Sakata UDA: Hivi ndivyo madiwani na wabunge wa DSM wanavyotuhumiwa kuhongwa kufunika kombe

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,094
  • Yabainika Fedha ziligawanywa kama njugu
  • kila Diwani alihongwa milioni 3 tu kubariki biashara
  • wabunge wote wamehongwa kasoro mdee wa kawe
  • madiwani wagombana kugombea mgao
Na. Mwandishi wetu:

wakati bado wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwa katika sintofahamu kuelekea kutimia kwa siku tano zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulitaka jiji hilo kuitisha kikao na kukubaliana kupanga matumizi ya fedha walizoingiziwa katika akaunti yao kiasi cha bilioni 5.8 zilizoingizwa na kamouni ya Simon Group wanaosemwa kununua asilimia 51 ya hisa za shirika la Usafirishaji Dar es salaam UDA, fedha ambazo halimashauri ya jiji hilo imekataa kuzitumia kwa kudai kwamba ni kidogo na kwamba kuzipokea ni kuhalalisha Ufisadi na upotevu ya mali ya wananchi wa Dae es salaam kwa kuuzwa bei ya kutupwa.

taarifa zimevuja kuwa madiwani waliokutana katika kujadili jambo hilo walikuwa tayari wamepokea rushwa ya shilingi milioni tatu kila mmoja na zawadi nyinginezo ili kupitisha jambo hilo.

''Diwani Asenga yeye alikuwa anatupigia simu na kutuambia tukakutane naye tuchukue pesa zetu za mgao, na kila mtu alikuwa akipokea kati ya shilingi milioni moja mpaka tatu''. kilisema chanzo chetu ambaye pia ni na mjumbe wa halimashauri hiyo ya jiji diwani kutokea manispaa ya temeke.
1.jpg

Meya wa Jiji la Dar es salaam Issaya Mwita.

unajua tarehe 4 mwezi wa 12 mwaka jana tulikutana kamati ya fedha, wakala wa Kisyena aliyempa pesa kutuletea alionekana kutiliwa mashaka, hivyo tukagooma kupokea maagizo yake na kiasi chochote cha fedha kutoka kwake mpaka atakapokuja yeye mwenyewe, na huo ndio ulikuwa msimamo wetu, na tarehe nane mwezi huo huo wa 12 kisyena akaja karimjee pale, akatuhakikishia kila kitu kuwa kipo sawa na tupokee mgao wetu utakaotolewa baada ya yeye kuondoka, na alipoondoka siku mbili baadae asenga akaanza nkupigia simu wajumbe tukachukue mgao wetu huo''. kiliongeza chanzo chetu
mabasi_UDA.jpg

Mabasi ya Uda kabla shirika hilo halijauzwa kiutata

katika hali ya kustaajabisha chanzo chetu hicho kilihoji kama ule ni mradi halali, na biashara iliyofanyika ni halali kwanini mmiliki huyo wa UDA aamue kugawa pesa kwa wabunge na madiwani kama njugu, anaogopa nini?.

''sasa tunashangaa, kama wao wanasema kisyena hana tatizo na mradi ni halali kwanini sasa ameamua kutuhonga mamilioni yote hayo''.? alihoji.

taarifa za uhakika ambazo JAMVI LA HABARI imezipata inasema kwamba katika siku hiyo ya tarehe 8 mwezi wa 12, Kisyena alipoingia ukumbini Karimjee, aliwahakikishia wajumbe kuwa wabunge wote wajumbe wa baraza hilo la jiji ameshamalizana nao Kasoro Halima Mdee tu.

