GE2025 Samia aahidi kujenga barabara za lami Kilimanjaro

GE2025 Samia aahidi kujenga barabara za lami Kilimanjaro

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ameahidi kuendelea kuufungua Mkoa wa Kilimanjaro kwa miundombinu ya barabara za lami, zege na changarawe ili kusisimua uchumi wa mkoa huo na kukuza biashara ya kimataifa kati ya Kanda ya Kaskazini na Nchi jirani.

Dkt. Samia ameyaeleza hayo leo Jumatano Oktoba Mosi, 2025 wakati wa mkutano wake wa kampeni Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro kwenye Viwanja vya Mashujaa, wakati wa mkutano wake wa kwanza mkoani humo akitokea mkoani Tanga, akisema miongoni mwa barabara zitazojengwa ni pamoja na barabara ya Holili- Tarakea yenye urefu wa Kilomita 53 ikitajwa kukuza biashara kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kuondoa foleni ya malori kwenye barabara ya Mwika- Tarakea.

Ameahidi pia kuendelea na ujenzi wa barabara ya mchepuko ya Kae- Airport yenye urefu wa Kilomita 31 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa barabara za ndani ya Mji wa Moshi kupitia mradi wa uendelezaji Miji Tanzania maarufu kama TACTIC pamoja na kukamilisha barabara ya Moshi International school- Kibosho Kati- Kwa Raphael yenye urefu wa Kilomita 13.

Aidha Dkt. Samia amezungumzia pia ujenzi wa barabara nyingine kwenye Wilaya za Rombo na Moshi Vijijini, Akiahidi pia kushughulikia ujenzi wa barabara za viwango vya lami na zege kwenye Wilaya ya Same maeneo ya Milimani ili kuzifanya barabara za Wilaya hiyo kuweza kupitika kwenye msimu ya mvua.

 
Back
Top Bottom