Mbona kama vile milaana kibao unatupatia? Sijui magorofa gani yatuangukie... sijui madaraja gani hayajajengwa kwa ustadi ndo yatuangamize... ujue hatukupenda yaliyowapata..... Usiiombee nchi yetu mabaya.... yakitokea tupambane tutakavyoweza....basi
Nakubaliana nawe kuwa kuishi kwenye mahema ni maisha magumu, sijui yakoje maana kwa kweli sijajaribu, lakini maisha yasiyo na privacy ni magumu. Pole kwa kufiwa na laazizi mke wako.
Lakini kuhusu maisha ya kusonga mbele, nakushauri, kwa vile umeshafahamu kuwa hii serikali haikusaidii chochote, usisubiri kuchimbiwa hadi choo. Kwa vile umeshatambua udhaifu wa serikali yako iliyowekwa madarakani kwa miaka mitano ijayo, usisubiri ikufanyie chochote, kwani haitafanya kitu, bali utaambulia usanii tuu. Tafuta pa kuishi kwa jinsi unavyoweza, we ni mwanaume. Omba msaada kwa marafiki, hata waJF, natumaini hutakataliwa na wote. Achana na serikali. Achana na kuishi kwenye mahema, acha kusubiri choo ijae serikali ije kukuchimbia nyingine. Anza maisha yenye akili upya. Sahau yaliyopita, yaani usipoteze muda mwingi kufikiria uliyokuwa nayo. USHAURI WA BURE, USIOE HARAKA. Ukikiuka hili utalijutia. Subiri wanao wakue kidogo, kisha uoe ukitaka. Pole sana tena. Mungu akubariki.