Mkuu unatakiwa ubadilike. Maisha ya kutegemea mshahara ni magumu sana. Azisha kabiashara ka aina yoyote ile na kwa mtaji wowote ule, ili uweze kujikopesha wakati ukisubiria hiyo salary.
Binafsi nashukuru nimetoka huko kwenye utegemezi wa salary kwa 100%! Yaani ilikuwa hata wakichelewesha siku moja tu, akili inavuruga kabisa! Samahani sana kama nitakuwa nimekukwaza kwa huu ushauri wangu.