Sala kwa ajili ya taifa

Sala kwa ajili ya taifa

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
408
Ee Mungu uliye mkuu,Mungu usiyeshindwa lolote,Mungu ujuaye mawazo ya kila mmoja wetu,ujuaye kila mmoja awazaye juu ya mwingine.

Mungu wangu,uliiumba Tanzania kwa makusudi yako,ukawaweka wanadamu kwa kusudi lako,ukaweka rasmali kwa ajili ya watz lakini tazama baba umeiweka serikali ya CCM angalia inavyokandamiza haki za watz,angalia rushwa ilivyotamalaki,angalia kashifa za ubadhilifu wa pesa kama EPA,Kagoda,IPTL, Meremeta, uuzaji wa madawa ya kulevya,uuzaji wa wanyama hai,ujangili nk. Mungu nakuomba usikie kilio cha watz, sikia shida zao, tazama wanavyoishi,umaskini umezidi lakini rasimali zinatafunwa na wachache.
Mungu wangu,walinde walio na nia njema na taifa hili kama Joseph Warioba, Butiku, Polepole, Dr.Slaa, Prof.Kabudi, Prof Baregu, Lissu, Mnyika, Mbowe na wengine wengi.

Pia,unajua kusudi la wewe kuiweka ccm madarakani na kumfanya ndugu Kikwete kuwa rais wa awamu ya nne,unajua kusudi la kumfanya dhaifu na mgumu wa kuchukua maamuzi,mgumu kujua shida za watz,kufumbia macho ufisadi nchini,Rushwa nk. Ulifanya hivyo ili ukombozi wa watz upatikane kupitia yeye.

Walinde wanaolitetea taifa hili dhidi ya mafisadi,dhidi ya maharamia(ccm),wanaotaka kutoa roho zao,walinde dhidi ya mateso, maharamia yanatamani yachukue roho zao,yanatamani kuchukua pumzi zao mara moja. Ee Mungu kwa uwezo wako,walinde wanao hawa dhidi ya vifo ,magonjwa,mateso,walinde dhidi ya mabaya yote ambao ccm na serikali yake wamekuwa wakiwawazia.Lilinde taifa hili dhidi ya machafuko,dhidi ya ufisadi.

Iondoe CCM madarakani kwa njia ya amani vinginevyo wanao wenye nia njema na taifa hili wako tayari kushika mabango na kuingia barabarani.Zilinde rasmali za taifa hili zitumike katika kuondoa umaskini wa watz.

Waangamize wote wenye nia mbaya na taifa hili,waliochakachua maoni ya wanao,waliojimiliksha nchi hii,walio tayari kumwaga damu ili waendelee kuiba. Roho za wizi,rushwa,ufisadi,kung'ang'ania madaraka na kutojali mahitaji ya wengine ni roho za kishetani,roho mtakatifu uwanguze na moto wako popote pale walipo.

Sema amina
 
Mbona Laki si Pesa and Co wanabwabwaja maneno? Mna roho za kishetani? Mbona mnahangaika? Kwani CCM ni mashetani?
 
Tunaomba na kushukuru katika jina la Yesu, eeimeen!
 
Back
Top Bottom