''wabunge wote tumeshamalizana kasoro Mdee peke yake'' alinukuliwa Kisyena katika kikao hicho alichoitwa kutoa uhakika.
MABASI%2B2.JPG

Mabasi mapya ya Mwendokasi yanayotokana na kuuzwa kwa UDA.

taarifa zaidi za uhakika zinasema kuwa wabunge wanaoingia katika halimashauri ya jiji ni watano kuwakilisha wilaya zao ambapo wilaya ya Temeke anaingia Mohamed Mtolea, wilaya ya ilala Mussa Zungu, Wilaya ya Kinondoni Halima Mdee, huku Ubungo ni Saed Kubenea na Kigamboni ni Dkt. Faustine Ndugulile.

taarifa za ndani ya kikao hicho cha tarehe 8 December 2016 zinasema kuwa wakati wajumbe wanauliza kuhusu wajumbe ambao wabunge kwa kisyena yeye alikuwa anajibu tayari tumeshamalizana naye...''Mtolea?? tayari kachukua 5m, Kubenea?? anajibu naye tayari kachukua 5m''. kilisema chanzo chetu.

taarifa zaidi za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa utawanywaji huo wa fedha kwa wabunge hao na madiwani ndio kulikowafanya wabadili kisimamo yao ya awali

''wewe si unakumbuka Kubenea alivyokuwa anaqlishupalia hili jambo?, leo yuko wapi, ameufyata kimyaaa, cheza na kila kitu usicheze na fedha kaka, waswahili wamesema pesa ni sabuni ya roho''. kiliongeza chanzo chetu.

chanzo zhetu kinasema Mgao wa mameya wa manispaa wao ulikuwa tofauti katika hizo milioni tatu tatu na tano tano za wabunge wao walikuwa na kitu kinachoitwa ''special package'

kitendo cha wabunge hao na madiwani kutuhumiwa kupokea rushwa hiyo ya mamilioni ya shilingi ili kukubali kupokea hizo bilioni 5.8 walizozikataa kwa kipindi kirefu sasa, kinatoa taswira kwamba Rais John Pombe Magufuli huenda alidanganywa na wasaidizi wake kuwa hakuna tatizo kwenye mradi huu na kwamba kwa namna Rais Magufuli alivyojitanabaisha, hakika angegundua madudu haya asingekubali kuunga mkono, taarifa za ziada zinaongeza.
maxresdefault.jpg

Halima Mdee mbunge pekee ambaye hakutajwa kuchukua rushwa ya shilingi milioni 5

''tumeandaa ujumbe maalum wa kwenda kumuona Rais Magufuli na kumuelezan kila kitu, tunaimani Rais wetu hawezi furahia ujinga huu, hili shirika lina thamani kubwa sana na umuhimu wake kwa jiji, halipaswi kuuzwa kwa fedha ya kununua nyanya kama hiyo, ujumbe ukimupona Rais tunaamini ataelewa na atawawajibisha wote wanaohusika na ubadhilifu huo''. aliongeza Diwani huyo ambaye kwa sasa tunamuhifadhi jina lake.

jitahada za kuwapata abunge wanaotajwa kuhongwa na madiwani zinaendelea na JAMVI LA HABARI litaendelea kuwahabarisha kwa kadri hatua zitakavyokuwa zinachukuliwa.

SOURCE : JAMVI LA HABARI
----------------------------------------------------------------------------------------------------------
UFAFANUZI
Naona Mjadala huu muhimu wa Rushwa dhidi ya wawakilishi wetu unataka kupotoshwa na kuonekana ni madiwani wa UKAWA tu,
ukweli ni kwamba halimashauri ya jiji inaundwa na CCM, CUF na CHADEMA ambao ndio huitwa UKAWA.

tusichanganye madesa hapa, ngoja nisaidie kutoa mfano mdogo tu kuhusu wajumbe wa jij ambao wanalalamikiwa hapa sio UKAWA peke yao, ni wabunge na madiwani wa vyama vyote nikupe mfano mdogo.

wajumbe wa halimashauri ya jiji ni
- mameya wa manispaa zote tano
- wabunge wawakilishi watano, mmoja kutoka kila wilaya
- madiwani 13

ambapo wabunge wa CCM ni - MUSSA AZAN ZUNGU - wilaya ya Ilala
- Dkt. Faustine Ndugulile - wilaya ya Kigamboni
wabunge wa CHADEMA ni - Halima Mdee - wilaya ya Kinondoni na Saed Kubenea Wilaya ya Ubungo ambapo wilaya ya Temeke inawakilishwa na Mohamed Mtolela wa CUF.

halikadharika Mameya wa Temeke - CCM , meya wa Kigamboni - CCM, na meya wa Kinondoni - CCM wengine ni Meya wa ILALA - CHADEMA, Meya wa Ubungo -CHADEMA na Meya wa Jiji - CHADEMA

