Sakata la uchaguzi mkuu TFF, Naibu Waziri MwanaFA amkingia kifua Karia, waziri Kabudi aingilia kati

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
866
Reaction score
805
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Paramagamba Mwaluko Kabudi amelazimika kuingilia kati sakata la uchaguzi mkuu wa TFF baada ya Naibu Waziri wake Hamis Mwinjuma "MwanaFA" kushindwa kuyafanyia kazi mapendekezo ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Taarifa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zinasema kuwa, Naibu Waziri Hamis Mwinjuma ameshindwa kulitolea maelekezo suala la mchakato wa uchaguzi baada ya kupokea uchambuzi wa kitaalamu na mapendekezo ya BMT.

"Suala hilo lilipofika BMT wataalamu walifanya uchambuzi wa kitaalamu na kutoa mapendekezo kwa Naibu Waziri kwa ajili ya maelekezo."

"Mapendekezo ya BMT ni kuwa baadhi ya viongozi wa TFF, vyama vya mikoa, wilaya na vyama shiriki wamezidisha muda wa kukaa madarakani, hawastahili kuwepo muhula wa tatu kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa, lakini Naibu Waziri alikosa maamuzi akaamua kufungia faili kabatini kusikilizia upepo"

"Jambo hilo ndio limemsukuma Waziri Kabudi kuingilia kati. Ameitisha faili na limefikishwa kwake wiki hii, ufumbuzi wa sakata la uchaguzi mkuu wa TFF huenda ukatoka kabla ya wiki ijayo kuisha.", chanzo kilidokeza.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) lilikuwa linapata kigugumizi kuchukua hatua dhidi ukiukwaji wa Sera ya Taifa ya Michezo kutokana ukinzani kutoka kwa Naibu Waziri, Hamis Mwinjuma "MwanaFA"

"Sera ya Michezo ya Taifa inamuondoa Karia kwenye mchakato. MwanaFA na Karia ni marafiki hivyo Naibu Waziri alishindwa kuchukua hatua stahili kwa kuhofia maamuzi yanayomuathiri swahiba wake"

Suala la mgongano wa Katiba ya TFF na Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa lilifikishwa BMT zaidi ya mwezi mmoja uliopita na baadhi ya wagombea urais wa TFF na wanasheria na kutokana na unyeti wake BMT walifanya uchambuzi wa kitaalamu na kulifikisha kwa Naibu Waziri, lakini ameshindwa kulitolea maelekezo kwa BMT ili wachukue hatua stahili.

"Mwanzoni kabisa suala hilo lilifika moja kwa moja kwa Waziri kwa kuwa barua ya mmoja wa wadau wa sheria ilielekezwa kwake. Waziri akaitisha kikao cha Msajili, Katibu Mkuu BMT na Naibu Waziri lakini MwanaFA hakuhudhuria, Waziri akaamua kuahirisha kikao.", alisema.

Taarifa kutoka ndani ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zinaeleza kuwa BMT walishapeleka mapendelezo ya kumng'oa Karia kwenye mchakato wa uchaguzi lakini Naibu Waziri Mwinjuma 'alilifungia kabatini faili' ili lisisogee kokote.

"BMT walilileta hili suala mapema sana. Mapendekezo yao ilikuwa ni kusimamia Sera ya Michezo ya Taifa, jambo ambalo lilikuwa linamuathiri Rais wa TFF,l Karia. Kutokana na athari hizo kwa Karia, MwanaFA alikosa maamuzi akalifungia faili kabatini", chanzo kilisema.

"Unajua Karia na MwanaFA ni maswahiba na wote wanatokea Tanga. Na Karia kupitia influence yake katika mpira wa miguu, kuna namna anamsaidia kwa hali na mali MwanaFA kule jimboni Muheza", kilieleza chanzo.

Mnyetishaji wa habari hizi anaeleza kuwa imekuwa ni kawaida kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Mwaluko Kabudi kumuachia Naibu Waziri wake ashughulikie masuala ya sanaa na michezo lakini katika suala hili la Karia, Naibu Waziri anaathiriwa na maslahi binafsi.

