Salamu za Maalim Seif kwa Wazanzibar

ACT Wazalendo

Verified Member
May 5, 2014
457
1,000
SEFU.jpeg

SALAMU ZA MGOMBEA URAIS NA MWENYEKITI WA ACT WAZALENDO KWA WANANCHI WA ZANZIBAR KUPITIA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUELEKEA TAREHE UCHAGUZI MKUU ULIOPANGWA KUFANYIKA TAREHE 27 NA 28 OKTOBA 2020 KATIKA OFISI KUU YA CHAMA, VUGA , ZANZIBAR 26/10/2020

Ndugu Viongozi wa Chama,

Ndugu Waandishi wa Habari,

Ndugu Wananchi wa Zanzibar.
Awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyenzi Mungu, muumba mbingu na ardhi kwa kutuwezesha kukutana muda huu tukiwa salama. Aidha niwashukuru nyinyi waandishi wa habari pamoja na vyombo mnavyoviwakilisha kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwapasha habari wananchi matokeo yanayoendelea kujiri, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Aidha nichukue fursa hii adhimu kuwashukuru Wananchi wa Zanzibar kwa ujumla, kwa namna walivyoniunga mkono katika kipindi chote cha Kampeni. Nimeweza kufanya mikutano 33 ya kamapeni, 12 Pemba na 21 Unguja. Nimepata moyo sana namna wananchi walivyojitokeza katika mikutano ya kampeni, mwitiko wa kampeni umetoa taaswira ya wazi pasina shaka kuwa ushindi upo upande wetu Inshaa Allah.

Waheshimiwa Waandishi wa Habari na ndugu Wananchi,
Kama mnavyofahamu kuwa kesho Jumanne tarehe 27/10/2020 na Jumatano ya tarehe 28/10/2020 ni siku zilizopangwa kwaajili ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar ambapo wananchi wa Unguja na Pemba watapata fursa ya kuchagua viongozi wao, Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani, sambamba na kuwapigia kura Wabunge na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mazingira ya Uchaguzi wa mwaka huu wa 2020 yameandaliwa na watawala kwa kuwatia khofu kubwa wananchi. Tumeshuhudia jana tu, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ndugu Nassor Ahmed Mazrui alitekwa kihuni na vyombo vya Dola na baadaye kuachiwa majira ya mchana. Tunashangazwa sana na Jeshi la Polisi kwa namna lilivyoshughulikia kadhia hii. Mshangao wetu umekuja pale jeshi hilo lilipoamua kuzishikilia mali zote za Ndugu Mazrui kama kwamba nao walikuwa ni sehemu ya Mpango huu wa utekaji.

Leo hii majira ya asubuhi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama chetu ambaye pia ni Mjumbe wa Timu ya Kampeni ya Taifa, Ndugu Hamad Masoud Hamad, amekamatwa Uwanja wa ndege Pemba akitokea safarini Unguja.

Viongozi wetu 6 wa ACT Wazalendo, Mkoa wa Wete (Ki-chama), wakiongozwa na Abdallah Suleiman Ali, Katibu wa Mkoa, Hassana Abdallah Matungi, Katibu wa Ngome ya Vijana, Moh’d Juma Amour, Mwenyekiti Jimbo la Wete, Issa Rubea Katibu wa Jimbo la wete, Maryam Abdalla, Mjumbe Kamati ya Uongozi na Bi Khamisa Khamis, Mjumbe wa Kamati ya Uongozi leo wameitwa Polisi Wete na kisha wamekamatwa kwa tuhuma ambazo bado hazijabainishwa na jeshi hilo.

Pia leo ni siku ya 12 tangu Viongozi, Wanachama na Mgombea wetu wa Ubunge wa Jimbo la Micheweni, Ndugu Iddi Khatib Hamad, wapo Polisi bila kufunguliwa mashataka.

Zanzibar imegeuzwa kuwa kama “Darfur”, kuna kila aina ya vikosi vya ulinzi, Kuna malefu ya majeshi kutoka bara, pia kuna Vijana wa JKT kutoka bara wameletwa Zanzibar kuisaidia CCM. Wote hawa wametakiwa kupiga kura. Askari waliopangwa katika vituo vya kupigia kura wote wameelekezwa kuwa wanajeshi na JKT wahakikishe hawazuiliwi kupiga kura kesho na watu wengine wote raia wa kawaida wazuiliwe kupiga kura.

