Sakata la TZS 1.5 Trilioni: Serikali yakiri haikupeleka Zanzibar TZS 204 Bilioni

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Serikali imekiri kudanganya kuhusu TZS 204 Bilioni za Zanzibar Katika Sakata la TZS 1.5 trilioni!

Katika majibu ya Serikali Kuhusu kutoonekana kwa TZS 1.5 trilioni, Serikali ilisema kuwa ilipeleka Zanzibar jumla ya TZS 203.9 bilioni ( transfer to Zanzibar). Tuliijibu Serikali kuwa haikuwa kweli Kwani makusanyo ya Zanzibar hubakia Zanzibar hivyo haiwezekani kuwa Serikali ya Muungano ilipeleka fedha Zanzibar. (Maelezo yetu yapo hapa chini ).

Jana Serikali imekiri kuwa maelezo yetu ni sahihi na Fedha ya Zanzibar haivuki maji hivyo kufanya majibu ya Serikali ya awali kupoteza maana. Serikali ilitaka kutumia kichaka za Zanzibar kujificha kwenye sakata hili. Maelezo mapya ya Serikali haya ( Serikali yafunguka sakata la trl. 1.5 ).

Serikali pia imekiri kuwa unapaswa kufanyika uchunguzi wa kina kupitia miamala ya TZS 1.5 trilioni ili kuthibitisha zilipo. Gazeti la The Citizen wamemnukuu vizuri Naibu Waziri wa Fedha ( Govt: No proof of corruption yet in connection to ‘missing’ ).

Hii inadhihirisha kuwa Majibu ya awali ya Serikali yalikuwa ni ya kujikosha na yamefutwa na kauli za sasa. Bado kuna haja ya Kamati ya PAC kuagiza Ukaguzi Maalumu kwenye miamala ya TZS 1.5 trilioni na kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu Kuhusu upotevu wa fedha hizo.

—————————

Maelezo ya Ado Shaibu kuhusu Fedha za Zanzibar katika TZS 1.5 trilioni

> Makusanyo ya TRA ya Zanzibar Hubaki kwa SMZ, Hayatokei Kwenye Hesabu za SMT

Kikawaida makusanyo ya TRA Zanzibar hubaki Zanzibar, hutuzwa kwenye akaunti za SMZ Katika Benki Kuu na huhesabika kuwa ni mapato ya Zanzibar, Kamwe fedha hizi hazichanganywi na mapato ya Serikali ya Muungano. Makusanyo haya, pamoja na matumizi yake, hukaguliwa na Ofisi ya CAG Zanzibar. Hivyo basi, hesabu zake hazitarajiwi kutokea kwenye ripoti ya CAG iliyokabidhiwa bungeni.

Ndio maana taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Zanzibar ya mwaka 2016/17 imeeleza namna makusanyo husika ya TRA na ZRB yalivyofanyika na namna fedha hizo zilivyotumika katika miezi 9 ya mwaka wa fedha 2016/17. Fedha zote za TRA Zanzibar kwa miezi hiyo 9 zimekusanywa na kubaki chini ya SMZ, na kutumika na SMZ bila kupitia SMT.

Mpaka Machi, 2017, Fedha ambazo SMZ hawakuwa wamekusanya kutoka TRA Zanzibar ni mapato tarajiwa ya robo ya mwisho wa mwaka (Aprili - Juni, 2017) yaliyokadiriwa kufikia shilingi 52.8 bilioni tu.

4. PAYE za Watumishi wa SMT Walioko Zanzibar Hukusanywa na SMT kwa Niaba ya SMZ

Fedha pekee za mapato ya kikodi ambazo Serikali ya Muungano huzikusanya kwa niaba ya SMZ, ni fedha za makato ya Kodi (PAYE) za watumishi wa Serikali ya Muungano wanaofanyakazi Zanzibar, watumishi hawa ni kama Polisi, Wanajeshi nk. Fedha hizi hukusanywa kila mwezi na TRA makao makuu, hutunzwa kwenye akaunti ya hazina Benki Kuu ya Tanzania, na kisha hupelekwa hazina ya Zanzibar.