"Kikawaida masuala ya Sanaa na Michezo yanashughulikiwa na Naibu Waziri moja kwa moja ndio maana sakata hilo lilikuwa mezani kwa MwanaFA lakini sasa Waziri kaona alishughulikie mwenyewe"

Taarifa zinaeleza kuwa Naibu Waziri anashindwa kusimamia sheria linapokuja suala ambalo ana maslahi nalo akitolea mfano pia sakata la mechi ya Simba na Yanga lililomalizika hivi karibuni.

"Angalia hata suala la dabi ya Simba na Yanga, Waziri Kabudi alikuwa very smart, alieleza masuala hayo hayawezi kushughulikiwa na serikali lakini Naibu Waziri Mwinjuma alijitokeza hadharani mara tatu kutaka mechi lazima ichezwe".

"Ukiangalia chanzo cha mechi hiyo kutokuchezwa Machi 08 ni Naibu Waziri aliyeagiza geti lisifunguliwe. Haya yote aliyafanya kutokana na Usimba wake. TFF nao wakabariki ukiukwaji wa kanuni wa Simba", alisema.

"Karia na MwanaFA ni Simba damu. Pia wote wanatoka Tanga. Suala la dabi liliwapalia mpaka imebidi likaamuliwe na mamlaka za juu. Hili peke yake lingetosha kuwajibika. Lakini gharama zote hizi wanazipata kwa sababu ya Simba yao."

"Sasa hili suala la uchaguzi wa TFF nalo lilikuwa linaelekea huko huko. Waziri Kabudi ameona aingilie kati mapema lisije likawa gumu kama dabi. Kabla ya wiki ijayo atakuwa ameshalitolea maelekezo", alisema.

Uchaguzi mkuu wa TFF unepangwa kufanyika Agosti 16 mwaka huu lakini mchakato wa uchaguzi ni kama umepata ganzi baada ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi kushindwa kusikiliza rufaa za wagombea wanne wiki mbili baada ya rufaa kukatwa.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba alisema maendeleo ya mchakato wa uchaguzi yanasubiri Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wanaotakiwa kusikikiza na kutoa matokeo ya rufaa ya wagombea waliokata rufaa.

"Kamati ya Rufaa wakimaliza kazi yao ndipo sisi tutaendelea na mchakato. Lakini kabla ya kuendelea na mchakato sekretarieti ya TFF inatakiwa kutuandalia kikao. Kwa sasa sekretarieti wanaonekana wako busy na CHAN"

Haikufamika mara moja kwanini Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi imeingia ubaridi kusikiliza rufaa za wagombea.

"Hauwezi kusema Kamati ya Rufaa nayo imeathiriwa na CHAN kwa sababu wajumbe wake sio wajumbe wa Kamati ya CHAN, labda uwatafute TFF wenyewe wanaweza kukuelezea" alisema.
 
Waziri wa Michezo na sanaa yupo kwa ajili ya muziki mpira na kanuni zake anasumbuka kidogo aliwahi kuwaamisha washabiki wa Simba kuwa mechi vs Berkane itachezwa Mkapa wakati CAF washatangaza Zanzibar hawezi kutatua tatizo la Karia TFF..
 
Kuna watu serikalini wanaitwa Bureaucrats utawaona wanavyoongea, wanavyovaa, wanavyonyoa, hawa ni maroboti hufanya yale tu sheria, kanuni, miongozo na taratibu za kazi zinavyosema, hawana undugu wala urafiki, kina FA sijui kidoti na wengine wengi wasio na kaliba ya bureaucrats si miongoni mwao, huwa naona ni masela tu wamedaka vitengo kutokana na upepo wao, huwa nikiona aibu sana kuangalia baadhi ya mawaziri wasio na hiyo kaliba , yule kipara wa tff hataki kuachia goli hadi aipe Simba ubingwa jambo ambalo ni gumu zaidi ya ngamia kupenya kwenye tundu la sindano maana Yanga ni bingwa kwa quality players wameshindikana, kombe letu miaka kumi, huyu kipara hana aibu, atoke sasa ligi irudishe hadhi , msimu ulioisha kauharibu vibaya mno marefa wameibeba Simba bila aibu mpaka mpira umekosa vibe na kuzishusha daraja timu nyingi kwa uonevu, genge lake la kihuni limeharibu vibe ya derby na kuwaibia watanzania kupitia tickets zao maana wengi hawakurudi tena kutokana na stori za tunacheza hatuchezi vurugu tupu, biashara zikaharibika, hasara zikawapata wengi, huyo waziri aoneshe ukubwa wake afanye Sheria inavyosema sijui katiba na mapendekezo ya BMT maana akipuuza kuna siku yatamrudia yeye faili likienda mbele, amtoe kipara tu kwasasa hana faida, nchi masikini zinachosha sana mambo ya viongozi wake ni hovyo kabisa, wengi hawana faida hasa mawaziri.

