Salamu za mwaka mpya kwa vijana wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salamu za mwaka mpya kwa vijana wote

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Emil Mwangwa, Dec 30, 2011.

 1. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Salam za mwaka mpya 2012 kwa vijana wote Vijana wenzangu salam.Mimi kijana mwenzenu ni mzima na buheri wa afya. Tumefika mwisho wa mwaka 2011.Tuna kila sababu ya kumshukuru mwenyezi Mungu kwani wengi walipenda kwa gharama zozote zile wafike mwaka mpya lakini hawakuweza,sisi hatukufanya mema zaidi yao kiasi cha kustahili kuwa hai,ni mapenzi yake mwenyezi Mungu kuwa bado tunaishi. Vijana,mwaka uliopita tumeshuhudia mengi,mazuri na mabaya.Mwanzoni kabisa mwa mwaka 2011 tulishuudia vijana wenzetu wawili wakipoteza maisha kule Arusha katika maandamano ya kupigania haki na thamani ya utu wetu.Wametangulia mbele ya haki. Tumeshuhudia mivutano mikali bungeni mpaka kufikia kuzomewa kwa baadhi ya wabunge na hata kususia baadhi ya vikao kwa kutoka nje pale ilipoonekana kuna kupuuzwa kwa hoja za msingi za watanzania.Wabunge walitoka nje wakazomewa lakini ukweli unasimama kwa kuwa hoja zote walizozisimamia zinaungwa mkono na karibu watanzania wote. Tumeshuhudia mbunge mmoja kwa uchungu akijitolea kwenda gerezani kwa hiari yake baada ya kutishiwa mauti na vifungo mara kwa mara na mpaka kufikia wananchi wake kuitwa panya.Kabla ya kuingia gerezani alituasa akisema kama jela tunakwenda kwa ajili ya kupigania haki za watu basi jela ni sehemu salama ya kuishi.Hakuogopa aliingia gerezani akijitolea sadaka maisha yake alijali sana mustakabali wa watu wake na kuacha familia yake nje. Tumeshuhudia maadhimisho ya miaka 50 ya Tanganyika mama yetu ingawa watawala hawakutaka kukutaja nitakutaja na kukumbuka daima.Walituambia tunasherehekea miaka 50 ya Tanzania bara ilhali wakifahamu 9.12.1961 katika ramani ya dunia hakukua na nchi iliyoitwa Tanzania bara,sijui mpaka leo kwa nini hawataki kukutaja mama Tanganyika. Vijana, mwaka 2011 tumeshuhudia hali ya maisha ikizidi kupanda,mfumuko wa bei umepindukia sukari,unga wa sembe,mafuta ya taa vyote viko juu,sijui tukimbilie wapi.Juzi tumesikia wabunge wamejipandishia posho kutoka elfu70 mpaka laki2,wakijinasibu kuwa maisha Dodoma yamepanda.Haya maisha wanayozungumzia ni yepi? Haya haya ambayo wakazi waliovunjiwa nyumba zao Njedengwa wanaishi?,ni haya haya wanayoishi wa Nkuhungu,area A ,area C na UDOM? Haingii akilini kuwa wewe ni mwalimu unalipwa mshahara wa kufundisha alafu unapokea posho kila siku ukihudhuria darasani,bado unapewa pesa za kujikimu na pesa ya mafuta.Ndugu zangu,kulikuwa na tatizo la umeme.Sijui na sielewi kama kuna makusudi ya kutatua tatizo hili.Tulishuhudia vijana wengi wakikosa ajira kutokana na matatizo ya umeme.Tumeshuhudia mengi. Vijana wenzangu,kubwa akatika yote ni kwamba mwaka huu kwa shinikizo la nguvu ya umma,.ndiyo nguvu ya umma tumelazimika kuanza mchakato wa kuandika katiba mpya.Serikali ilileta mswada wa kwanza tuliukataa kwa sababu ulikuwa na mapungufu lukuki.Ukaletwa wa pili (mpya) ukakataliwa ila imetumia nguvu ya Chama Cha Mapinduzi bungeni kuipitisha,Rais mwenyewe alinukuliwa akikiri kuwa kualikuwa na mapungufu katika ule mswaada lakini asipousaini wenzake katika Chama hawatamuelewa,mswaada ukasainiwa,sasa kama Rais alikiri una mapungufu,ameusaini je,sheria hiyo itazaa katiba ya aina gani?.Ngoja tuone. Vijana tunaingia mwaka 2012.Nikitazama mbele naona tuna changamoto nyingi mno.Vijana wengi wengi hawana ajira,hali ya maisha imepanda juu sana.Lakini mimi naamini wanaoweza kubadili muelekeo wan chi hii ni sisi vijana,wanaoweza kuweka misingi imara ya