JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
TUTATOKA TU - HEDARU SAME
Wiki hii ilikuwa ni kutengeneza barabara umbali wa km. 3 kwa kumwaga moram na kuisambaza katika kitongoji cha Mbuyuni B kijiji cha Hedaru kata ya Hedaru. Barabara hiyo ni ya mtaa inaelekea kijiji cha Makasa umbali wa Km. 30 kutoka Hedaru.
Wananchi wa kitongoji hicho walimuomba DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule aridhie ombi lao la kuiita barabara hiyo kwa jina lake. DC awapongeza kwa kujitokeza wakiwa na vifaa vya kazi.
Katika mkutano wa hadhara, kero ya maji kwa mradi ujulikanao kama mradi wa Masasi yatawala mkutano; ikiongozwa na Mkt. Wa CCM kata.
DC atoa wiki moja kwa wataalamu kukamilisha kero zote ili mradi huo ukabidhiwe kwa kamati iliyoteuliwa.
Aagiza mgogoro wa wakulima na wafugaji ushughulikiwe ndani ya wiki moja.
DC aeleza mpango wa Wilaya wa kiwanda kila kata- kwa maana ya kiwanda kidogo. Atembelea kiwanda cha tangawizi kilicho mbioni kuanza.
Afurahishwa na watu kuitika mwito wa Mh. Rais juu ya serikali ya viwanda na kufanya kazi.
" Same is not same"
Wiki hii ilikuwa ni kutengeneza barabara umbali wa km. 3 kwa kumwaga moram na kuisambaza katika kitongoji cha Mbuyuni B kijiji cha Hedaru kata ya Hedaru. Barabara hiyo ni ya mtaa inaelekea kijiji cha Makasa umbali wa Km. 30 kutoka Hedaru.
Wananchi wa kitongoji hicho walimuomba DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule aridhie ombi lao la kuiita barabara hiyo kwa jina lake. DC awapongeza kwa kujitokeza wakiwa na vifaa vya kazi.
Katika mkutano wa hadhara, kero ya maji kwa mradi ujulikanao kama mradi wa Masasi yatawala mkutano; ikiongozwa na Mkt. Wa CCM kata. DC atoa wiki moja kwa wataalamu kukamilisha kero zote ili mradi huo ukabidhiwe kwa kamati iliyoteuliwa.
Aagiza mgogoro wa wakulima na wafugaji ushughulikiwe ndani ya wiki moja.
DC aeleza mpango wa Wilaya wa kiwanda kila kata- kwa maana ya kiwanda kidogo. Atembelea kiwanda cha tangawizi kilicho mbioni kuanza.
Afurahishwa na watu kuitika mwito wa Mh. Rais juu ya serikali ya viwanda na kufanya kazi. " Same is not same"