Mbunge wa Mchinga Mkoani Lindi Salma Kikwete, kwenye kipindi cha maswali na majibu amehoji Serikali ina mpango gani na Jimbo lake halina Stendi hata moja wakati Magari makubwa yanapita kutoka Mikoa mbalimbali kama Ruvuma na Mtwara na mengine kutoka Nchini jirani ya Msumbiji.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa TAMISEMI Reuben Kwagilwa, amesema Serikali itafanya mapitio pamoja na kutathmini hali ilivyo ili kujenga stendi katika Jimbo hilo la Mchinga “Serikali itafanya mapitio pamoja na kutathmini hali ilivyo Mchinga, ni muhimu sana Mji huo uwe na stendi hivyo sisi Serikali tutafanya mapitio na kuainisha cha kufanya”