Naisujaki Lekangai
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 1,340
- 1,377
Habari nzuri zimeenea kwamba meli ya kisasa ya kubeba mizigo ziwa nyasa itazinduliwa hivi karibuni.Cha kufarahisha mno ni kwamba meli hiyo ya kisasa imeundwa hapa hapa nchini na mhandisi mzalendo aitwate Eng. Salehe Songoro.
Kwa serikali hii inayotaka kuhimiza ukuaji wa viwanda huyu mhandisi ni zawadi kubwa toka kwa Mungu. Ni mbegu nzuri ya kuanzisha viwanda vya kanda vya kuunda mashua na meli za kisasa.
Yapaswa sasa serikali iunde mkakati maalum wa kumtumia huyu mhandisi katika kutekeleza hiyo azma ya viwanda vya kanda vya mashua na meli kwa soko la afrika mashariki.
Yale makosa yaliyofanywa na wizara ya afya ya kumsononesha mtaalamu wa magonjwa ya moyo Dr Ferdinand Masao mpaka akafariki yasitokee hata chembe kwa mhandisi Songora.
Tukiletewa mbegu ya maendeleo toka kwa Mungu tuipande na sio kuichezea mpaka ipotee.
Opportunities never come twice. Songora akipata maudhi anaweza kwenda kenya au uganda na kufungua viwanda vya meli.Watampokeaje!