By the way, for Eng Hersi please chukua Yakub Selemani nimemuona mechi nyingi za taifa Stars , ni kipa Bora kabisa sasa anastahili kucheza Yanga, anaongea mno na mabeki, anapanga ukuta vizuri mno, anacheza krosi zote anapaa hewani kama nyani, ana foot work nzuri, ana kimo kizuri, huyu ni mbadala wa Diarra siku akitimka au akiumwa au kupumzika, huyu ni screen protector number 2 Yanga naomba tumsajili haraka huyu kipa for CAF champion league, kawaida huwa sikosei!
 
Uwezo wa mwana FA ni mdogo sana na hii ni moja ya legacy ya magufuli msimu uliopita yeye na karia walikusudia kuharibu ligi maksudi ili tu simba achukue kombe baada ya kugundua hana quality ya kushindana na Simba uwanjani na kama wangefanikiwa ingekuwa a new normal

Hii kubebwa bebwa ndo imemfikisha mwana Fa hapo alipo ni aibu sana
 
Hivi,mudawote hup FIFA bado inawatazama tu ,mmesahau miaka 10 tz bila kujihusisha na mpira ,sasa hivi itakuwa 30
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Paramagamba Mwaluko Kabudi amelazimika kuingilia kati sakata la uchaguzi mkuu wa TFF baada ya Naibu Waziri wake Hamis Mwinjuma "MwanaFA" kushindwa kuyafanyia kazi mapendekezo ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Taarifa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zinasema kuwa, Naibu Waziri Hamis Mwinjuma ameshindwa kulitolea maelekezo suala la mchakato wa uchaguzi baada ya kupokea uchambuzi wa kitaalamu na mapendekezo ya BMT.

"Suala hilo lilipofika BMT wataalamu walifanya uchambuzi wa kitaalamu na kutoa mapendekezo kwa Naibu Waziri kwa ajili ya maelekezo."

"Mapendekezo ya BMT ni kuwa baadhi ya viongozi wa TFF, vyama vya mikoa, wilaya na vyama shiriki wamezidisha muda wa kukaa madarakani, hawastahili kuwepo muhula wa tatu kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa, lakini Naibu Waziri alikosa maamuzi akaamua kufungia faili kabatini kusikilizia upepo"

"Jambo hilo ndio limemsukuma Waziri Kabudi kuingilia kati. Ameitisha faili na limefikishwa kwake wiki hii, ufumbuzi wa sakata la uchaguzi mkuu wa TFF huenda ukatoka kabla ya wiki ijayo kuisha.", chanzo kilidokeza.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) lilikuwa linapata kigugumizi kuchukua hatua dhidi ukiukwaji wa Sera ya Taifa ya Michezo kutokana ukinzani kutoka kwa Naibu Waziri, Hamis Mwinjuma "MwanaFA"

"Sera ya Michezo ya Taifa inamuondoa Karia kwenye mchakato. MwanaFA na Karia ni marafiki hivyo Naibu Waziri alishindwa kuchukua hatua stahili kwa kuhofia maamuzi yanayomuathiri swahiba wake"

Suala la mgongano wa Katiba ya TFF na Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa lilifikishwa BMT zaidi ya mwezi mmoja uliopita na baadhi ya wagombea urais wa TFF na wanasheria na kutokana na unyeti wake BMT walifanya uchambuzi wa kitaalamu na kulifikisha kwa Naibu Waziri, lakini ameshindwa kulitolea maelekezo kwa BMT ili wachukue hatua stahili.