Fedha hizi hukusanywa kila mwezi, na zinapaswa kupelekwa Zanzibar kila mwezi ili kugharamia shughuli mbalimbali za SMZ. Kwa mwaka wa fedha wa 2016/17, matarajio ya makusanyo PAYE yalikuwa ni shilingi 21 bilioni. Kwa kuwa idadi ya watumishi hawa inafahamika, Wizara ya Fedha ya Zanzibar, wakati ikielezea utekelezaji wa Bajeti ya 2016/17, ilionyesha kuwa yalikusanywa yote kwa 100%.

5. Juni 30, 2017 akaunti ya Zanzibar BoT Ilikuwa na Shilingi Bilioni 14 tu.

Fedha za Zanzibar kwenye akaunti zake Benki Kuu (BOT) zinaweza kuonekana kwa urahisi kwenye Hesabu za Benki Kuu. Hesabu za BOT kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2017 hazionyeshi uwepo hizo shilingi 203.9 bilioni ambazo SMT wanadai kuikusanyia SMZ. Hata wakati wa kufunga hesabu za BOT kwa mwaka 2016/17 fedha pekee zilizokuwa kwenye akaunti hiyo zilikuwa ni shilingi Bilioni 14. Hivyo sio sahihi hata kidogo kwa Taarifa ya Naibu Waziri Fedha kuonyesha kuwa kulikuwa na ‘transfer to Zanzibar’ kutoka Makusanyo ya Mapato ya Serikali ya Muungano.

Serikali Ijibu Maswali Haya. Isituhadae!

Maelezo ya SMT bungeni ni kinyume na nyaraka za BOT, pamoja na taarifa za Wizara ya Fedha na Mipango ya Zanzibar. Ni vema sasa SMT ijibu chanzo cha mapato haya ya kikodi (203.9b) ni kipi? Kama fedha zilizokusanywa na TRA Zanzibar, zimeonywesha na SMZ kwenye BLW kuwa zimekusanywa, kubaki na kutumika Zanzibar, hizi SMT inazodai kuikusanyia Zanzibar na kukaa nazo kwa mwaka mzima ni zipi? Na ziko wapi? Fedha hizi zimekusanywa na kulipwa Zanzibar kupitia akaunti gani? Zanzibar wamepewa lini fedha hizi? Matumizi yake ni yapi kwa mujibu wa bajeti iliyopitishwa na BLZ? Je utaratibu wa makusanyo ya Zanzibar umebadilika na sasa Fedha za Zanzibar zinakaa Hazina ya Muungano? Kama utaratibu umebadilika, ulibadilika lini na je utaratibu mpya una ridhaa ya Baraza la Wawakilishi?

Kwa taarifa ile ya Serikali Bungeni, mpaka Juni 30, 2017, ni wazi kuwa SMT bado ilikuwa imezishikilia fedha za SMZ, ambazo kikawaida hutolewa kila mwezi ili kuwezesha Zanzibar kujiendesha. Tukiamini kuwa huu ndio ukweli, na kuwa bunge halijadanganywa, basi ni dhahiri kuwa tunapaswa kuamini kuwa Serikali ya Zanzibar ilikuwa inajiendesha kwa MIUJIZA, ikikusanya mapato HEWA na kufanya matumizi ya KUFIKIRIKA ya mishahara, ruzuku, pensheni kwa wazee na miradi ya maendeleo.

Maana ni jambo lisiloweza kuingia akilini kuwa Fedha zote zinazokusanywa kwa niaba ya Zanzibar Katika mwaka 2016/17 hazikutolewa kwenda Zanzibar na kubakia Bara mpaka baada ya mwaka kuisha. Pia taarifa za mwenendo wa Akaunti za SMZ zilizoko BOT ni uthibitisho wa dhahiri kuwa hakukuwa na fedha za SMZ, shilingi 203.9 bilioni zilizoshikiliwa na SMT wakati au mara baada ya mwaka wa fedha wa 2016/17 kuisha.