taifa hili kijamii,kisiasa na kiuchumi miaka hata 200 ijayo ni sisi.Ni sisi vijana kama tutaungana na kusimama kwa nia moja tunaweza kuleta mageuzi katika nchi hii,tunaweza.Ni sisi tunaotakiwa kulinda rasilimali zetu na kuhakikisha zinatunufaisha,migodini tunaweza kujenga misingi ya thamani ya utu na kunifaishwa na madini,maofisini na katika kilimo,viwandani na katika biashara tunaweza kuleta mabadiliko kama tukiamua.Tunaweza! Julius Nyerere,Rashid kawawa,Abdulwahid Sykes ,Ally Sykes,Clement Mshana na wengine wengi waliopigania uhuru wetu walipigana wangali vijana.Hawakuogopa,hawakusinzia walikubali kugharimika wakitazamia uhuru wao.walipofikiria kuwa huru walipata msukumo wa kupambana zaidi na mkoloni.Mpaka mkoloni akaondoka.Hawa walijitolea maisha yao.Kama kweli tuko serious na mabadiliko ya kweli,hatuna namna ya kukwepa gharama.Gharama ziko nyingi lakin kubwa ni kutazamia ni nchi ya namna gani tunatamani kuiona.Je, tunataka kuona nchi yenye viwanda,nchi yenye uchumi imara,nchi ambayo watu wake wanamiliki makampuni makubwa ya kimataifa? Ni nchi ipi tunatamani kuiona? Haya yatatufanya tugharamie kwa namana yoyote mabadiliko tunayotaka kuyaona. Vijana msisahau hatuwezi kukwepa siasa.Huwa nawasikia vijana wengine wanasema mimi sipendi siasa.Unaposema sipendi siasa maana yake hauko tayari kwa namna yoyote kushiriki kujenga mifumo mizuri ya upatikanaji wa sera nzuri zinazosaididi kuleta maendeleo.Kwa mifumo yetu sisi hatuwezi kukwepa siasa.Siasa si uongo,siasa si mzaha,siasa si uzushi,siasa si rushwa,siasa si unafiki,siasa si ugomvi,siasa si kutowajibika,hapana hapana.Siasa ni mfumo unaoelekeza ni namna gani mwanadamu atatawala na kutawaliwa na jinsi gani ya kutumia rasilimali zilizopo katika kuleta maendeleo katika jamii husika.Lazima tutofautishe,kuna siasa safi na siasa chafu.Mtu msafi hufanya siasa safi bali mtu mchafu hufanya siasa chafu,..siasa yenyewe iko katikati swala ni watu gani wanafanya siasa.Mimi kwa mtazamo wangu kila mtu ni mwanasiasa,daktari mwalimu,injinia n.k hawa wote ni wanasiasa.Ubunifu na utekelezaji wa sera ndio hasa siasa.mmiliki wa daladala anaweza kusema sitaki mambo yenu ya siasa,lakini leseni ya kufanyia biashara yake anapewa na SUMATRA,ambayo kiongozi wake mkuu(mtunga sera) anateuliwa na wanasiasa ambao wanachaguliwa na wanachi kupitia uchaguzi.Kama hatukuchagua mtu makini huyu atafanya uteuzi mbovu wa SUMATRA ambaye ataweka utaratibu mbovu wa uendeshaji daladala. Mwisho ndugu zangu vijana,tumepata bahati ya kuweka historia.Ni katika Mchakato wa kuandika katiba mpya.Vijana,ushiriki wa kila mmoja wetu ni muhimu.Ni wakati wa kulipa gharama ambayo thamani yake ikiwezekana ikae miaka hata 200 ijayo.Tunataka kuiona Tanzaia ya aina gani? Sema ndiyo kwa Tanzania yenye neema,kwa kuunganisha nguvu zetu kuiandika katiba mpya kama tunavyotaka iwe.Tuwe na Katiba inayothamini utu wa mtu kwamba ni mtoto ama mkubwa,kwamba ni mwanamke au mwanamme,kwamba ni wa kabila hili ama lile kwamba ni ni dini hii ama ile,kwamba ni wa rangi hii ama ile mrefu ama mfupi.Tusiogope.Woga ni kielelezo cha ufukara wa fikra.Tuwaonyeshe wanaotudharau kama tuna nguvu,tuwaambie kwa sauti kuu tanataka maisha bora.Tunataka uchumi imara.Tunataka heshima ya utu wetu.Tunataka uhuru wa nafsi zetu.Hatupaswi kutazama yeyote kama mfano ,sisi tuwe mfano.Namaliza kwa maneno aliyopata kunena Mahtma Gandhi,alisema “be the change you want to see in the world” .Tukitaka badiliko la kweli wewe uwe badiliko kwanza.Ahsante kwa kusoma hapa.Nawatakia Heri na fanaka katika mwaka mpya 2012,Mwenyezi Mungu awafanikishe katika Yote.Saa ya ukombozi ni sasa. Wasaalam ndugu yenu Emil Lusambo
   
Loading...