Sam Nujoma tunachinjana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sam Nujoma tunachinjana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chereko, Aug 3, 2009.

 1. C

  Chereko Member

  #1
  Aug 3, 2009
  Joined: Jul 20, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Ajali, Ajali, Ajali!!!!!!!!

  Tutakosaje kupata ajali kwa mwendo wa kasi wa magari Sam Nujoma? Hivi watu wote kasi kasi wanakimbilia wapi? Shoprite? Mwenge? Ubungo? Kichekesho kweli kweli!!!!! Hivi madereva hawa hawajawahi kuona au kupita kwenye lami iliyokaa sawa? Hivi askari wako wapi?????

  ROUND ABOUT
  Madereva wengi inaonekana hawajui kuwa roundabout unamwachia anayezunguka apite kwanza au "mpe nafasi apite aliye kulia" wao mwendo tu mwendo tu "mimi najua gari kuliko anayeendesha gari ile", "gari yangu ni bora kuliko la yule".....vichaa tupu barabarani, kaa karibu na round about au kwenye kona utacheka kweli!!!!!

  Taa za barabarani
  Madereva wengi hawajali taa za barabarani, bila shaka kwa ajili hiyo na mwendo wa kasi hamad! taa hizo!! halafu Mzinga

  Zebra
  Zebra za Sam Nujoma na hata Nyerere Road ni kama maua yaliyochorwa kama picha tu, madereva hawazioni, wao mbio tu mbio tu mnakimbilia wapi???????

  Dala dala hawaoni vituo
  Watu wakitoka Mlimani city au kona ya supa star wanasubiri basi kwenye kona badala ya kwenda kwenye kituo mita chache tu hazizidi 30, wenye magari wanaotaka kupinda kona wanakwazwa na daladala na hii ni hatari kubwa. Vituo vilivyojengwa na Mchina havina kazi, tumezoea kila kitu short cut. Hivi Askari hawaoni hili????? Wawakamate madereva wanaosimamisha daladala hovyo na hata wananchi wanaosubiri daladala kwenye kona badala ya kituoni!!!!!! Siku moja nimekaa kituoni mabasi yanapita basi ikabidi nirudi kwenye kona basi likasimama inachekesha kweli kweli haaa haahaaaaaaa!!!!!!!  Mwalimu wa BP wa udereva ITV, John Muro wa ITV fanyeni kazi yenu hapa kuelimisha jamii matumizi bora na ya usalama ya kutumia barabara za kisasa waache kila dereva kuona ana haraka kuliko mwingine matokeo yake kila mmoja ana haraka hatima yake wote kuharaka kwenda Ahera au hospitali !!! au kusababisha au kuwasababishia wengine matatizo.
  1. Watu wataacha kazi kwenda kwenye msiba au hospitali kuona mgonjwa, watatumia pesa walizopangia shughuli nyingine za maendeleo kwa shughuli za msiba au ugonjwa uliosababishwa na ajali
   [*]Watoto watabaki hawana wazazi, wamefariki kwenye ajali
   [*]
   Madaktari wataacha kazi zao na kushughulikia majeruhi wa ajali DHARURA
  2. Ndugu watatoka mbali na kuacha shughuli zao, mashamba etc na kwenda kwenye msiba au ugonjwa wa ajali, jamani!!!!
  3. Mwenye kumiliki gari ana hasara gari litasimama na atatumia pesa kutengeneza
  4. Askari wataacha kazi zao kushughulikia ajali
  Jamani angalieni sekunde moja ya ajali madhara yake ni makubwa mno na ya muda mrefu

  Chereko hawezi kuchereka namna hii
   
Loading...