Kama SMT wanadai kubaki na fedha hizi kwa mwaka mzima wa fedha (2016/17), na kushindwa kuziwasilisha hesabu zake kwa CAG miezi mitatu baada ya mwaka wa fedha kufungwa (Septemba 2017), na hata kwenye Exit Meeting (Januari 2018), ni vema waonyeshe tu hata walikozitunza katika akaunti zao BOT.

Shilingi 1.5 trilioni ni karibu mara 2 ya bajeti yote ya Zanzibar, kupotea namna hii na maelezo ya kupotea kwake yawe ni uongo wa kuisingizia Zanzibar ni dharau kubwa kwa Zanzibar, ni kuidogosha Zanzibar, ni kitengeneza kero mpya ya muungano wetu kwa SMT kuitupia madudu yake SMZ, ni hadaa kwa umma, ni kutudharau Watanzania. Hatutakubali. Tutaendelea kuhoji ziliko shilingi 1.5 trilioni zetu mpaka tujue ziliko.

[HASHTAG]#1Point5TrilioniZipoWapi[/HASHTAG]?
 
Kabla haujaja na hii taarifa kuna nyuzi zilifululiza kuonyesha kua na wewe ni fisadi vilevile.

Inachoonyesha walijua kua watakuja kuusema ukweli ila mjumbe wetu upakwe matope ufike unanuka ili tusikusikilize kwa kinyaa.

Lakini unawaaminije watu wanaodai barua ni feki na wanamsimamisha mtu kazi hapohapo?
 
Zitto taarifa hizi zimenifurahisha lakini zingenifurahisha zaidi ningezipata kwa wabunge wetu wa Zanzibar.

Sisi wengine sio wanasiasa pengine wamefahamishwa mambo yao yote waweke siri wakayatoe kwenye makao makuu yao.

Nakupongeza sana unaposimamia haki bila ya ubaguzi. Hukuegemea kwenye siasa tu upo kila sehemu.

Mungu akutie Nguvu, Mungu ndie mtegemewa wetu.
 
Watuambie sasa trillion 1.5 ziko wapi na zinafanya kazi gani laa sivyo huu utakuwa ufisadi mkubwa kuwahi kutokea katika awamu zote za urais wa nchi hii.

Na mbaya zaidi utakuwa umefanywa na serikali inayojidai kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha zetu za kodi
 
Hongera Zitto na wabunge wengine wote mnaofuatilia upotevu huu wa pesa. Mnajenga mwelekeo mzuri. Japo kwa udikteta wanaweza kupuuza lakini angalao watajua kuwa wakitumia pesa ya umma kama ya familia yao, wataulizwa.

Hili sakata kama ingekuwa ni mtu wa kawaida, alistahili kufunguliwa kesi ya wizi, uhujumu uchumi na utakatishaji pesa.

Hii pesa ndiyo inayotumika kwenye uovu mbalimbali, matumizi yasiyopitishwa bungeni, n.k.
 
Serikali hii imelaaniwa. Ndiyo maana sishangai N/waziri kutumwa aseme uongo bungeni halafu naye akakubali.

Zanzibar waliposikia kuwa wana muamala mkubwa T/Bara, BLW wakakomaa wabazitaka fedha zao. N/W yule yule aliyetumwa kudanganya ametumwa kuusaliti uongo wake.

Bado Mwijage na takwimu zake feki za viwanda.
 
Hivi Huwa hauoni aibu kufanya spinning Zitto???

Hata kama kazi yenu ni KUPINGA nakushauri wakati mwingine uwe Unahisi aibu fulani hivi

Haya twambie wapi kakiri kudanganya???

Au neno Kupeleka kwako wewe lazima iwe ni kutoka Dar kwenda Znz

Kufanya transaction Siyo Kupeleka??
 
