Saladi zinaweza kustawi nje ya mto?

Saladi zinaweza kustawi nje ya mto?

Sijui kama zina jina jingine zaidi ya tulilolizoea tokea tukiwa wadogo!

Arusha tulikuwa tukiziita SALADI. Na Mwanza napo pia zianitwa hivyo, japo ni watu wachache wanaozifahamu, na hata upatikanaji wake ni adimu. Lakini ukifika soko kuu la

Mwanza unaweza ukabahatika kuzipata.

Kwa kawaida hizo mboga zinaoteshwa pembezoni mwa mto unaotiririsha maji. Sijui kama inawezekana kuziotesha nje ya mto.

Inawezekana kuotesha nje ya mto? Nimejaribu kutafuta taarifa zake mtandaoni lakini sijafanikiwa kuziona. Labda zina jina jingine zaidi ya SALADI?

Msaada tafadhali kwa mwenye taarifa!
Yes unaweza kukuza hata kwenye beseni sema uwe unabadili maji yake hata mara 2 kwa wiki. Kwenye YouTube hutakosa tutorials
 
Kwa maelezo yako hiyo ni watercress au yellowcress. Inahitaji maji mengi kukua.Jina la kisayansi Nastrutium officinale.
Jamii forum ni maktaba inayotembea! Asanteni sana mkuu!
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
SALAD = KACHUMBARI
Ni sahihi! Salad ni KACHUMBARI, lakini pia hiyo mboga ninayoizungumzia tulizaliwa tukaikuta huko kwetu ikiitwa kwa jina la SALADI.

Sijui kwa nini "mabibi" zangu waliita SALADI! Labda kwa kuwa WAZUNGU walikuwa wakizitumia kuandalia SALAD ya mboga za majani, nao wakaishia kuziita SALADI.

Hata sasa ndivyo inavyofahamika Arusha, na hata jijini Mwanza.

Na mimi sikuwa nikizifahamu kwa jina jingine mpaka nilipokutana nalo kwenye huu uzi, kwamba zinaitwa WATERCRESS au YELLOWCRESS!
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kweli nimeiona nayo ni saladi, basi saladi zipo aina nyingi
Ukimwambia mama yangu akuandalie salad, atakuandalia mboga za majani almaarufu kama WATERCRESS. Lakini ukimwambia Mzungu akuandalie SALAD, yeye atakuandalia KACHUMBARI, labda ya WATERCRESS, au LETTUCE, n.k.
 
Hata kachumbali ni salad ya nyanya, vitunguu, matango na ingredients nyingine yoyote unayoweza kuweka.
Lakini pia kuna mboga inayoitwa SALADI kwa baadhi ya mikoa.

Niliifahamu kwa jina hilo tokea nazaliwa hadi nilipokuja kufahamu humu JF kuwa SALADI ni WATERCRESS
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Nawashukuruni nyote! Nishajua cha kufanya. Inawezekana kulima "SALADI" nyumbani kwa matumizi ya nyumbani, na hata "shambani" (large scale) kwa ajili ya biashara.
 

Attachments

  • Watercress_Farm_by_Emma_Boyns(360p).mp4
    11.6 MB
  • How_to_grow_Chinese_watercress_from_cuttings_at_home._如何在家種植扦插西洋菜。(144p).mp4
    5.9 MB
  • HOW_YOU_CAN_GROW_SUPERFOOD_WATERCRESS_in_POTS_successfully___Easy_Method_for_Home_Gardeners(36...mp4
    10.7 MB
  • Planting_Watercress(360p).mp4
    9.6 MB
Nawashukuruni nyote! Nishajua cha kufanya. Inawezekana kulima "SALADI" nyumbani kwa matumizi ya nyumbani, na hata "shambani" (large scale) kwa ajili ya biashara.
 

Attachments

  • how_to_grow_watercress_at_home_in_a_container(360p).mp4
    16.8 MB
Zinalika zikiwa mbichi au baada ya kupikwa
 

Attachments

  • The_Best_Watercress_Salad_Recipe_You_ll_Ever_Eat(144p).mp4
    8.7 MB
  • WATERCRESS_SALAD(144p).mp4
    5 MB
  • Watercress_Salad_Recipe__Shahee_Salad_(144p).mp4
    3.4 MB
  • Simple_Stir_Fry_Watercress_with_Soy_Sauce_Recipe(144p).mp4
    8.5 MB
  • Cooking_Tips___How_to_Prepare_Watercress(240p).mp4
    532.4 KB
Back
Top Bottom