Salome: Diamond Platnumz ft Rayvanny - General Views

Mi ni fan wake mkubwa lakn ajab wimbo sijaupenda kiivo.Labda kadri sinazokatka ntaupenda!
 
Unaliwa wewe
 
Oreraa bakuru vani oreraa ngambee aisee hii kitu inapenyaaa chaa! Mond we dogoo unapandisha preshaa na salome wako.
 
Hii nayo iko njiani,kakumbuka zamani za kale wakati ana rap.
 
Lakini wimbo wa taifa bado unasumbua kitaa.
 
Ego ni kitu kinatesa sana anajaribu kuwaambia wajinyonge ila ukweli utabaki pale pale hata aiforce Ego kupanda
 
Hapa ni suala la mtazamo tu lakini uhalisia ni kwamba hii inaonyesha ubora wa Saida dhidi ya diamond.
Tatizo letu kubwa ni kwamba tunaangalia mafanikio kwa vigezo vya nani anamiliki nini (possession) badala ya traits halisi, Na sio ajabu kukuta vijana wametoa nyimbo mbili tu na wanamiliki used cars na nyumba alafu tunajiaminisha eti 'kijana kafanikiwa' na ukimwambia mtu huyo huyo kuwa hakuna mwanamuziki wa kizazi hiki aliyefikia hata robo ya Dr. Remmy (kwa mfano) anakucheka!
Pamoja na dhuluma alizofanyiwa Saida anaendelea kuwa juu tangu nyakati zake na ahitaji promo za kitoto, muda utadhihirisha ukweli huu.
 
Jini anaendelea kuvimiliki vibanda tu,wao wapo kwenye kushindanisha nani mwenye sauti nzuri kuliko Hadija Koppa,huku wanaamka kwa mama.
 
Ila dunia haiko fair kabisa, eti anayegawa haki ya wimbo ni Felician Mutta na si Saida Karoli, yaani kwa maana nyingine Siada Karoli huo wimbo hana haki nao haumuhusu daah, kweli shule ni muhimu
Toka zako
 
Tunamheshimu Saida kutokana na uwezo wake lakini watu wakiwa na mawazo kama yako basi wanaweza kusema unaporudia wimbo wa zamani ni kwamba unaona aliyefanya kuna mahali kaukosea na wewe unaweza kuufanya vizuri zaidi kuliko original version. Lakini kwa watu wanaofahamu hawawezi kusema hivyo kwa sababu kurudia ngoma au hata movie ya zamani (remake) ni mambo ya kawaida kwenye tasnia ya muziki na filamu!

Kwamba tunaangalia mafanikio kwa kuangalia mtu anamiliki nini ni wewe ndie umejikita kwenye hayo mambo na kujifanya huoni maeneo ya kisanaa!!! Unataka kuniambia mtu aliyedumu kwenye game zaidi ya miaka 5 bila kushuka amefanikiwa kubaki juu kwa kuwa anamiliki nyumba na magari?! Ferouz alikuwa ni miongoni mwa wasanii wa awali kumiliki gari za bei mbaya... leo hii yupo wapi?! Nature ni miongoni mwa wasanii wa awali kufanikiwa kujenga na kumiliki usafiri wa maana, leo hii unamsikia?!

Let's learn how to appreciate na tuache roho ya kwanini! Watu wana-hustle huku na kule kutengeneza kazi mpya, Mtu kama Diamond ni kawaida sana kukuta hadi usiku wa manane yupo studio, wanahangaika huku na kule kufanya featuring na wasanii wa level mbalimbali, wanafanya staili hii na ile ili kuvutia mashabiki wa aina mbalimbali... lakini yote hayo huyaoni na kinyume chake unaamini tunawapima kutokana na vile wanavyomiliki!!!
 
Una lugha kali sana.
Ni kweli una lugha kali lakini uzuri ni kwamba, ukielewa mitusi iliyomo mle basi fahamu ushakuwa mtu mzima vinginevyo utaishia kudhani anazungumziwa ngongoti mwanadamu kumbe ngongoti mlingoti ukiwa unasoma network 101%!! Tena Raymond ndo kazidi kumwaga mitusi sema the kid is so smart... huwezi kujua kwamba sehemu kubwa ya mashairi yake ya verse ya kwanza ni mitusi tupu!!
 
Na hii dabate itaendelee kwa muda mrefu lakini mwisho sote tutajua kuwa Saida ndiye alikuwa na kipaji na ndio maana huyu Muta hajamtoa msanii mwingine baada ya hapo ...kama kweli ni 'professional promoter'!?
Vivyo hivyo huyu anayesema kurudia nyimbo (remake) ni kitu cha kawaida ajiulize kipindi wimbo huu unatoka ulihit kiasi gani kulinganisha na nyingine za wakati huo alafu uangalie miaka 16 baadae ni nyimbo ngapi zimetolewa mpaka urudiwe huo!? Hata mimi naweza kukaa studio usiku kucha lakini kipaji changu kikategemea wengine kunitoa.
cc: chige
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…