Sakata la UDOM na majibu ya rais Magufuli: Siasa imenishinda, natangaza Kustaafu rasmi

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,626
Mpaka hapa nimechoka na sina hamu kabisa...yaani nimepotezwa hata sielewi kuhusu mjadala wa UDOM unahusiana na nini. Nakumbuka awali tuliambiwa kuwa wahadhiri wa wanafunzi hao wamegoma hivyo chuo kikaamua kuwarudisha majumbani wanafunzi hao ili wasiendelee kukaa bure chuoni hapo.

Muda ukatolewa wa wanafunzi hao kuondoka chuoni hapo, muda huo ulidaiwa kuwa hautoshi kwa maana kwao ni mfupi sana, ndipo wakatumwa askari wenye silaha na mbwa kwenda kuhakikisha wanafunzi hao wanaondolewa chuoni kinguvu iwapo watakaidi amri hiyo. Ndipo wabunge walipoyaona mateso ya wanachuo na kuamua kuuleta mjadala wa dharura bungeni na kwa umoja wao bila ya kujali tofauti zao vyama na kiitikadi wakajaribu kushinikiza jambo bila mafanikio.
mbi1.jpg

Cha ajabu kadiri siku zinavyokwenda, sababu zinabadilika badilika, leo hii tunaambiwa sababu ni kwamba wanafunzi wale hawana sifa za kusoma degree ndiyo maana wamefukuzwa (???). Rais anatuambia degree wakati taarifa nyingine zinadai ni wanafunzi wa Diploma, magoli yanazidi kuhamishwa.

Mbaya zaidi wabunge wa upinzani wanabebeshwa lawama kwa kuwatetea 'Vilaza', huku watoa lawama wakijisahaulisha kwamba aliyewadahili 'vilaza' hao na kuona kuwa wanafaa ni serikali hiyohiyo, na mbaya zaidi wanabadilisha hoja ya upinzani, kuwa wanatetea wale kufukuzwa kwa kufeli kwao, wakati madai hayo si ya kweli, ukweli ni kwamba wanachopigania ni logistics, kwamba angalau muda ungeongezwa ili kuwapa nafasi ya kuondoka pasipo dharura na kutoishia 'kudhalilika' mitaani.

Inasikitisha zaidi tunapokuwa na rais anayedhalilisha raia wake kwa kiwango hiki na kuthubutu kuwaita Vilaza, huku akiongea maneno mengi ya masimango. Jambo lingine linalonisikitisha ni kambi ya upinzani kususia vikao vya bunge vitakavyokuwa vikiongozwa na Naibu Spika wakishinikiza eti mpaka jambo lile litakapojadiliwa kwa dharura.

Dharura ambayo haipo tena maana wanafunzi wale wameshafika makwao huku wengine wakiwa wameshaanza kusahau kama waliwahi kuwepo pale UDOM, hapa nashindwa kabisa kuelewa maudhui ya ususaji huu ni yapi hasa. Maana kama wataendelea kususa mpaka mwaka 2020, mwaka ambao wengi wanafunzi hawa watakuwa tayari wameshapata vyuo vingine, wame graduate na tayari wapo makazini, hapo ndiyo ninapochoka.

Upinzani umekurupuka, kama wangejuwa na dhamira ya kitaifa wasingeiteka hoja hii ili kuifanya ni ya upinzani bali wangeshiriki kuipa nguvu ili kuipa sura ya Kibunge zaidi. Lakini uchoyo na ubinafsi ukapelekea wenzao wa CCM waachane nao na waone ni heri warudi ndani kuendelea kuginga meza na kuitikia 'ndiyoo' kuliko 'kuburuzwa' na watu wenye uchu na choyo kuliko wao.

NAOMBA KUPITIA UZI HUU NITANGAZE RASMI KUACHA KUFUATILIA SIASA ZA BONGO. TUKUTANE KWENYE MAJUKWAA MENGINE.

Baada ya kushuhudia uongo, porojo, mizaha na vituko hivi vya wanasiasa wetu, nathubutu Hakuna kitu ambacho sijakisoma au kukisikia kwenye hii dunia.
Nadhani muda umefika sasa wa kuhamia mwezini au sayari nyingine za mbali kabisa.

f82a2b2d016c603ee5ffe0155eab4531.jpg
 
Mkuu nakupa pole ya kutoka moyoni.Nami nimesikitishwa sana na hayo mambo ya sasa.Natamani kujua familia za waliotimuliwa UDOM wana had I gani maana raisKANIACHA hoi,eti Wa toto Wa viongozi nao wanasoma diploma ya ualimu siku hizi badala ya kaenda BOT na TRA! Upinzani nao majangaa!
 
Katika kuweka misingi mipya ya nchi yetu wengi watapata majeraha.Ni lazima wote tukubaliane kwamba hali ni mbaya sana and we must do something.Sasa kwa vile wengi tulishazoea the old system ambayo ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo,tunaona kama we are going to the unknown, ingawa tunakubaliana kwambba we have to go there.Kitu chochote kizuri kina sacrifices,so must be ready to make those sacrifices.
siasa za nchi hii ni ngumu sana...rais anasema anauchungu na masikini halafu watoto wa hao hao masikini anawafukuza kama mbwa na kuwaita vilaza.....
 
Katika kuweka misingi mipya ya nchi yetu wengi watapata majeraha.Ni lazima wote tukubaliane kwamba hali ni mbaya sana and we must do something.Sasa kwa vile wengi tulishazoea the old system ambayo ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo,tunaona kama we are going to the unknown, ingawa tunakubaliana kwambba we have to go there.Kitu chochote kizuri kina sacrifices,so must be ready to make those sacrifices.
ni kweli maana suala la sukari limewaumiza watu wengi sana...na hatma yake haijulikani mpaka leo, angemaliza kwanza kufanya jambo moja akishamaliza ahamie lingine..hii ya kuacha mambo hewani hewani hatutafika popote ni kupoteza muda tu
 
ni kweli maana suala la sukari limewaumiza watu wengi sana...na hatma yake haijulikani mpaka leo, angemaliza kwanza kufanya jambo moja akishamaliza ahamie lingine..hii ya kuacha mambo hewani hewani hatutafika popote ni kupoteza muda tu
Mkuu upo? Kimya sana
 
Haya uwasalimie mkuu sisi bado tunaendeleza mapambano
Mapambano ya wanaolipwa kwa kutengeneza kutetea hoja za upande Fulani dhidi ya hawa wasiolipwa wanaotetea hoja zenye maslahi kwa upande mwingine wa walio wengi. Hata mie nahisi kupumua kidogo
 
Hahahahahah mimi nilijiamulia kubaki na Magufuli tu akikosea tunavumilia akipatia tunampa heko.. Sitaisahau siku niliyoona picha ya Lowassa anakaribiahwa Chadema usiku ule bahari beach nilihisi ni kuchafuana ila niliumia zaidi na siasa siku ile Lowassa anatambulishwa rasmi na Mbowe anammwagia sifa.. Dah ile siku niliichukia sana siasa sana sana ila nilijifunza kitu kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom