Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Tanzania tumepata kiongozi mchapa kazi, Mpenzi wa Mungu, mwenye maamuzi, Mzalendo, msema kweli na mkali. Haya yamejidhihiri wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT John Pombe Joseph Magufuli kwenye mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. Hakika naweza kudiriki kusema kuwa kwa mara ya kwanza nimeshuhudia ziara tofauti kabisa. Ziara ya Rais Magufuli ni ya kiutendaji zaidi na kuna maamuzi alikuwa anafanya tit for tat.
Kwa niaba ya wana Kusini wote, natumia ukurasa huu kutoa salamu za pongezi kwa Rais wangu Magufuli kwa yote uliyotufanyia. Binafsi nililazimika kutoka Songea kufuatilia ziara hiyo kuanzia pale Mkuranga, kupitia Nangurukuru, kuelekea Lindi, kuchepuka Mnazimmoja hadi Mtwara. Nililazimika kuacha majukumu yangu ya kibiashara ili nisipitwe kitu kutokana na ziara hiyo hadi ilipokamilika jana jioni.
Mheshimiwa Rais, katika ziara hiyo, Uliweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda kikubwa cha marumaru cha kampuni ya Goodwill pale Mkuranga, Pwani. Ulizungumza mambo mengi kubwa zaidi ni marufuku ya kusafirisha mchanga kwenda nje ya nchi. Nakupongeza sana kwani hapa Watanzania tulikuwa tunaliwa mchana kweupe.
Ukiwa Nangurukuru, ulitoa mchango wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa naye alichangia milioni 10. Wananchi walikushangilia sana kutokana na uamuzi huo kwani huduma ya afya ni kipaumbele namba moja kwao. Baada ya kuondoka kwako, wananchi wameahidi kujitolea ujenzi wa Hospitali hiyo kwa nguvu zao na wamekuahidi kuwa kazi zote ambazo hazihitaji manunuzi kama kuponda mawe, kufyatua matofali na kusomba mchanga watajitolea ili kupunguza gharama za ujenzi na kuharakisha mradi. Wanakushukuru na kukupongeza sana na wameweka ahadi kuwa ikiwa hospitali hiyo itakamilika kabla ya 2020, kura zote watakupa wewe.
Ukiwa mjini Lindi, ulitembelea mradi wa maji pale Ng'apa ambao umeshindwa kukamilika kwa zaidi ya miaka 5. Mheshimiwa Rais, umejionea mwenyewe. Umetoa maagizo kuwa hadi tarehe Moja Aprili 2017, mradi huo uwe umekamilika. Umetoa maagizo kuwa mkandarasi wa mradi huo kutoka India, anyang'anywe hati ya kusafiria ili abaki Tanzania hadi kukamilika kwa mradi. Umetoa maagizo pia kuwa Wizara ya Maji iunde Timu maalum kwa ajili ya kufuatilia mradi huo na wewe ndiye utakaousimamia kwa karibu. Hakika haijapata kutokea. Nimeiona shauku yako ya kutaka Wana Lindi waepukane na kero ya maji iliyodumu kwa muda mrefu. Wananchi wamekushangilia sana na kwa kweli wana imani nawe.
Mheshimiwa Rais, umetoa ufafanuzi wa kero kadhaa zinazowakabili wana Lindi na nyingine umezipatia ufumbuzi. Umewaahidi wana Lindi kuwapelekea kivuko kimoja hata kile cha Kigamboni ili kiwasaidie wana Kusini. Hakika watu wa kule Mitwelo wamefurahi sana. Umewafaa na wamekuahidi hawatakuangusha. Pia umeeleza mkakati wa kuboresha umeme kwenye mikoa ya kusini. Hata hivyo, pamoja na yote uliyoeleza, hili suala la Umeme ambalo hoja yake ilitolewa na Mama Salma Kikwete ni kero kubwa kwa wana Lindi.
Nikuambie kitu, umeme wa REA kwa kweli kwa mikoa ya Kusini umekuwa ndoto. Naweza kusema kuwa zaidi ya robo tatu ya vijiji vya mikoa ya kusini havina umeme. Hivyo, pamoja na kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme, jitihada zifanyike ili kusambaza umeme vijijini. Najua Serikali ilipunguza gharama ya kuunganisha umeme kwa mikoa ya kusini na kufikia 27,000 tu. Hata hivyo, pamoja na wananchi kuwa tayari, REA wapo mbali na fikra za wananchi. Pamulike hapo Rais.