Kwa upande wa ZEC nao hawajaacha kuendeleza njama zao ovu za kutaka kuibeba CCM.

Hadi muda huu ninapozungumza nanyi Mawakala wetu wote nchi nzima hakuna aliyepewa Kitambulisho cha Uwakala wakati uchaguzi upo kesho. Maafisa wa ZEC Wilayani wanaendelea kuwasumbua Viongozi wetu.

Pia Wagombea wetu wote na Viongozi wa Chama wamenyimwa fursa ya kuwa waangalizi. Wagombea Waliambiwa wangepatia barua maalum ya utambulisho badala ya vitambulisho. Kwa masikitiko hadi sasa hakuna Mgombea hata mmoja aliyepatiwa barua hiyo.

Haya hayatokei kwa bahati mbaya, yanafanywa na mamlaka pamoja na vyombo vya dola, kwa kudhani kuwa yatawakatisha tamaa Wananchi wa Zanzibar wanaotaka mabadiliko.

Pamoja na kuwepo kwa masuala mengi yasiyo na majibu mpaka sasa kutoka kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, hali inayothibitisha mashaka yetu kuwa ZEC haipo kuendesha uchaguzi huru, wa haki na wa wazi. Wazanzibari wanapaswa kufahamu kuwa ni umoja wetu na mshikamano wetu ndio utakaoleta mabadiliko ya kweli nchini.

Hivyo basi nisisitize msimamo wa Chama chetu kwa Wazanzibari kama ifuatavyo;

Kwa kuwa ZEC imeshindwa kutoa takwimu za Wapiga kura ya mapema na pia kushindwa kuweka wazi majina ya wapigakura hadi sasa niwatake Wananchi wote kujitokeza kwa wingi kesho Jumanne tarehe 27/10/2020 katika vituo vyote vya kupigia kura. Wananchi wote wajitokeze kwa amani, bila vurugu na kudai haki ya kupiga kura kwa amani.

Kwa wananchi watakaokosa fursa ya kupiga kura siku ya Jumanne ya tarehe 27/10/2020 kwa sababu zozote zile, Wasiache kujitokeza tena Jumatano ya tarehe 28/10/2020 ili kutimiza haki yao ya msingi.

Kwa kuwa ZEC imeshajiondolea sifa ya kuwa chombo huru chenye kutenda haki, hakuna sababu ya kuiamini kuwa inaweza kutenda haki wakati wa kutangaza matokeo. Ni wito wetu kwa wananchi wote wakati ukiwadia kusimama kulinda ushindi wetu.

Ndugu Wananchi,
Sisi Viongozi wa ACT Wazalendo tunauhakikishia umma wa Wazanzibari, Watanzania na dunia kwa ujumla, kuwa pamoja na vitimbi vyote vinavyofanywa na ZEC na Vyombo vya dola katu hatutorudi nyuma na tutakuwa bega kwa bega na Wananchi kuvishinda vitimbi hivi vyote. Huu ni mwaka wa mabadiliko hakuna la kutuzuia hadi kuufikia ushindi wetu. Tutasimama kwa pamoja kulinda ushindi wetu.

Maalim Seif Sharif Hamad

Mgombe Urais wa Zanzibar na

Mwenyekiti,

ACT Wazalendo – Taifa.
 
Attachments

  • File size
    186.7 KB
    Views
    5

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
14,488
2,000

Hapo juu nadhani ulimaanisha masheha badala ya Madiwani.
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,193
2,000
Maalim anajua hatashinda kabisa mpaka anakua sema kelele zake tu
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,404
2,000
Maneno ya mgombea binafsi wa Zanzibar Maalim Seif miaka yote kashindwa kujenga upinzani Zanzibar uonekane kama ni taasisi anajijenga yeye tu kwa kutumia muundo mbinu wa chama ndio maana kutwa yeye ndie mgombea uraisi anaelekea miaka 90 anatembea na mkongojo bado anajenga brand name individual badala ya chama

CCM hii brand name individual tunaishinda mapema asubuhi kama ambavyo tutaishinda brand name individual Tundu Lisu ,Sugu,Lema,Mbowe,Halima Mdee ,Msigwa,Zito Kabwe etc
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom