Samatta kuonekana UEFA au Ligi Kuu ya England. BIG up jembe la Tanzania

Ana Mashabiki Wengi Nchini, Ila Kwa Kujenga Msikiti Ndani Ya Jumba Lake Ni Udini Mtupu, Bora Ajenge Jumba Jingine Na Ndani Yake Aweke Kanisa Itapendeza Sana Kwa Mashabiki Wake Wasio Waislam
Inaonyesha hata yeye kuwa muislamu kwako unaona ni udini...
 
Akina Kanu waliishia kujenga taasisi ya kutibu magonjwa ya moyo yeye anajenga msikiti kana kwamba nchi watu wote wataenda kusali pale. Mafanikio yake alenge kunufaisha wengi, msikiti ni kitu gani kwa nchi isiyofuata na kuongozwa kwa misingi ya imani hiyo? Bora angejenga kituo cha kukuza na kuendeleza mchezo wa soka kwa chipukizi. Yeye ni mwanasoka mambo ya kujenga msikiti angewaachia masheikh wajenge hata kama yeye ni mfadhili. Inapendeza zaidi kujenga miradi ya kitaifa siyo nyumba ya ibada. Kama anampenda mungu wake na anataka kumtolea sadaka ipo misikiti akatoe huko
Samatta ni rais wa nchi gani mpaka unataka afanye haya kwa kodi yako?.. Umekomaa nakuona tu .
Hivi wewe huna ela ukajenge haya unayotaka? Au kwenu nani kajenga hata darasa moja la baby class??
Ela yake unaipangia matumizi.. Eti nchi haina dini?.. Kwa hiyo hutaki awe na imani yake?.. Anamuabudu MUNGU au anakuabudu wewe na wenzio waliokutuma?

Jenga wewe taifa likusifu.. Ye kajenga
 
Anaweza enda akaucheza lakini. Ila mimi mwenyewe naona angebaki genk. Kuna wachezaji wengi sana england wanasugua. Mpaka uwe mfayiliaji sana wa mpira ndio unaweza kuwajua.
Mtu kama bachuayi, niasse, kone, ni wazuri tu na wamechemsha.
Harafu ukkshachemsha pale hata soko lako linashuka.
Mkuu kwa maana ya kuchukua UEFA au EPL akiwa Everton ni kweli atachemsha... Ila EPL anacheza acheni uoga wakati jitihada na uwezo ni wake na yeye anajua England ni ligi ya aina gani?
**Angekuwa amefeli hapo GENK afu akasema aende England ungesemaje?.. mbona tunaficha ukweli wadau. au wanaocheza epl wote wametokea PSG, Monaco na Valencia?
 
Anaweza enda akaucheza lakini. Ila mimi mwenyewe naona angebaki genk. Kuna wachezaji wengi sana england wanasugua. Mpaka uwe mfayiliaji sana wa mpira ndio unaweza kuwajua.
Mtu kama bachuayi, niasse, kone, ni wazuri tu na wamechemsha.
Harafu ukkshachemsha pale hata soko lako linashuka.
Huyu Batshuayi unaemsema amecheza chelsea japo mechi nyingi ametokea sub... Akapelekwa mkopo Valencia ya LA LIGA amecheza hadi UEFA..
Akapelekwa Dortmund ya BUNDESLIGA mkopo akacheza nafasi ya AUBEMAYANG aliyetimkia Arsenal... Amerudi EPL yuko Crystal Pallace anacheza soka.
**Anazunguka hv kwa kuwa timu yake chelsea ni timu kubwa kuna watu pale wanaomzidi uwezo anakosa muda mwingi wa kucheza.. Ndio maana anapoenda Pallace na timu ambazo anahitajika anapata nafasi kubwa anacheza.. kama ni kufeli kafeli kupata namba chelsea sio epl na ligi kubwa.
Angekuwa na uwezo mdogo BVB na VALENCIA wasingemchukua angeenda EFL daraja la 1/2 huko.
 
Ushabiki Wa Kidini Uende Sambamba Na Michezo? Hiyo Haitakuwa Michezo Bali Dini Kujiingiza Na Kutawala Michezo. Bora Siasa Itawale Michezo Kuliko Dini, ndiyo maana kuna wizara ya michezo na inaongozwa na waziri wa michezo ambaye ni mwanasiasa, si padri, mchungaji wala sheikh. Michezo inaunganisha watu wa imani zote. Hivyo basi wanamichezo wanapaswa kuanzisha huduma za watu wote ili waendelee kunufaika kwa mafanikio yake bila ubaguzi wa kidini. Yule mchezaji ni wa wote siyo wa dini yake pekee, afanye vitu vya kunufaisha wengi. Hachezi Kwa Ajili Ya Imani Yake, Anacheza Kama Pia Kwa Ajili Ya sifa kwa taifa lake.Taifa lake halina dini
We jamaa una msongo sio bure.
 
