Vijana wengi wengi bado hawajui thamani ya muda na jinsi ya kuutumia vyema........
Vijana wengi waliopata bahati au fursa za kupata elimu ya juu hawajui kuwa hiyo ni nafasi adimu sana kwenye maisha yao hasa kwenye hizi nchi zetu za kiafrika kwani siku ukifunguliwa macho na kuona vilio vya watu waliokauka machozi kwa kuiokosa nafasi hiyo adimu au majuto ya watu wanaoteseka maishani mwao kwa kuichezea bahati hiyo adimu....sidhani kama kuna kijana angekuwa anakuja kuandika ujinga angali bado yupo masomoni.........
Kimsingi ni kuwa kila jambo linafanywa kwa wakati wake....hivi vitu vinavyokutoa udenda na kukuumiza moyo ni vitu vidogo sana kwenye maisha na pia huu sio wakati wake.....lakini vile vile kujihakikishia upatikanaji wa vitu hivyo ambavyo wewe unaviona kuwa ni vya msingi kunategemea na juhudi zako katika kulifanya hili la wakati huu vyema zaidi.....
Muda ni rasilimali adimu sana na ni rahisi kuipata lakini gharama za kuupoteza hazilipiki...kwani ukishaupoteza kinachofuata ni majuto.....