GE2025 Samia: Mkituchagua tutakamilisha vituo vya Afya Nakapanya

GE2025 Samia: Mkituchagua tutakamilisha vituo vya Afya Nakapanya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumanne Septemba 23, 2025, ameendelea na kampeni zake katika eneo la Nakapanya, mkoani Ruvuma.

Akizungumza kwenye mkutano uliohudhuriwa na wananchi, Dkt. Samia alisema endapo atapewa ridhaa ya kuendelea kuongoza baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, serikali yake itaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma muhimu za kijamii.

Katika hotuba yake, Dkt. Samia ameahidi ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Namiungo pamoja na kukamilisha zahanati iliyo katika eneo hilo. Pia amegusia changamoto ya upatikanaji wa maji, akieleza kuwa ni moja ya maeneo yaliyoainishwa kwenye Ilani ya CCM, ambayo inalenga kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi na salama.

Dkt. Samia amesema dhamira ya kuimarisha huduma hizo ni sehemu ya kulinda hadhi na utu wa Mtanzania, akisisitiza kuwa azma hiyo itabaki kuwa kipaumbele endapo ataendelea kuongoza serikali baada ya uchaguzi.
 
Miaka zaidi ya 8 alikuwa anakamilisha kituo cha afya ikulu😀 na ziara za nje kujenga vituo vya afya vya uingereza na USA
 
ccmtanzania_0e488f988f4f4ec6b7fbdef6e8a97fe3.jpg
 
Back
Top Bottom