Samatta hatomaliza misimu miwili ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Kwa haraka haraka tu nimegundua kwamba hujawahi kucheza mpira hata kidogo...samatta ni no. 9 kazi yake ni kufanya finishing na kunyemelea mipira ya mwisho. Mambo ya kukaba kukokota mipira anawaachia wengine. Mfano mzur ni Ruud van Nisteroy...mtaalam wa kumalizia tu

Nisteroy huyo unaemtaja angalia magoli yake kama alikua hajitengenezei mengine..
 
Kuna center foward, target man, deep lying striker na striker which is a rare bleed, sasa mtoa uzi ukishajua sifa za kila aina ya mshambuliaji utapata jibu Samatta ni aina gani ya striker na kupitia sifa hizo ndipo utagundua why kasajiliwa na Aston villa.

Don't hunt what you can't kill.
 
Najua nitashambuliwa kwasababu waTz hatupendi kuambizana ukweli, hata uone mapungufu ya wazi kabisa tuko radhi tukayaseme pembeni au kukaa nayo kimya.

Kwanza nampongeza alipofika na apangacho Mungu lazima kitimie inawezekana alipangiwa kufika hapo alipo, lakini pia kwenye maisha kuna suala na bahati, inawezekana kafika hapo kwa bahati aliyonayo ukiondoa juhudi na maarifa.

Twende kwenye hoja, ukiangalia samatta aina yake ya ushambuliji utagundua ni mtu wa kutengenezewa kila kitu yani apikiwe, apakuliwe yeye aje kula tu, ligi ya EPL inataka uhangaikaji, utafutaji na sometimes hata kama wewe ni mshambuliaji basi ujue kujitengenezea pia. Ukiangalia magoli ya Samatta toka alipokua Genk utagundua ni mzuri sana kumalizia, yani yeye ni mipira ya kichwa, kama ni mguu basi ile one touch nyavuni, hakina kujitengenezea wala kujitafutia.

Ndio maana tumeanza kusema ooh anabaniwa pasi, hakuna kitu kama hicho, angalia game zote mbili hakuna sehemu ametafuta, zote alikua na mtu anaezengea zengea golini, kibongo bongo tunaita kuibia . Sasa kwa wenzetu hata wachezaj wenzie wanamchora tu ni rahis kumuona aah jamaa anasubiri tumpelekee haya aendelee kusubiri, sasa sisi tunatafsiri kama wanambania

Lakini pia Samatta akisema aanze mashambulizi ya kujitengenezea utagundua anawahi sana kuchoka, hana pumzi na hapo ndio linakuja suala la kuongeza juhudi kwenye kijijengea pumzi, tusishangae akianza kutokea benchi round ya pili ikianza. Yote ya yote kijana anajituma anastahili pongezi.

Wenzetu wale hawakawii kukuuza kwa mkopo wakiona mambo sio mambo..
unamaanisha hana utofauti na Oliver Giroud, right?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nazisoma Twitter tu naunganisha na hii
Adjustments.jpg
Adjustments.jpg
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom