Lusato
Member
- Apr 16, 2013
- 29
- 5
Mbeya. Samaki wanaoingizwa nchini
wakitokea nchi jirani wanadaiwa
kusababisha madhara ya kiafya
ikiwamo wanaume kuota matiti na
wanawake kuota ndevu.
Samaki hao huingizwa nchini kupitia
mipaka ya Kasumulu-Kyela na
Malawi na ule wa Tunduma na
Zambia.
Kutokana na uwapo wa taarifa za
samaki hao, Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Amos Makalla ameagiza
mamlaka zote zinazohusika na
usimamizi na ulinzi mipakani
kuongeza nguvu ya udhibiti na
uhakiki wa bidhaa zote
zinazoingizwa nchini.
“Mbeya na Songwe ni kitovu cha
biashara ya samaki wanaotoka nje ya
nchi. Lakini kibaya zaidi kuna
taarifa za uwapo wa samaki kutoka
nje wanaodaiwa kuhatarisha afya za
watu. Nimesikia kina baba wakiwala
huota matiti na wanawake huota
ndevu kwa wingi na athari zingine
nyingi,” alidai Makalla na kuongeza:
“Sipingi kuingizwa kwa vyakula
kutoka nje ya nchi, lakini ni vizuri
utaratibu ukafuatwa, idara zote
mipakani zijiridhishe na bidhaa zote
zinazoingizwa hapa kwetu.”
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Uvuvi nchini, Magese Bulayi
alisema mikoa ya Songwe na Mbeya
ni kitovu cha biashara ya mazao ya
majini.
Alitoa wito kwa wafanyabiashara wa
samaki kuzingatia maagizo na
maelekezo yatolewayo na Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) pindi
waingizapo samaki hao kupitia
mipaka ya Tunduma na Kasumulu
wilayani Kyela.
Bulayi alisema samaki hao wana
madahara kwa binadamu na Idara
ya Uvuvi makao makuu baada ya
kupata taarifa, tayari imewatuma
maofisa wake kutoa elimu kwa
wadau kuhusu utaratibu wa uingizaji
wa biashara ya vyakula vitokanavyo
na mazao ya majini.
Mmoja wa wafanyabiashara wa
samaki katika Soko la Soweto jijini
Mbeya ambaye hakutaka jina lake
litajwe gazetini, alisema samaki
wanaowaagiza huletewa wakiwa
wamefungwa na juu huandikwa
samaki aina ya sato, migebuka,
kibua, au magege.Hivyo hawawezi
kujua kama wana madhara kwa
binadamu. “Ila siku za hivi karibuni
tunapokea malalamiko mengi kutoka
kwa wateja wetu wanaodai kuwa
tunawauzia samaki waliooza,”
alisema.
Mkazi wa Ruanda jijini hapa,
Atuganile Kasyupa alisema kwa sasa
samaki anaonunua hawana radha.
“Tukiwauliza wauzaji wanasema eti
kwa sababu ya balafu,” alidai
Kasyupa.
Source Mwananchi
wakitokea nchi jirani wanadaiwa
kusababisha madhara ya kiafya
ikiwamo wanaume kuota matiti na
wanawake kuota ndevu.
Samaki hao huingizwa nchini kupitia
mipaka ya Kasumulu-Kyela na
Malawi na ule wa Tunduma na
Zambia.
Kutokana na uwapo wa taarifa za
samaki hao, Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Amos Makalla ameagiza
mamlaka zote zinazohusika na
usimamizi na ulinzi mipakani
kuongeza nguvu ya udhibiti na
uhakiki wa bidhaa zote
zinazoingizwa nchini.
“Mbeya na Songwe ni kitovu cha
biashara ya samaki wanaotoka nje ya
nchi. Lakini kibaya zaidi kuna
taarifa za uwapo wa samaki kutoka
nje wanaodaiwa kuhatarisha afya za
watu. Nimesikia kina baba wakiwala
huota matiti na wanawake huota
ndevu kwa wingi na athari zingine
nyingi,” alidai Makalla na kuongeza:
“Sipingi kuingizwa kwa vyakula
kutoka nje ya nchi, lakini ni vizuri
utaratibu ukafuatwa, idara zote
mipakani zijiridhishe na bidhaa zote
zinazoingizwa hapa kwetu.”
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Uvuvi nchini, Magese Bulayi
alisema mikoa ya Songwe na Mbeya
ni kitovu cha biashara ya mazao ya
majini.
Alitoa wito kwa wafanyabiashara wa
samaki kuzingatia maagizo na
maelekezo yatolewayo na Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) pindi
waingizapo samaki hao kupitia
mipaka ya Tunduma na Kasumulu
wilayani Kyela.
Bulayi alisema samaki hao wana
madahara kwa binadamu na Idara
ya Uvuvi makao makuu baada ya
kupata taarifa, tayari imewatuma
maofisa wake kutoa elimu kwa
wadau kuhusu utaratibu wa uingizaji
wa biashara ya vyakula vitokanavyo
na mazao ya majini.
Mmoja wa wafanyabiashara wa
samaki katika Soko la Soweto jijini
Mbeya ambaye hakutaka jina lake
litajwe gazetini, alisema samaki
wanaowaagiza huletewa wakiwa
wamefungwa na juu huandikwa
samaki aina ya sato, migebuka,
kibua, au magege.Hivyo hawawezi
kujua kama wana madhara kwa
binadamu. “Ila siku za hivi karibuni
tunapokea malalamiko mengi kutoka
kwa wateja wetu wanaodai kuwa
tunawauzia samaki waliooza,”
alisema.
Mkazi wa Ruanda jijini hapa,
Atuganile Kasyupa alisema kwa sasa
samaki anaonunua hawana radha.
“Tukiwauliza wauzaji wanasema eti
kwa sababu ya balafu,” alidai
Kasyupa.
Source Mwananchi