Salamu zangu za eid kwako Hanifa

Salamu zangu za eid kwako Hanifa

Ni mwaka sasa umepita tangu niifute namba yako kwenye simu yangu

Japo juzi juzi umenitafuta ila sio kupitia namba yangu kupitia kwa ndugu yangu habari nikazipata nikamwambia achana nae

Kiukweli baada ya kuniambia kichwa changu hakikukaa sawa ndo nikajua bado upo moyoni mwangu na kichwani ila mikononi mwangu haupo

Nikikumbuka tulivyokuwa pamoja japo kwa kipindi kifupi ulikaa sana moyoni kuliko yeyote yule nilikupenda kweli sijawahi kupenda hivi hata ile nyimbo yetu niliifuta siitaki tena kuisikia picha zako nikafuta ila kukufuta moyoni nimeshindwa nasikitika kwa kweli

Sijui nilipokosea nahisi uliniona mtoto nilipokuwa nakuimpress ndo tatizo

Kwa kweli nilikupigia simu tukaongea nachoshukuru hukuniuliza mimi nani ulinijua japo nimebadili namba kwa ajili yako ila sauti yangu umeikumbuka sijui unawaza nini huko ulipo

Ila nahisi utakuwa unafuraha umempata mwengine labda mrefu kuliko mimi hensam boi na mweupe au labda ana hela kunizidi

Mimi bado nipo vile vile mcheshi as always nikiwa na buku mfukoni nitakupa mia 9 mia iliyobaki nitakudanganya ya kukwangulia vocha

Nilipanga tutazunguka sehemu nyingi ila mpaka nikizipata ukachoka ahadi zangu

Ni mimi uliyeukodi moyo wangu kwa kipini chako puani

Mr H
You killed it..
Uandishi mahiri umenivutia mpka nikatami niitwe hanifa.
 
Hannah najua umekasirika sana kisa sijalipia kisimbuzi naahidi kulipia uendelee na ile tamthilia yako usilipie wewe
 
Ujumbe mzuri sana nami niudediketi kwa H wangu humuhumu jf! Dear H, najua bado tunapendana sana tena sanaaa kiasi kwamba tukikutana bila kujali una mke au wapenzi lukuki, I believe ni mahug makiss na malovee nonstop! Japo nikama tumeachana ila ukweli tunaujua wenyewe na ahadi yangu ipo palepale tukikutana utafurahi naroho yako na utaapreciate my decency! I do appreciate you alot ni majaribu yakidunia tu! With regards,, Azial,
 
Pole sana mkuu,,, usijikaze mtafute mnaweza pasha kiporo
 
Back
Top Bottom