Mheshimiwa Rais, umeeleza nia ya serikali kujenga barabara ya lami kutoka Nangurukuru hadi Liwale. Hata hivyo, pamoja na wana Lindi kuipongeza serikali kwa dhamira hiyo, wananchi hasa wa Nachingwea na Ruangwa wana shauku ya kuona utekelezaji wa mradi wa Barabara kutoka Nanganga - Nachingwea - Liwale - Ruangwa - Nanganga. Mradi huu ukikamilika nakuhakikishia Mkoa wa Lindi utakuwa na kasi kubwa sana kimaendeleo.
Mheshimiwa Rais, Ukiwa Mkoani Mtwara, maelekezo yako kwa watendaji wa Serikali ili kumsaidia mwekezaji wa kiwanda cha Saruji, Aliko Dangote yamewaingia sana wananchi. Watanzania tuna hamu ya kushuhudia gharama ya saruji inashuka ili tujenge nyumba bora. Nafurahi kuwa umegundua kuna Watu wanashinikiza saruji isiuzwe chini ya shilingi 10,000 kutokana na sababu zao binafsi. Hili umelikemea na Watanzania tumekuelewa. Pia umetoa maagizo ya kushughulikia kero zote ili mwekezaji huyo atimize lengo lake. Natoa wito kwa watendaji wa Serikali mliopewa maagizo mahsusi kama kupeleka gesi kiwandani hapo, kutoa leseni ya kuchimba makaa ya mawe kwa Dangote nk kuharakisha ili Kusini ifunguke.
Mheshimiwa Rais, umeagiza watendaji wa Serikali kuitumia benki ya NMB kuweka fedha zao kwa sababu serikali ina share ya asilimia 32. Maagizo haya watumishi wengi wameyafurahia sana kwani wanaamini watapata mishahara kwa wakati. Kwa sasa mishahara inavyoanzia kwenye benki fulani wanaichelewesha kwa zaidi ya siku tatu ili watengeneze faida. Kuna biashara inafanyika hapo na wanaoumia ni wananchi.
Maelekezo yako kuhusu upanuzi wa Bandari ya Mtwara kwa kweli wana kusini tunafurahia sana. Mathalan, ili mafuta yafike Songea, inalazimika kuyasafirisha kwa malori kwa zaidi ya kilomita 900 kutoka Dar es Salaam wakati tungeweza kutumia umbali wa chini ya kilomita 500 kama yangetokea Mtwara.
Wana kusini tumeridhishwa na dhamira yako ya kukamilisha ujenzi wa barabara kutoka Masasi hadi Mbambabay. Kwa kweli ujenzi ni kama upo ukingoni hasa kutoka Tunduru hadi Namtumbo. Yaani tunaona kama ndoto kutembea kwenye barabara ya Lami. Nafurahi kukutaarifu kuwa sasa kuna mabasi yanatoka Mbinga hadi Dar es Salaam tena yana kiyoyozi. Hii ni kama ndoto lakini ndio uhalisia. Yapo mabasi pia yanatoka Songea hadi Mtwara. Hii yote ni kazi yako.
Nikuombe sana Mheshimiwa Rais, fanya sana ziara kama hizi kwenye mikoa yote Tanzania nina hakika utatatua kero nyingi sana. Wakati ule ulipofanya ziara kanda ya Ziwa na kutatua kero zao, sisi wana Kusini tulijawa na wivu sana. Tukadhani ati unapendelea kwako. Ila kwa haya uliyotufanyia wana Kusini, ninadiriki kusema kuwa wewe ni Rais wa wanyonge. Nchi yote ni yako na huna upendeleo. Jana usiku nilikaa na baadhi ya Wachagga na Wasukuma kwenye Hotel ya Nafu ambayo nimefikia, kwa kweli walijawa na wivu sana. Wakasema sasa mbona anawapendelea sana wana Kusini. Nikawauliza, mbona alipofanya ziara kanda ya Ziwa alifanya kama alichotufanyia wana kusini? Basi walibaki wanacheka na sote tukafurahi.
Mheshimiwa Rais, dhamira yako ya kuboresha bei ya zao la korosho tumeipokea kwa mikono miwili. Pia tumeona hisia zako kwa jinsi tulipoacha majani yaote kila mahala huku yakinawiri kutokana na kuwa na mboji nyingi badala ya kulima mazao. Ni kutokana na hali uliyoiona ndipo ulipokazia kauli yako kuwa hutapeleka chakula cha msaada. Kwa hali uliyoikuta mikoa ya Kusini kwa kweli hakuna atakayekulaumu kutokana na kauli yako
Nimalizie kwa kuwaomba Watanzania kumunga mkono Rais Magufuli. Tanzania itaendelea sana chini ya usimamizi wake. Nimuombe tu aache upole. Awe mkali ili upuuzi ulioanza kujitokeza ufutike.
Nawasilisha
Lizaboni, safarini Songea kutoka Mtwara