Sijakataa kuwa kaiva, Samatta hawezi kucheza ligi za nguvu kama ya MLS na EPL atakuwa majeruhi kila msimu kwa namna ya uchezaji wake.
Uliitazama mechi yao waliyotangaza ubingwa dhidi ya Anderlecht? Samatta alikuwa kama Toy kwa kifupi abaki Genk acheze UEFA akikutana hata na CSKA Moscow ndipo angalau aanze kujitathmini akikurupuka kwenda Crystal palace kisa Wilfred Zaha anaondoka Haki ya Mungu utakuja kuniambia hatokuwa na lolote na atapigwa benchi EPL kuna wachezaji kibao wakiafrika ambao nauhakika huwajui ila wapo Arsenal, Liverpool na hawachezi ni backbenchers wakubwa na wengi ni wamisri
Kuna ligi za nguvu duniani kupita za Afrika?
 
Sijakataa kuwa kaiva, Samatta hawezi kucheza ligi za nguvu kama ya MLS na EPL atakuwa majeruhi kila msimu kwa namna ya uchezaji wake.
Uliitazama mechi yao waliyotangaza ubingwa dhidi ya Anderlecht? Samatta alikuwa kama Toy kwa kifupi abaki Genk acheze UEFA akikutana hata na CSKA Moscow ndipo angalau aanze kujitathmini akikurupuka kwenda Crystal palace kisa Wilfred Zaha anaondoka Haki ya Mungu utakuja kuniambia hatokuwa na lolote na atapigwa benchi EPL kuna wachezaji kibao wakiafrika ambao nauhakika huwajui ila wapo Arsenal, Liverpool na hawachezi ni backbenchers wakubwa na wengi ni wamisri
Samatta angekuwa Msenegali ungeandika haya?!
 
Tuweke pesa mkuu Mashahidi ni wachangiaji wa huu uzi naweka laki nane mezani nawe uweke.
Samatta akienda EPL atacheza timu ya daraja la kati.
Samatta hatofunga magoli zaidi ya saba kwa kila msimu hata akicheza misimu miwili (Kama ataondoka Genk bila kucheza UEFA).
Samatta atapata majeraha yatakayomuweka nje kwa msimu mzima.
Haya tu
Kwa hiyo unataka kutuambia wewe una akili kupita hao maskauti wa timu za Epl walimuona atafiti kwenye ligi?!
 
Bwege wewe
Unadhan ukiwa star maana yake uishi kipagani?
Angepiga picha kakumbatia Malaya ndio kuishi bila ya udini?
Mpira ni kazi kama wewe ya kuuza Mitumba lakin kuna Maisha binafsi lazima awe nayo
Kama umekerwa na picha yake akiwa Umra achana nae kawafuate kina Mrisho ngasa na videoclip zao chafu chafu
Hahaha tisha sana kada. Umeijibu vizuri hiyo jamaa.
 
Samatta ni bora abaki Genk kuliko kwenda EFL ama EPL akacheze timu itakayoshuka daraja.
Samatta hana kiwango cha kupata namba kwa uhakika EPL ligi ile ni ya nguvu sana na maarifa, Jupiter league ni mdebwedo sana sibezi mafanikio yake ila ndio ukweli mara elfu 10 abaki Genk akacheze UEFA kuliko kwenda Swansea au stoke city kwa sasa asubiri awe mtambo mkubwa.
Alicheza EUROPA na vitimu vya ajabu ajabu akafunga sanaa alipokutana na Fernebahce ndipo akauona mpira wa ulaya ulivyo mara slavia Prague HAHAHAA Samatta ndugu yangu komaa na Genk
Mkuu Genk Ilikomea makundi EUROPA... hv tatizo ilikuwa Samatta au timu nzima kwa ujumla..??
**Hivi nikisema ubora wa mtu unategemeana na wanaomzunguka kwenye timu nitakuwa nimekosea?.. Kama sijakosea kwa nini Tunamroga kabla hajakanyaga huko epl?
 
Uzuri wake Mbwana anajielewa..humu ushauri mwingi ni wa wivu na husuda na roho pana.Ndio maana hatupigi hatua hata moja.Kuna watu tuna comments kama vile tunachezea hivyo vilabu.Nakumbuka tu safari ya Samata ilipoanza tuliongea sana mbovu baadhi yetu.Mpaka alipofikia angesoma comments za humu muda huu angeishia kwenye magazeti ya bongo hapa.

