PreGE2025 Salum Mwalimu Katibu Mkuu CHAUMMA: Yaja siku CHADEMA watataka kufanya kazi na CHAUMMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Dhoruba iliyotokea sisi wengine tukasema hapana. Tukasema hapana kwasababu tunazizuia akili zetu zisitawaliwe na mihemko, tunazizuia akili zetu zijawe na sifa za kuja mbele za watu na kupigiwa makofi huku tukijua hatuna namna yoyote ya kuwasaidia watanzania, tukakataa, ndio sababu tukasema tuachane tu kwa amani. Mabadiliko ya fikra hayajawahi kuwa dhambi kwenye maisha kama fikra zenu ni hizi na zetu ni hizi basi tuachane.

Tukaamua kwenda CHAUMMA, Nako ikawa nongwa, tukiwaambia ndani mnasema sisi ni wabaya, sisi ni wasaliti, tumeshindwa, tuwaachie Chama. Tukiwaambia fanyeni hivi hamtaki. Tumeona basi sisi akili zetu tukazitekeleze kwingine, bado imekuwa nongwa. Sasa hivi adui wao sio CCM tena ni CHAUMMA, matusi, fedheha, kudhalilishana. Hiyo sio Taasisi tuliyoijenga. Kama kutofautiana ni dhambi basi hata upinzani nchi hii usingekuwepo."- Salum Mwalimu, Katibu Mkuu CHAUMMA akiwa kwenye ziara ya Chama hicho Usa River, Mkoani Arusha.
Your browser is not able to display this video.

source: JAMBO TV​
 
CHADEMA siyo daladala ya kila mtu kupanda, na wala hawawezi kushirikiana na chama kinachotafuta nafasi kwa kivuli cha upinzani. In politics, principles matter more than desperation.
 
Salim Mwalimu ana frustration za mke wake kuja kukosa ubunge wa viti vya wanawake na yeye kukosa mgao wa ile per day ya bunge
Chadema hawazungumzii chama mfu hata siku moja ni hoja ya kijinga ya huyu mzanzibari wa Kinondoni
Huyu pungo anatafuta kick na fadhila ya Fisiemu
 
Jibuni hoja zake badala ya kumchafua. Huyo Suzan Kiwanga aliyebezwa na Makamu Mwenyekiti wenu ni wa chama gani? Mnaendekeza mno matusi.

Amandla...
 
Watakapoanza kufanya hivyo ndio itakuwa mwisho wangu kuwafatilia na mambo yake🤣, kwa sasa nawazingatia sana ila wakizingua tu nawaacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…