Samatta umewaangusha sana Watanzania

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,188
8,214
Nakubali Mbwana Samata ni kijana wetu na ni mchezaji mzuri sehemu zote alikopita tuko nae bega kwa bega kumoa support na hata wazungu walipojaribu kumsema vibaya tulikiwa tayari kuingia vitani kwa ajili yake.

Habari ya kusikitisha ni kwamba mapenzi waliyoonyesha Watanzania kwake ameshindwa kuyalipa amekuwa mchezaji wa hovyo linapokuja suala la timu ya taifa haonyeshi juhudi yoyote kama hataki ni bora astaafu tu kuchezea starz mimi ni gekuwa kocha wa staz nisingemuita tena.

images%20(2).jpg
 
Daaaah ukikaa kwenye TV ukiangalia Samatta anavocheza pale stars unaona kabisa hafai kupangwa kikosini,maana anacheza anavojua yeye mpaka unajiuliza ndo huyu watu walimtukana Grealish kwa ajili ake, naungana nawe mtoa mada samatta anatuhujumu simuoni hata akitia morali wenzake, refer game dhidi ya E. Guinea alkua kapooza kama panga limelala nje, sametime watu tulishuhudia juhudi za captain wa Guinea mpaka akawapa bao baadae.

Kama kachoka au anahofia majeruhi ni vema astaafu kiroho safi tujue namna ya kupambana na hali yetu.
 
Mbaya zaidi game za Timu ya Taifa Samata anamaliza Dk 90, Msuva anafanyiwa sub kila mechi. Samata anatembea tu uwanjani
 
Huyu alichemka Villa Park....Uturuki nako jamaa wanalalamika hafungi magoli.....
tunamuombea arudi kwenye peak
 
Mtamlaumu bure...watanzania wanafiki mwacheni kwani akiumia hapa hana msaada
Suala la kuumia lisiwe kichaka cha kufichia uduni wa uwezo wake kwa sasa, kwani kina Msuva wanaocheza kwa kujituma hawahofii kuumia?
 
Kuna muda lawama zinamuangukia mtu kutoka kwa watu, wengine awanasema kama vipi hasiitwe hapo hapo hasipoitwa watauliza kwanini hajaitwa? yote kwa yote lazima utambue mchango wa kapteni samatta ndani ya uwanja. nyie mnamuona anatembea lakini anatembea na akina nani?.

linapokuwaja swala la mpira hususa mpira wa kisasa effort ya mtu mmoja mmoja haiwezi kuleta impact kubwa kama sio team work. tujiulize samatta asipofunga nani atafunga? samatta asipokuwa na mpira nani atakuwa nao?

vitu vya vinavyotumia nguvu na akili vinaendana sambamba na umri, ushajiuliza anaumri gani? je ile kasi alokuwa nayo miaka mi5 nyuma unadhani atakuwa hadi sasa (kwa mpira wa afrika)??

Tusijenge misingi ya kumlaumu mchezaji pasina kujua tupo kwenye wakati gani?? baada ya samatta kuibeba Tanzania within 7 years back nani mwingine atavaa kiatu cha samatta??
 
Kwani TFF inasemajee, inatoa tathmini ipi kwa kila mchezaji... mpira wetu hufuata uchambuzi tu... Lazima tukosoane ili tujirekebishe
 
Kuna muda lawama zinamuangukia mtu kutoka kwa watu, wengine awanasema kama vipi hasiitwe hapo hapo hasipoitwa watauliza kwanini hajaitwa? yote kwa yote lazima utambue mchango wa kapteni samatta ndani ya uwanja. nyie mnamuona anatembea lakini anatembea na akina nani?.

linapokuwaja swala la mpira hususa mpira wa kisasa effort ya mtu mmoja mmoja haiwezi kuleta impact kubwa kama sio team work. tujiulize samatta asipofunga nani atafunga? samatta asipokuwa na mpira nani atakuwa nao?

vitu vya vinavyotumia nguvu na akili vinaendana sambamba na umri, ushajiuliza anaumri gani? je ile kasi alokuwa nayo miaka mi5 nyuma unadhani atakuwa hadi sasa (kwa mpira wa afrika)??

Tusijenge misingi ya kumlaumu mchezaji pasina kujua tupo kwenye wakati gani?? baada ya samatta kuibeba Tanzania within 7 years back nani mwingine atavaa kiatu cha samatta??
Tangu yuko mazembe hajawai kuwa msaada starz
 
Samata hajawahi kuwa msaada Taifa stars, sijui hata kwa nini alipewa captaincy, hajawahi kujituma na anafanya timu nzima inacheza kwa morale ya chini, Samata aanzie benchi ili aheshimu nafasi anayopewa.
 
Back
Top Bottom