Na hata uwakilishi wa Madiwani pia wapo madiwani wa CCM kadhaa, CUF kadha na CHADEMA kadhaa.

hivyo biashara hii imefanywa na watu wa vyama vyote sio UKAWA peke yao, wala sio CCM peke yao
 
  • Yabainika Fedha ziligawanywa kama njugu
  • kila Diwani alihongwa milioni 3 tu kubariki biashara
  • wabunge wote wamehongwa kasoro mdee wa kawe
  • madiwani wagombana kugombea mgao
Na. Mwandishi wetu:

wakati bado wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwa katika sintofahamu kuelekea kutimia kwa siku tano zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulitaka jiji hilo kuitisha kikao na kukubaliana kupanga matumizi ya fedha walizoingiziwa katika akaunti yao kiasi cha bilioni 5.8 zilizoingizwa na kamouni ya Simon Group wanaosemwa kununua asilimia 51 ya hisa za shirika la Usafirishaji Dar es salaam UDA, fedha ambazo halimashauri ya jiji hilo imekataa kuzitumia kwa kudai kwamba ni kidogo na kwamba kuzipokea ni kuhalalisha Ufisadi na upotevu ya mali ya wananchi wa Dae es salaam kwa kuuzwa bei ya kutupwa.

taarifa zimevuja kuwa madiwani waliokutana katika kujadili jambo hilo walikuwa tayari wamepokea rushwa ya shilingi milioni tatu kila mmoja na zawadi nyinginezo ili kupitisha jambo hilo.

''Diwani Asenga yeye alikuwa anatupigia simu na kutuambia tukakutane naye tuchukue pesa zetu za mgao, na kila mtu alikuwa akipokea kati ya shilingi milioni moja mpaka tatu''. kilisema chanzo chetu ambaye pia ni na mjumbe wa halimashauri hiyo ya jiji diwani kutokea manispaa ya temeke.
1.jpg

Meya wa Jiji la Dar es salaam Issaya Mwita.

unajua tarehe 4 mwezi wa 12 mwaka jana tulikutana kamati ya fedha, wakala wa Kisyena aliyempa pesa kutuletea alionekana kutiliwa mashaka, hivyo tukagooma kupokea maagizo yake na kiasi chochote cha fedha kutoka kwake mpaka atakapokuja yeye mwenyewe, na huo ndio ulikuwa msimamo wetu, na tarehe nane mwezi huo huo wa 12 kisyena akaja karimjee pale, akatuhakikishia kila kitu kuwa kipo sawa na tupokee mgao wetu utakaotolewa baada ya yeye kuondoka, na alipoondoka siku mbili baadae asenga akaanza nkupigia simu wajumbe tukachukue mgao wetu huo''. kiliongeza chanzo chetu
mabasi_UDA.jpg

Mabasi ya Uda kabla shirika hilo halijauzwa kiutata

katika hali ya kustaajabisha chanzo chetu hicho kilihoji kama ule ni mradi halali, na biashara iliyofanyika ni halali kwanini mmiliki huyo wa UDA aamue kugawa pesa kwa wabunge na madiwani kama njugu, anaogopa nini?.

''sasa tunashangaa, kama wao wanasema kisyena hana tatizo na mradi ni halali kwanini sasa ameamua kutuhonga mamilioni yote hayo''.? alihoji.

taarifa za uhakika ambazo JAMVI LA HABARI imezipata inasema kwamba katika siku hiyo ya tarehe 8 mwezi wa 12, Kisyena alipoingia ukumbini Karimjee, aliwahakikishia wajumbe kuwa wabunge wote wajumbe wa baraza hilo la jiji ameshamalizana nao Kasoro Halima Mdee tu.

