Bila shaka wengi tunakumbuka sakata la wabunge wa kike wa upinzani kudhalilishwa utu wao bungeni kwa hoja kwamba wameweza kuwa wabunge kwa kuwa na mahusiano na viongozi wakuu wa vyama vyao. Kama jamii inatupasa kukemea tabia hii chafu ya watu kuropoka kwa mihemko ya kisiasa kwa kuwa waliodhalilishwa ni mama zetu, dada zetu na ndungu zetu pia. Vyombo vya habari vilipaswa kukemea jambo hili kwa kuelimisha na kuonya juu ya tabia hii kupitia tahariri zao mbalimbali. Cha ajabu vyombo hivi hasa magazeti yanaripoti katika mtindo wa kushangilia yaliyotokea. Nilitegemea tafakuli za kina juu ya udhalilishaji huu katika njia ya kuelimisha na kuonya. Sasa ni lini mbunge aliyetoa kauli ile atajifunza kuwa ni vibaya kudhalilisha utu wa binadamu. Mbaya zaidi alisahau kuwa mama yake (RIP) naye alikuwa ni mbunge wa kike. Sasa alitaka kufikisha ujumbe kwamba mtindo kama huo ulitumika kumpitisha kugombea ubunge? Mimi binafsi sidhani kama ni hivyo.
Chondechonde vyombo vya habari acheni kuripori katika mtindo wa ushangiliaji bila tafakuli katika baadhi ya mambo ambayo ni nyeti.
Chondechonde vyombo vya habari acheni kuripori katika mtindo wa ushangiliaji bila tafakuli katika baadhi ya mambo ambayo ni nyeti.