"Mwanzoni kabisa suala hilo lilifika moja kwa moja kwa Waziri kwa kuwa barua ya mmoja wa wadau wa sheria ilielekezwa kwake. Waziri akaitisha kikao cha Msajili, Katibu Mkuu BMT na Naibu Waziri lakini MwanaFA hakuhudhuria, Waziri akaamua kuahirisha kikao.", alisema.

Taarifa kutoka ndani ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zinaeleza kuwa BMT walishapeleka mapendelezo ya kumng'oa Karia kwenye mchakato wa uchaguzi lakini Naibu Waziri Mwinjuma 'alilifungia kabatini faili' ili lisisogee kokote.

"BMT walilileta hili suala mapema sana. Mapendekezo yao ilikuwa ni kusimamia Sera ya Michezo ya Taifa, jambo ambalo lilikuwa linamuathiri Rais wa TFF,l Karia. Kutokana na athari hizo kwa Karia, MwanaFA alikosa maamuzi akalifungia faili kabatini", chanzo kilisema.

"Unajua Karia na MwanaFA ni maswahiba na wote wanatokea Tanga. Na Karia kupitia influence yake katika mpira wa miguu, kuna namna anamsaidia kwa hali na mali MwanaFA kule jimboni Muheza", kilieleza chanzo.

Mnyetishaji wa habari hizi anaeleza kuwa imekuwa ni kawaida kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Mwaluko Kabudi kumuachia Naibu Waziri wake ashughulikie masuala ya sanaa na michezo lakini katika suala hili la Karia, Naibu Waziri anaathiriwa na maslahi binafsi.

"Kikawaida masuala ya Sanaa na Michezo yanashughulikiwa na Naibu Waziri moja kwa moja ndio maana sakata hilo lilikuwa mezani kwa MwanaFA lakini sasa Waziri kaona alishughulikie mwenyewe"

Taarifa zinaeleza kuwa Naibu Waziri anashindwa kusimamia sheria linapokuja suala ambalo ana maslahi nalo akitolea mfano pia sakata la mechi ya Simba na Yanga lililomalizika hivi karibuni.

"Angalia hata suala la dabi ya Simba na Yanga, Waziri Kabudi alikuwa very smart, alieleza masuala hayo hayawezi kushughulikiwa na serikali lakini Naibu Waziri Mwinjuma alijitokeza hadharani mara tatu kutaka mechi lazima ichezwe".

"Ukiangalia chanzo cha mechi hiyo kutokuchezwa Machi 08 ni Naibu Waziri aliyeagiza geti lisifunguliwe. Haya yote aliyafanya kutokana na Usimba wake. TFF nao wakabariki ukiukwaji wa kanuni wa Simba", alisema.

"Karia na MwanaFA ni Simba damu. Pia wote wanatoka Tanga. Suala la dabi liliwapalia mpaka imebidi likaamuliwe na mamlaka za juu. Hili peke yake lingetosha kuwajibika. Lakini gharama zote hizi wanazipata kwa sababu ya Simba yao."

"Sasa hili suala la uchaguzi wa TFF nalo lilikuwa linaelekea huko huko. Waziri Kabudi ameona aingilie kati mapema lisije likawa gumu kama dabi. Kabla ya wiki ijayo atakuwa ameshalitolea maelekezo", alisema.

Uchaguzi mkuu wa TFF unepangwa kufanyika Agosti 16 mwaka huu lakini mchakato wa uchaguzi ni kama umepata ganzi baada ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi kushindwa kusikiliza rufaa za wagombea wanne wiki mbili baada ya rufaa kukatwa.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba alisema maendeleo ya mchakato wa uchaguzi yanasubiri Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wanaotakiwa kusikikiza na kutoa matokeo ya rufaa ya wagombea waliokata rufaa.

