EZZ CHEZZ
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 1,230
- 1,352
Samatta angalia usije kuwa kama Emmanuel Eboue na wengine kama yeye.
Tumeona kilichompata aliyekuwa mchezaji mahili wa washika bunduki wa London mchezaji Emmanuel Eboue. Mafanikio aliyoyapata yalimtia upofu akaishia kuwanufaisha wazungu (kwa kuwatumikia uwanjani na kisha jasho lake lote kumzawadia Delila wa kizungu aliyemgeuza mgodi wa mafanikio).
Kwa kuchupa mpaka kwenye kitovu cha mafanikio ya soka ulimwenguni (EPL) na kupata mkataba (mnono?) wa miaka mi4 na nusu ni dhahili kuwa kijana katusua.
Nakuomba sana #Samagoal usianze kuishi maisha kama vile hauna deni huku Tz. Yaani kesho keshokutwa tuanze kusikia eti umenunua jumba la vyumba vi3 kwa £mil 2, 3 au 4 ! Ilhali unaweza ishi maisha ya kawaida tu huko na kisha mipesa kama hiyo ukaja kuwekeza huku Tz (kwa kujenga shule ya soka kwa mfano).
Maeneo ya uwekezaji yako mengi sana yanaeleweka na faida zake zinaeleweka (kwako na kwa taifa lako).
Wajibu wa kuanzisha academy umejipa wewe mwenyewe kwa mafanikio uliyoyapata. Sasa fanya utengeneze njia ili wadogo zako uliowaacha huku watinge pande hizo za ulimwengu wa kwanza wa soka mapema (umri wa akina Kelvin John).
Faida za kuanzisha soccer/sports academy kwako;
Kwanza itazidi kukujengea heshima mbele ya Taifa lako. Pia ni uwekezaji mzuri sana kiuchumi kwani ukifanyika vizuri mazao kama ya akina Kelvin John yatakiingizia kituo chako pesa nyingi na manufaa mengine ya kiuchumi. Vile vile itakufanya unufaike na "social capital/network" ambayo ni dhahili kuwa umeijenga huko ughaibuni.
Faida kwa Taifa na jamii;
Kwanza ni ajira hususan kwa watumishi na wengine wote watakaohusishwa na mnyororo huo. Kubwa zaidi ni kuwajengea uwezo wa kitaaluma (ya soka) watoto au vijana wetu. Yaani utakuwa umetupatia jiko la kuwapika akina Kelvin John.
Mbali na hayo utaifungua zaidi hii sekta ya michezo na kuwavutia wawekezaji wengine (wa ndani na nje) kwenye eneo hilo la kiuwekezaji.
Nawasilisha maada wadau. Hebu tuipe nyama zaidi mpaka imfikie mhusika.
Anayeweza kumtag mhusika (au management yake!?) popote pale alipo afanye hima amtonye.
Sent using Jamii Forums mobile app