Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
KAMPUNI ya Udalali ya Yono ya jijini Dar es Salaam itauza kwa mnada bidhaa zenye thamani ya Sh. bilioni 6.5, ambazo wamiliki wake ni miongoni mwa wafanyabiashara wanaodaiwa kutorosha kontena 329 bila kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kutoka bandari kavu (ICD) ya Azam mwaka jana.
Wafanyabiashara hao walikwepa kodi ya jumla ya Sh. Bilioni 18.
Mwenyekiti wa Yono, Yono Kevela amesema wanatarajia kuanza kuuza mali hizo kuanzia keshokutwa katika maeneo ya Tabata Matumbi, jijini Dar es Salaam.
Amesema wameamua kuuza mali hizo baada ya wamiliki kushindwa kulipa kodi stahiki ambayo walipaswa kuilipa TRA na kwamba iwapo watauza mali hizo na kushindwa kufikia madeni wanayodaiwa, watalazimika kukamata mali zingine.
“Tumeanza rasmi kazi ya kuwafilisi wadaiwa wa kodi ya TRA na tumeanza kumtafuta mmoja mmoja," alisema Kavela.
"Kuna ambao hawajalipa lakini wameonyesha ushirikiano wa kupunguza madeni yao taratibu, hao hatuna shida nao sana lakini wale ambao hawajalipa na hawaonyeshi ushirikiano kabisa tutawafilisi.
” Aidha, Kavela alisema iwapo kampuni yake itashindwa kuwapata baadhi ya wadaiwa wa TRA, watalazimika kukamata mali za Kampuni za Bakhresa ili kufikia kiwango cha fedha kitakachokuwa hakijalipwa, kwasababu wafanyabiashara wanaodaiwa walipitisha mizigo yao kwenye ICD yake.
Alisema bidhaa nyingi zitakazouzwa keshokutwa ni mabati na kwamba yakiisha wataitisha mnada mwingine kwa ajili ya kuuza betri zenye thamani ya Sh. bilioni 7 ili kurudisha kodi ya serikali.
Kuhusu fedha ambazo wameshakusanya tangu kuanza kamatakamata ya mali za wafanyabiashara hao, alisema kwa sasa hana takwimu kamili na Mamlaka ndiyo inaweza kutaja kiasi kwasababu wafanyabiashara wamekuwa wakilipa kwa nyakati tofauti tofauti.
“Takwimu kamili hadi leo waulizeni TRA wao wanajua ni kiasi gani maana mimi nikitaja kwa sasa nitakuwa na takwimu tofauti na Mamlaka kwasababu unaweza kukuta hata muda huu kuna mfanyabiashara kapeleka fedha,” alisema Kevela.
Desemba 12 mwaka jana, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam, Suleiman Kova, alitangaza zawadi ya Sh milioni 20 kwa mtu atakayefanikisha kupatikana kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Regional Cargo Services Ltd, Abdulkadir Kassim Abdi (38).
Mkurugenzi huyo anadaiwa kukimbia nchi baada ya kugundulika kuwa kampuni yake ndiyo ilifanikisha kutorosha makontena 329 kwenye ICD ya Azam bila kulipiwa ushuru wa forodha.
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, Abdulkadir ambaye ni mkazi wa Temeke Mikoroshini ndiye aliyeruhusu kutolewa kwa makontena yote 329.
Licha ya Abdi, mwingine anayetafutwa kwa mujibu wa Kova ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “Jas Express Freight Ltd” na “XL Clearing And Fowarding Co. Ltd,” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo.
Kamanda Kova alisema uchunguzi ulikuwa ukifanywa kwa pamoja na TRA kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2,489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.
Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Machi mpaka Septemba, 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.
Ni miezi mitano sasa imepita tangu Jeshi la Polisi litangaze kumsaka Abdi lakini hadi leo hajapatikana.
Source:Nipashe