohammed Interprises na WATCO kazi imewashida

Samia: Mohammed Interprises na WATCO kazi imewashida

Hahahah!! Kweli nyani aoni kundule. Yy pia nae kashindwa nchi.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Mgombea wa kiti Cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali inaenda kufanya tathimini ya Mashamba ya chai ambayo waliwapatia sekta Binafsi ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) na kampuni ya Wakulima Tea Company (WATCO)kutokana na kushindwa mikataba ya uwekezaji ya kuongeza thamani Chai

Dkt. Samia ameyasema hayo Leo Sept 5,2025 katika uwanja wa Tandare uliopo mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe jijini Mbeya Kwenye muendelezo wa Mikutano yake ya Hadhara ya Kampeni za uchaguzi Mkuu 2025

Dkt. Samia amesema kuwa inavyoonekana kampuni hizo kazi hiyo imewashinda hivyo kinachofanyika sasa Serikali imeunda Timu ya kuyafanyia tathimini mashamba na viwanda lengo likiwa ni kuyachukua Mashama hayo pamoja na viwanda ili kuvimilikisha kwenye vyama vya Ushirika.
Kwa hiyo mpaka awe rais kwa Muhula mwingine ndo atatue matatizo hayo? Elimu ni vazi la akili.
 
Habari zilizopo , ni kuwa hii serikali ambayo uwezekano mkubwa atashinda Samia, ambaye atachaguliwa na wananchi wachache sana, Ina mipango ya kiwakomesha wafanyabiashara wakubwa ambao hawakuchanga kampeni za CCM.

Hofu hiyo imetanda hasa baada ya mama Samia Kusema hadharani kuwa atampokonya Mo dewji mashamba na viwanda ambavyo alimilikishwa na serikali ya CCm. Mo dewji tajiri namba moja , hakuweka mchango akiwa yeye kama mo, Bali ni kina Azim dewji na family members walitoa pesa kidogo around 150-300m, Mo kama Mo hakuonekana kutoa.

Hali hii pia ya Mo kutotoa pesa za kutosha na Kwa jina lake, itasababisha matatizo makubwa pale Simba, na siioni Makolo wakipata Saport ya Samia au Serikali ya CCm, na naweza SEMA yanga Bingwa

Hivyo, wafanyabiashara wakubwa nawaambieni dirisha bado lipo wazi pelekeni pesa
 
Mgombea wa kiti Cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali inaenda kufanya tathimini ya Mashamba ya chai ambayo waliwapatia sekta Binafsi ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) na kampuni ya Wakulima Tea Company (WATCO)kutokana na kushindwa mikataba ya uwekezaji ya kuongeza thamani Chai

Dkt. Samia ameyasema hayo Leo Sept 5,2025 katika uwanja wa Tandare uliopo mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe jijini Mbeya Kwenye muendelezo wa Mikutano yake ya Hadhara ya Kampeni za uchaguzi Mkuu 2025

Dkt. Samia amesema kuwa inavyoonekana kampuni hizo kazi hiyo imewashinda hivyo kinachofanyika sasa Serikali imeunda Timu ya kuyafanyia tathimini mashamba na viwanda lengo likiwa ni kuyachukua Mashama hayo pamoja na viwanda ili kuvimilikisha kwenye vyama vya Ushirika.
Hapa mchango harambee haukutoka. Hii ni maajabu
 
Nahisi akuenda kwenye ile gala pale mlimani city
 
Hii ndo Tanzania, au Bhai itakuwa anachukulia mikopo nini?
 
Uongo tu kulagai wananchi huyu Dewiji si chawa wake anaweza vipi kumpokonya mashamba?
Sasa mkuu wa nchi kaongea hadharani wewe unasema uongo? Nilidhani busara ya akili unge save hii uone kama Mo akikaidi hatanyooshwa? Usicheze na taasisi ya Rais. Akisema hadharani kitu ni ama ujirekebishe haraka au usombwe na mafuriko.
 
Back
Top Bottom