Samata Pambana ufikie ndoto zako maana unayecheza ni wewe si sisi tunaondika hapa nyuma ya Keyboard.Ukiona una uwezo wa kupambana kule EPL au LaLiga nenda ndugu yangu,ukiona kuwa unataka pia kubaki Genk na Maslahi yanaruhusu pia fanya hayo maamuzi kwa kujitazama stamina na Intelligent yako ndani ya soka kwa ujumla.Achana na sisi wenye roho pana hizi ...mazoezi unafanya wewe na uwanjani upo wewe sisi ni wasemaji tu wenye kila aina ya ushauri ambao wengi tunafanya kwa mazoea tu.

Hakuna anayependa mafanikio yako mzee,kwanza wengi wanasema unabahitisha na kweli Mungu amekupa zaidi na zaid katika ubahitishaji wako mpaka sasa hajakuangusha.Nikutakie mafanikio mema na uzidi kupambana kwa ajili ya maisha yako kama ilivyo vijana wengi tunaohangaika kupata mkate wa kila siku na kukutana na changamoto kibao za raia na vijana wenzetu.
 
Nilichoona kwa Samata ni mtu wa kuadapt na kila anapoenda anaibuka kuwa star wa team, Genk inatoa wachezaji wengi wazuri wanaokwenda kutesa Ujeruman, Epl, na Serie A.. Kuna akina Trosard pale Genk ila kaibuka mbele yao..
Anaweza kucheza vizuri sana hata EPL na kufunga zaidi ya goli 10.
Hata akifunga goli 7 mkuu tutamrank na game alizocheza na timu yake..
Anachotaka Samatta ni kuvuka level asogee ya juu na yuko kwenye wakati wake.. asipoenda leo ataenda lini na age inakata...
Wengine wanaomba acheze UEFA kwanza.. sio mbaya lakini EPL ni top jamani na mkwanja uko kule , ngoja apige pesa umri unaruhusu bado.
 
Mkuu kubaliana nami Samatta akienda EPL atacheza mechi 5 alafu atakaa nje msimu mzima eidha kwa majeraha au kwa kupata mbadala (akienda msimu ujao)
Genk haina wachezaji wazuri wanaotesa ligi zingine wanaozidi wanne wana Thiba cotwaa (jina lake la mwisho kama nimekosea kuliandika niwie radhi) na mmoja EPL nimemsahau jina.
Samatta EPL hapawezi mnampa kichwa kikubwa atapasuka angalau aende Scotland akapate ujuzi wenzake wengi wa Africa huanzia huko au hata ufaransa ENGLAND watamsajili EFL washenzi wale alafu timu ishuke daraja na huko EFL unategemea atakuwa wapi? Genk ni better
Thibatous kipa wa Real madrid
Lukaku wa man utd
De bruyne wa City
Bailey wa Leverkussen
Koulibaly wa napoli.
Halafu mkuu hv vitu muda mwingine juhudi zaidi na umakini ndio vinawatoa hawa... Tumpe moyo akakomae kuliko kuogopa na kumtisha.
 
Thibatous kipa wa Real madrid
Lukaku wa man utd
De bruyne wa City
Bailey wa Leverkussen
Koulibaly wa napoli.
Halafu mkuu hv vitu muda mwingine juhudi zaidi na umakini ndio vinawatoa hawa... Tumpe moyo akakomae kuliko kuogopa na kumtisha.
Lukaku na Koulibaly hawajawahi kucheza Genk.
Lukaku kacheza Antwerp na Anderlecht.
Koulibaly ana St louis na zingine
 
Mkuu Genk Ilikomea makundi EUROPA... hv tatizo ilikuwa Samatta au timu nzima kwa ujumla..??
**Hivi nikisema ubora wa mtu unategemeana na wanaomzunguka kwenye timu nitakuwa nimekosea?.. Kama sijakosea kwa nini Tunamroga kabla hajakanyaga huko epl?
Simlogi ila akienda EPL sasa ndio kapotea hivyo
 
Everton naiona nafasi yake pale wale jamaa wako vizuri sana kiuchezaji wanamkosa tu mmaliziaji makini anayejua kukaa kwenye nafasi kwa wakati muafaka.
Mkuu pale Everton kuna jamaa raia wa Brazil anaitwa Richarlison... walimtoa Watford na msimu huu amefunga goli 17 mashindano yote...
Huyu jamaa Man u, Psg naBarca wanamtaka ..kama ataondoka linaweza kuwa gape kwa Samatta.
Bado Mbwana popote atakapoenda apige kazi kweli kupata namba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom