Salim amkumbuka JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salim amkumbuka JK

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by valour, Oct 30, 2010.

 1. v

  valour Senior Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  WAZIRI Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Ahmed Salim, amemmwagia sifa mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dk. Jakaya Kikwete, kuwa ana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi huku akilinda misingi ya amani na utulivu.

  Mbali na sifa hizo, pia alitumia nafasi hiyo kuwataka Watanzania kutafakari kwa makini wakati wa kupiga kura ili kuhakikisha wanachagua viongozi wanaotokana na CCM ambacho ndicho kimejenga misingi ya amani inayoleta sifa katika nchi za Afrika.

  Dk. Salim aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kimanga Jimbo la Segerea. “Jamani nimepata bahati ya kuzifahamu vizuri nchi za Afrika kutokana na nyadhifa nilizokuwa nazo, nimekuwa msuluhishi wa migogoro mingi ambayo imetokana na uvunjifu wa amani, tukianza Rwanda, (DRC) na kwingine maelfu ya wananchi wanapoteza maisha yao bila sababu ya msingi, hivyo tusibeze dhana ya utulivu na amani ni jambo la msingi sana,” alisema Dk. Salim. Dk. Salim hakusita kumwelezea Rais Kikwete alivyo mvumilivu na kiongozi ambaye anapata sifa kubwa kimataifa kutokana na nia yake thabiti ya kuwatetea Watanzania kila mahali anapokuwa.

  Source: Tanzania Daima
  JAMANI WAZEE WENGINE WANGEPUMZIKA TU SASA WATUACHIE WANANCHI TUFANYE MAAMUZI
   
 2. p

  p53 JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  na yeye aonekane kapiga kampeni lakini deep down...
   
 3. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hana lolote huyu anaangalia tumbo lake tu wakati haya madudu yanalolifilisi taifa yanafanyika alikuwa wapi? Wakati wa kuhesabiwa umepita ngoja moto uwake.
   
 4. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dun anawabeep waTZ.
   
 5. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nampongeza kwa ujasiri wake wa kumpamba adui...deep inside anajua
   
 6. K

  Kashishi JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2010
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 1,101
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mimi binafsi nalipata kuwa supporter mzuri sana wa SAS miaka nyuma na kuona ni mtu mmoja anayefaa kuwa Rais kwenye uchaguzi wa mwaka 2005. Japo kulikuwa na jamaa yangu mmoja aliyewahi kumfahamu SAS kwa karibu na hata kufanya nae kazi kwa karibu alipata kunishawishi sana kila mara tulipokuwa tukiwajadili wagombea kuwa SAS hafai kuwa Rais. Na hoja zake kuu ni kuwa SAS hana confidence na mtu muoga mno wa kuudhi mtu katika kufanya maamuzi. Na ni mtu asiyetaka kumkera mtu hata kwa jambo lililowazi kabisa atazungusha maneno pasipo hata kueleweka. Kipindi hicho sikupata kumu elewa kabisa jamaa yangu yule.

  Lakini basi baada ya uchaguzi 2005 kupita ndio kidogo kidogo nikafumbua macho na nikapata kumfahamu na kumsoma vizuri SAS na kauli zake na nikaanza kuunganisha na hoja za jamaa yangu yule. Binafsi nimefika mahala hata SAS aki - comment kitu siku hivi huwa hata sishangai wala kumtilia tena maanani juu ya comments zake. Hata jambo liwe chafu namna gani SAS atapata kigugumizi na ataamua kuzungusha. Sasa huwa najiuliza huyu ndie mtu Wa-Tanzania walikuwa wamkabidhi nchi...maana hata sijui ndio ingekuwaje yarabi?

  Sasa hebu tazama hizo comments zake hapo kwenye hiyo makala na ulinganishe na mtu caliibre ya ufahamu wake? eeh ? hata unajiuliza SAS na comments hizi wapi kwa wapi ?

  Hivi sasa namchulia kuwa na yeye 'si lolote wala chochote' bali ndio hao hao wote wanaoangalia matumbo yao binafsi na familia zao tu, Wamefanya Wa-Tanzania ni ngazi yao ya kufikia juu tu.
   
Loading...