East African Eagle
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 3,759
- 2,209
Ili kutatua mgogoro wa Sudan ya kusini viongozi wakuu wawili wa Sudan kusini ambao ni Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar inabidi waondolewe wote katika utawala na siasa za sudan kusini kwa kushindwa kuiongoza na kuhakikisha sudan kusini inakuwa na utulivu wakati wa uongozi wao.
Kuendelea kuwepo kwa watu hao wawili katika siasa za sudan kutafanya mgogoro huo kuwa more complex na usioeleweka utaisha lini na vipi.Huyo Raisi na makamu wake wameonyesha wazi kuwa hawawezi kufanya kazi kama team wakiwa katika utawala bali kila mmoja amekuwa ni kiongozi wa kundi badala ya kuwa kiongozi wa wasudan kusini wote.
Suluhu ni kutimua wote wawili na kutafuta kiongozi wa mpito atakayehusika na kusimamia uchaguzi huru wa haki wa raisi atakayechaguliwa na wasudani kusini kusimamia nchi yao.Hao wawili wasirudi kugombea cheo chochote wawastaafishe wawalipe mafao yao na wawe viongozi wastaafu wasiohusika kwa lolote kwa siasa za sudani.Wasuluhishi wa kimataifa wawatake watoke kwenye uongozi.
Hilo likiwa linafanyika UN itume majeshi ya kulinda amani ya kuzuia pande zote za waasi na serikali zisirushe risasi hata moja kuelekea upande mwingine wala kwa majeshi ya UN.Jeshi la UN lipewe mandate ya kushambulia upande wowote utakaorusha risasi ili kuhakikisha Sudan Kusini inakuwa na amani wakati wa kipindi cha mpito.