"Kamati ya Rufaa wakimaliza kazi yao ndipo sisi tutaendelea na mchakato. Lakini kabla ya kuendelea na mchakato sekretarieti ya TFF inatakiwa kutuandalia kikao. Kwa sasa sekretarieti wanaonekana wako busy na CHAN"

Haikufamika mara moja kwanini Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi imeingia ubaridi kusikiliza rufaa za wagombea.

"Hauwezi kusema Kamati ya Rufaa nayo imeathiriwa na CHAN kwa sababu wajumbe wake sio wajumbe wa Kamati ya CHAN, labda uwatafute TFF wenyewe wanaweza kukuelezea" alisema.
Upigaji tiefuefu unaratibiwa na hawa wawili , huyuana mpigia pasi huyu, na huyuana Rudisha mpira kwa huyu.
Vizuri Waziri kashtukia michezo.
 
Mwana FA unaleta uswahiba kwenye mambo ya msingi! Unafahamu wadau wa michezo tuliteseka kwa miaka mingapi pale Muhidin Ndolanga alipojimilikisha FAT?

Baada ya kufanikiwa kwa mbinde kumuondoa madarakani ndipo ikaanzishwa hii TFF! Leodgar Tenga, rais wa kwanza alihudumu kwa mihula miwili tu akaachia ngazi (na huyu alikuwa ni rais bora sana kuwahi kutokea), akaja Jamal Malinzi naye akahudumu vipindi viwili, akaondoka!

Sasa inakuwaje unataka swahiba wako Wallace Karia ahudumu vipindi vitatu, kinyume kabisa na sera ya michezo ya Taifa inayotaka viongozi wa vyama vya michezo kuhudumu vipindi viwili pekee?

Mwana FA, you are a snitch!
 
Hatari
 
Kuna watu serikalini wanaitwa Bureaucrats utawaona wanavyoongea, wanavyovaa, wanavyonyoa, hawa ni maroboti hufanya yale tu sheria, kanuni, miongozo na taratibu za kazi zinavyosema, hawana undugu wala urafiki, kina FA sijui kidoti na wengine wengi wasio na kaliba ya bureaucrats si miongoni mwao, huwa naona ni masela tu wamedaka vitengo kutokana na upepo wao, huwa nikiona aibu sana kuangalia baadhi ya mawaziri wasio na hiyo kaliba , yule kipara wa tff hataki kuachia goli hadi aipe Simba ubingwa jambo ambalo ni gumu zaidi ya ngamia kupenya kwenye tundu la sindano maana Yanga ni bingwa kwa quality players wameshindikana, kombe letu miaka kumi, huyu kipara hana aibu, atoke sasa ligi irudishe hadhi , msimu ulioisha kauharibu vibaya mno marefa wameibeba Simba bila aibu mpaka mpira umekosa vibe na kuzishusha daraja timu nyingi kwa uonevu, genge lake la kihuni limeharibu vibe ya derby na kuwaibia watanzania kupitia tickets zao maana wengi hawakurudi tena kutokana na stori za tunacheza hatuchezi vurugu tupu, biashara zikaharibika, hasara zikawapata wengi, huyo waziri aoneshe ukubwa wake afanye Sheria inavyosema sijui katiba na mapendekezo ya BMT maana akipuuza kuna siku yatamrudia yeye faili likienda mbele, amtoe kipara tu kwasasa hana faida, nchi masikini zinachosha sana mambo ya viongozi wake ni hovyo kabisa, wengi hawana faida hasa mawaziri.

By the way, for Eng Hersi please chukua Yakub Selemani nimemuona mechi nyingi za taifa Stars , ni kipa Bora kabisa sasa anastahili kucheza Yanga, anaongea mno na mabeki, anapanga ukuta vizuri mno, anacheza krosi zote anapaa hewani kama nyani, ana foot work nzuri, ana kimo kizuri, huyu ni mbadala wa Diarra siku akitimka au akiumwa au kupumzika, huyu ni screen protector number 2 Yanga naomba tumsajili haraka huyu kipa for CAF champion league, kawaida huwa sikosei!
Umeongea mengi ya maana ulipofika hapo unaposema hawezi kuondoka madarakani bila kuipa simba ubingwa nikajiuliza kama una akili ndogo hivi marinda ipo salama kweli
 
Back
Top Bottom