Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mgombea Urais wa CCM Dk. Samia Suluhu Hassan amesema tangu kuanza kwa mpango wa serikali wa kutoa ruzuku za mbolea pamoja na pembejezo za Kilimo mwaka 2021/22, serikali imetumia takribani Sh. Bilioni 726 kwaajili ya kunufaisha wakulima wa Tanzania.
Akiomba kura kwa mamia ya wananchi wa Mtwara leo Septemba 26, 2025 Dk. Samia ameeleza dhamira yake ikiwa wananchi wataendelea kukipa ridhaa Chama Cha Mapinduzi ni kuendelea kuongeza kiwango hicho cha ruzuku ili kukuza uzalishaji na kuongeza tija kwa wakulima.
"Tunatumia Sh. Bilioni 152 kila mwaka fedha ambayo ingetoka mfukoni kwa mkulima lakini tumeibakisha mifukoni kwao na serikali tunagawa kwa ruzuku ya nusu bei na pembejeo nyingine ni bure kabisa kama salfa, dawa za kuulia wadudu na blight na tunafanya hivyo kwasababu tumedhamiria kukuza kilimo na uzalishaji wa Korosho.
"Kwa hakika uzalishaji tumeuona ikiwemo kwenye zao la korosho kutoka tani 118, 811 mwaka 2020/21 zikiwa na thamani ya Sh. Bilioni 265 na leo mwaka 2024/25 tunazungumzia uzalishaji wa tani 330, 505 zikiuzwa Sh. Trilioni moja na Bilioni 900." amesema Dk. Samia.
Chanzo: Nipashe