Sakata linaloendelea ndani ya Simba SC liko hivi...

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Kuna mpasuko mkubwa sana ndani ya klabu ya watani zangu, ila kwa bahati mbaya wengi hawafahamu kwa sababu mpasuko huo umewekwa siri kwa manufaa ya klabu.

Chanzo kimeanzia kwa Barbra Gonzalenz.

Namna ha uendeshwaji wa klabu wa huyu binti unawakwanza sana wenye simba yao. Yes namaanisha wenye simba yao, yaani lile kundi maalumu ambalo hunufaika pakubwa sana na klabu kifedha.

Kundi hilo hawataki kabisa kumuona huyu binti akifanya maamuzi makuu kuanzia msimu ujao.

Wanataka wao ndio waishikilie shoo nzima ya uendeshaji wa klabu. Mo amekwisha poke mapendekezo kutoka kwa kundi hilo. Mapendekezo hayo yamemkwaza sana Mo kiasi kwamba amefanya kama kuipotezea klabu kwenye gharama za usajili za msimu huu. Si mnajua mambo ya Mo ya kususa susa!

Lile kundi bhana ndio wakujita “ marafiki wa simba”.

Hawa jamaa ndio waliotaka kufanya madam ajiuzulu kipindi kile alichotaka kuitisha press. Ni hekima tu ya mmoja wao bwana jaribu tena kumrudisha ili waje kumuondoa kiujanja janja hapo baadae.

Hili kundi linafahamu kuwa boss kawasusia majukumu na anataka kubembelezwa na aombwe msamaha. Marafiki wamegoma kumlamba nyayo muhindi.

Wakaona wajiongeze kusaini mkataba wa M-BET mapema ili kupata pesa za kuendesha klabu lengo kumuonyesha Mo kuwa hata akisusa basi linaweza safiri kwa umbali mrefu.

Jamaa hao hao wakaona wampigie simu adui mkuu wa boss bwana Kigwanomics ili aongeze nguvu kiuchumi kama ikiwezekana. Kigwa akakubari baada ya kupewa simulizi nzima ya kinachoendelea.

Kigwa hatogharamia usajili wa wachezaji ila sasa atakuwa beneti na “marafiki wa Simba” ili kulisukuma basi.

Nitakuwa nikitoa update ya kinachoendelea. Stay tuned.

“WATANI ZANGU JIANDAENI, LESO HAZITOTOSHA BALI TAULO LITAFAA KUFUTA MACHOZI.
 
Unateseka Sana na bado



 
Simba itakutesa Sana


 
Unawashwa sana na mambo ya Simba,,kama kweli Kuna migogoro Simba basi we kama utopolo ndo inabidi ufurahie sasa sio ujifanye unaishauri klabu bora kabisaa Tanzania

Sina uadui na shabiki wa simba sc.

Shabiki wa simba ni MTANI WANGU WA JADI.

Siwezi furahia anguko la mtani wangu
 
Simba itakutesa Sana



Unanikumbusha mbali:

Huu uzi ulifanya Yanga SC wakitoe kwenye huo upuuzi.

Timu ina tajiri mkubwa afrika kuna sababu gani ya kuchangisha masikini bukubuku.
 
Hili linawezekana kabisa yule bibie na boss kubwa wamekua kimya sana...anayejaribu kutamba ni msemaji japo unamuona ni kama hana confiďence flani hivi...

Unajua kuwa hata huyu kocha mpya wa Simba wamemleta wakia Bwana “try again”.

Ndio maana katambulishwa na msemaji.

Madam anavyopenda sifa asinge iacha hiyo fursa.

Pia ni expensive kuvunja moataba wa kocha wa miaka 2 wakaona waingie mwaka 1 ili kuuvinjja iwe kazi nyepesi bila kuhitaji msaada wa Mo Dewji
 
Back
Top Bottom