Sakata la upotevu maiti sarakasi tupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la upotevu maiti sarakasi tupu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir.JAPHET, Sep 25, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Jumanne, Septemba 25, 2012 06:45 Na Benjamin Masese, Dar es Salaam

  SAKATA la mwili wa marehemu Ntimaruki Khenzidyo (23), uliodaiwa kuibwa Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam na kuzikwa Handeni mkoani Tanga, limechukua sura mpya, baada ya Mahakama ya Kinondoni, kuomba Sh milioni 1.5 ili kutoa kibali cha kuufukua.

  Uamuzi wa kufukuliwa mwili wa Khenzidyo ulifikiwa Dar es Salaama juzi, baada ya kikao kilichofanyika katika kituo cha polisi Oysterbay chini ya Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Moses Fundi.

  Kikao hicho ambacho kilikuwa na mvutano mkali, kilijumuisha polisi, ndugu wa marehemu, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Sofinius Ngonyani na watu waliodaiwa kuusafirisha mwili wa Khenzidyo kimakosa.

  Pamoja na mambo mbalimbali yaliyozungumzwa juzi, waliafikiana mwili wa marehemu Khenzidyo, unatakiwa kufukuliwa na kurudishwa Dar es Salaam, huku mwili wa marehemu Ramadhan Mhina, uliobaki Mwananyamala, unatakiwa kusafirishwa hadi Handeni, lakini makubaliano hayo yamekwama kutokana na kukosa kibali.

  Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, baba mdogo wa marehemu, Jonas Ntayombala alisema, asubuhi walikutana kituo cha Polisi Oysterbay kama walivyokubaliana juzi na Mkuu wa Upelelezi, Fundi na kwenda Mahakama ya Kinondoni, ili kupewa kibali cha kufukua mwili.

  Alisema baada ya kufika mahakamani, walikutana na hakimu mmoja na kumwelezea suala hilo, ambapo aliwataka kwa upande wa ndugu wa marehemu Khenzidyo, kuandika barua ya kuomba kufukua maiti, kitendo ambacho walikipinga vikali.

  “Hakimu alisema, kama ndugu wa marehemu tunataka maiti ifukuliwe, lazima tuandike barua ya kuomba na kisha tulipie Sh milioni 1.5 na baadaye twende Mahakama Kuu kuapishwa.

  “Sisi tulimwambia barua hiyo, inapaswa kuandikwa na uongozi wa Hospitali ya Mwananyamala na kugharamia kiasi hicho, lakini hakimu alipoona tumekataa, alituomba tutoke nje ili wajadiliane na mahakimu wengine.

  “Baada ya muda mfupi walituita na kuendelea kutushauri kutoa fedha, lakini tulikataa kabisa na kuamua kuondoka kwenda Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu, nao hawakuweza kutusaidia lolote.

  “Sasa Mkuu wa Upelelezi kituo cha Oysterbay, Fundi aliamua kuondoka na baadhi ya ndugu zetu kwenda Mahakama Kuu kuangalia kama wanaweza kupata msaada.

  “Kweli Fundi amehaha sana, kwa sababu jana (juzi) kwenye kikao cha pamoja pale Oysterbay, alituhakikishia kusimamia kibali hadi kipatikane na ndio maana hivi sasa anatumia gari lake kwenda huku na kule,” alisema.

  Alisema kama uongozi wa Mwananyamala, ungekuwa unashughuhulikia suala hilo, kusingekuwa na madai ya fedha na hata wangedai gharama zote zingekuwa juu ya hospitali hiyo.

  Naye ndugu wa marehemu Ramadhani Mhina, aliyebaki Dar es Salaam kama mwenyeji wa kuwapeleka Hendeni alikozikwa Khenzidyo, Fadhili Mohamed alisema, mwili wa marehemu Mhina ulifika juzi usiku na taratibu za mazishi zinaendelea.

  MGANGA AJIFUNGIA

  MTANZANIA ilifika katika Ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Sofinius Ngonyani ili kuzungumzia sakata hilo, lakini alikataa kuonana na mwandishi akidai ana wageni muhimu.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
Loading...