Sakata la Ukwapuzi wa UDA kufufuliwa?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
LAAC ilifikia uamuzi huo jana baada ya kukosa majibu ya maswali kadha iliyotaka kufahamu, kutoka kwa uongozi wa mkoa na jiji la Dar es Salaam, ikiwamo nani ni wamiliki wa Uda. Katika swali hilo jina la Profesa Juma Kapuya lilitajwa lakini majibu ya uhalali wake yalikosekana.
Mbali ya Waziri na AG, LAAC pia imeagiza Msajili wa Hazina, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Leseni na Majina ya Biashara (Brela), Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam, Mchumi wa Jiji, Meya wa Jiji, Mkaguzi wa Ndani na Mwanasheria wa Jiji, kufika ili watoe majibu ya kina ili suala hilo lifikie tamati.

Hali hiyo ilijitokeza kamati hiyo ilipoihoji Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam juu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2014/15.

Katika kikao hicho, wajumbe wa kamati hiyo walilaumu halmashauri hiyo kuwa watendaji wake wanajua ukweli kuhusu sakata hilo, lakini hawataki kuusema.

LAAC ilihoji kampuni ya Simon Group iliingiaje katika ununuzi wa hisa za Uda, lakini hakuna aliyetoa majibu ya kueleweka, hivyo kuagizwa kufika mbele ya kamati kwa vigogo hao.

Halmashauri hiyo ilibainisha imewasilisha maombi kwa AG ili kupata ushauri juu ya hatua za kuchukua juu ya uuzwaji wa asilimia 51 ya hisa za Uda, ambazo fedha, Sh. bilioni 4.6, ziko kwenye akaunti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdallah Chikota, aliitaka halmashauri hiyo kuwasilisha mbele ya kamati hiyo taarifa jinsi kampuni ya Simon ilivyoingia kwenye shirika hilo.

Alisema maelezo yameandikwa vizuri kuhusu shirika hilo lakini ilipofika eneo la Simon Group, eneo hilo limerukwa na hakuna taarifa inayoonesha alivyoingia. Alibainisha hakuna mahali panapoonyesha mchakato wa upatikanaji wake.

Aidha, wajumbe waliwabana watendaji wa halmashauri hiyo huku Mbunge wa Ulyankulu (CCM), John Kadutu, akihoji kama halmashauri hiyo inatambua Juma Kapuya ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo.

Mbunge wa Rombo (CHADEMA), Joseph Selasini, alisema anashangazwa na kukosekana kwa taarifa kuhusu kampuni hiyo na kwamba ni vyema halmashauri wakatambua kuwa serikali haijaenda likizo.

“Hawa watendaji wa muda mrefu wanajua ukweli kuhusu hili. Naomba mwenyekiti endapo itabainika wanajua ukweli wawe tayari kuwajibishwa na kuachia ngazi,” alisema Selasini.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, akijibu maswali ya wajumbe hao, alikiri kuwa yeye ameona tatizo hilo kwa kuwa hakuna taarifa yoyote inayoonyesha mchakato uliowezesha kupatikana kwa kampuni hiyo na kuuziwa hisa za Uda.

Kuhusu Sh. milioni 320 zilizoingizwa kwenye akaunti ya Mwenyekiti wa Bodi ya Uda, Iddi Simba, Liana alisema amejaribu kuuliza lakini hajapata majibu na anaendelea "kushangaa hadi kesho".

Mchumi wa halmashauri hiyo, Sarah Yohana ambaye ameshika wadhifa huo tangu mwaka 2013, alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kudaiwa kuwa anajua ukweli, lakini hataki kusema.

Mchumi huyo alisema hakuna nyaraka zinazoonyesha Simon Group ilivyopatikana, isipokuwa kuna taarifa zinazoonyesha iliuziwa hisa na iliyokuwa Bodi ya Uda.

“Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo waliohusika na uuzaji wa hisa hizo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi, Idd Simba, Salum Mwaking’inda na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji, Bakari Kingobi,” alisema.

Alisema hisa zenye thamani ya Sh. bilioni saba ziliuzwa na bodi kwa kampuni ya Simon Group mwaka 2011 wakati yeye akiwa mtumishi.

“Nimekuwa mchumi mwaka 2013, nafahamu mchakato mzima wa namna asilimia 51 ya hisa za jiji ilivyouzwa lakini upatikanaji wa Simon Group sijui lolote Mheshimiwa Mwenyekiti,” alijitetea.

Naye Mwanasheria wa Jiji, Jumanne Mtinangi, alikiri kukosekana kwa nyaraka zinazoonyesha kampuni hiyo ilivyoingia Uda.

Kuhusu umiliki wa Kapuya, alisema hana taarifa zozote isipokuwa anachokumbuka kuna wamiliki wawili au watatu.

SOURCE: IPP Media
 
Mtangulizi wake keshasema kuwa aje na mambo mapya na sio kuharibu aliyoyakuta, naona dalili ya 'kuharibu' dili hapa!
 
Hakuna namna yoyote ya kufukia wizi wa UDA , kila aliyehusika atakamatwa na wananchi kwa utararibu uleule wa kupiga kiberiti vibaka , unaoitwa SHERIA MKONONI , sometimes Mahakama zinaremba sana .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nawaonea huruma. Hakuna mtu anaweza kufunua haya madude. Huu ni ufisadi ambao uko inextricably linked na chama fulani. Wao wanajuana vizuri sana na wako tayari kulindana kwa gharama zozote. Stop wasting your time. Hakuna mwenye ubavu wa kufunua kashfa hii pamoja na nyingine zinazofanana na hii..
 
Back
Top Bottom