''wabunge wote tumeshamalizana kasoro Mdee peke yake'' alinukuliwa Kisyena katika kikao hicho alichoitwa kutoa uhakika.
MABASI%2B2.JPG

Mabasi mapya ya Mwendokasi yanayotokana na kuuzwa kwa UDA.

taarifa zaidi za uhakika zinasema kuwa wabunge wanaoingia katika halimashauri ya jiji ni watano kuwakilisha wilaya zao ambapo wilaya ya Temeke anaingia Mohamed Mtolea, wilaya ya ilala Mussa Zungu, Wilaya ya Kinondoni Halima Mdee, huku Ubungo ni Saed Kubenea na Kigamboni ni Dkt. Faustine Ndugulile.

taarifa za ndani ya kikao hicho cha tarehe 8 December 2016 zinasema kuwa wakati wajumbe wanauliza kuhusu wajumbe ambao wabunge kwa kisyena yeye alikuwa anajibu tayari tumeshamalizana naye...''Mtolea?? tayari kachukua 5m, Kubenea?? anajibu naye tayari kachukua 5m''. kilisema chanzo chetu.

taarifa zaidi za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa utawanywaji huo wa fedha kwa wabunge hao na madiwani ndio kulikowafanya wabadili kisimamo yao ya awali

''wewe si unakumbuka Kubenea alivyokuwa anaqlishupalia hili jambo?, leo yuko wapi, ameufyata kimyaaa, cheza na kila kitu usicheze na fedha kaka, waswahili wamesema pesa ni sabuni ya roho''. kiliongeza chanzo chetu.

chanzo zhetu kinasema Mgao wa mameya wa manispaa wao ulikuwa tofauti katika hizo milioni tatu tatu na tano tano za wabunge wao walikuwa na kitu kinachoitwa ''special package'

kitendo cha wabunge hao na madiwani kutuhumiwa kupokea rushwa hiyo ya mamilioni ya shilingi ili kukubali kupokea hizo bilioni 5.8 walizozikataa kwa kipindi kirefu sasa, kinatoa taswira kwamba Rais John Pombe Magufuli huenda alidanganywa na wasaidizi wake kuwa hakuna tatizo kwenye mradi huu na kwamba kwa namna Rais Magufuli alivyojitanabaisha, hakika angegundua madudu haya asingekubali kuunga mkono, taarifa za ziada zinaongeza.
maxresdefault.jpg

Halima Mdee mbunge pekee ambaye hakutajwa kuchukua rushwa ya shilingi milioni 5

''tumeandaa ujumbe maalum wa kwenda kumuona Rais Magufuli na kumuelezan kila kitu, tunaimani Rais wetu hawezi furahia ujinga huu, hili shirika lina thamani kubwa sana na umuhimu wake kwa jiji, halipaswi kuuzwa kwa fedha ya kununua nyanya kama hiyo, ujumbe ukimupona Rais tunaamini ataelewa na atawawajibisha wote wanaohusika na ubadhilifu huo''. aliongeza Diwani huyo ambaye kwa sasa tunamuhifadhi jina lake.

jitahada za kuwapata abunge wanaotajwa kuhongwa na madiwani zinaendelea na JAMVI LA HABARI litaendelea kuwahabarisha kwa kadri hatua zitakavyokuwa zinachukuliwa.

SOURCE : JAMVI LA HABARI

tumuombe Mungu atuepushe na mabalaa ya uwakilishi wa aina hii
 
Ukweli ni kuwa kuna mchezo mchafu hapa, isingekuwa Simbachaweni kusema Simon group wametoa 5.8bn tusingeambiwa chochote, baada ya Simbachaweni kuongea na UKAWA ndio wanajidai kuongea ila jiji lipo chini ya UKAWA, transaction ya pesa imefanyika December mpaka saivi February ndio tunaanza kupewa taarifa, huu ni usanii.
 
lakini taarifa zinasema madiwani na wabunge wa vyama vyote wameramba mchongo huo. si CCM wala CUF wala UKAWA
 
MBONA KAMA UME PANIKI HIVI
Hivi mtu duni kama wewe utampanikisha nani kwa propaganda za kiwango cha chini namna hii ?

Sasa hivi dawa yenu ni kuwaanika hadharani wanafiki wote , huyo Magufuli unayeaminisha watu kwamba mmepanga kumuona ndio huyohuyo aliyezindua mradi wa magumashi , watu wamegoma kutumia hela za mafisadi , na mmeona mnaenda kuumbuka ndio mnaleta uzushi .

Dawa yenu inachemka kudadeki !
 
Back
Top Bottom