GE2025 Salum Mwalimu: Mkinichagua nitajenga viwanda vya matunda

GE2025 Salum Mwalimu: Mkinichagua nitajenga viwanda vya matunda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,131
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Salum Mwalimu amesema akichaguliwa kuwa Rais atahakikisha Viwanda Vidogo vidogo vya kusindika Matunda vinaanzishwa katika Jimbo la Muheza Mkoani Tanga ili kuwasaidia Wananchi kiuchumi tofauti na sasa Matunda hayo yanaoza yakiwa Shambani kwa kukosa soko.

Mwalimu ameyasema hayo leo Septemba 1, wakati akinadi sera zake kwa Wananchi wa Muheza na kuwataka wasimuangalie kwasababu ya kuwa yeye ni KIjana bali waangalie nani atakayeweza kuwaletea maendeleo sahihi kwa muda huu baada ya miaka mingi ya Uhuru.

“Ingieni mtandaoni angalieni Miji kama ya Muheza huko Duniani yenye Matunda muone kama kuna umasikini hakuna umasikini kwasababu inazalishwa Viwanda vidogo vidogo.

Umasikini wa Mtu wa Muheza hauwezi kuondokana kwa mambo makubwa, mmepewa ardhi nzuri yenye Matunda mkapewa na akili ili muondokane na umasikini tupeni sisi CHAUMMA tupelekeni Ikulu.”

Soma Pia:

1756877224089.png
 
Back
Top Bottom