Naona serikali ya ccm wanapima kina cha maji marefu kwa mguu kumpata msafi ndani ya ccm ni sawa na kutafuta bikra wodi ya wazazi.
IMG_20180609_072529.jpg
 
safi sana Zitto!

sasa parallel to that, anzisha legal process kama alternative approach ikiwa hizi pressure za kisiasa au kupitia bunge zitashindikana.

we need our moolah (1.5tr) back....and fast!
 
Serikali imekiri kudanganya kuhusu TZS 204 Bilioni za Zanzibar Katika Sakata la TZS 1.5 trilioni

Katika majibu ya Serikali Kuhusu kutoonekana kwa TZS 1.5 trilioni, Serikali ilisema kuwa ilipeleka Zanzibar jumla ya TZS 203.9 bilioni ( transfer to Zanzibar). Tuliijibu Serikali kuwa haikuwa kweli Kwani makusanyo ya Zanzibar hubakia Zanzibar hivyo haiwezekani kuwa Serikali ya Muungano ilipeleka fedha Zanzibar. ( maelezo yetu yapo hapa chini ).

Jana Serikali imekiri kuwa maelezo yetu ni sahihi na Fedha ya Zanzibar haivuki maji hivyo kufanya majibu ya Serikali ya awali kupoteza maana. Serikali ilitaka kutumia kichaka za Zanzibar kujificha kwenye sakata hili. Maelezo mapya ya Serikali haya ( Serikali yafunguka sakata la trl. 1.5 ).

Serikali pia imekiri kuwa unapaswa kufanyika uchunguzi wa kina kupitia miamala ya TZS 1.5 trilioni ili kuthibitisha zilipo. Gazeti la The Citizen wamemnukuu vizuri Naibu Waziri wa Fedha ( Govt: No proof of corruption yet in connection to ‘missing’ ).

Hii inadhihirisha kuwa Majibu ya awali ya Serikali yalikuwa ni ya kujikosha na yamefutwa na kauli za sasa. Bado kuna haja ya Kamati ya PAC kuagiza Ukaguzi Maalumu kwenye miamala ya TZS 1.5 trilioni na kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu Kuhusu upotevu wa fedha hizo.

—————————

Maelezo ya Ado Shaibu kuhusu Fedha za Zanzibar katika TZS 1.5 trilioni

Makusanyo ya TRA ya Zanzibar Hubaki kwa SMZ, Hayatokei Kwenye Hesabu za SMT

Kikawaida makusanyo ya TRA Zanzibar hubaki Zanzibar, hutuzwa kwenye akaunti za SMZ Katika Benki Kuu na huhesabika kuwa ni mapato ya Zanzibar, Kamwe fedha hizi hazichanganywi na mapato ya Serikali ya Muungano. Makusanyo haya, pamoja na matumizi yake, hukaguliwa na Ofisi ya CAG Zanzibar. Hivyo basi, hesabu zake hazitarajiwi kutokea kwenye ripoti ya CAG iliyokabidhiwa bungeni.

Ndio maana taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Zanzibar ya mwaka 2016/17 imeeleza namna makusanyo husika ya TRA na ZRB yalivyofanyika na namna fedha hizo zilivyotumika katika miezi 9 ya mwaka wa fedha 2016/17. Fedha zote za TRA Zanzibar kwa miezi hiyo 9 zimekusanywa na kubaki chini ya SMZ, na kutumika na SMZ bila kupitia SMT.

Mpaka Machi, 2017, Fedha ambazo SMZ hawakuwa wamekusanya kutoka TRA Zanzibar ni mapato tarajiwa ya robo ya mwisho wa mwaka (Aprili - Juni, 2017) yaliyokadiriwa kufikia shilingi 52.8 bilioni tu.

4. PAYE za Watumishi wa SMT Walioko Zanzibar Hukusanywa na SMT kwa Niaba ya SMZ

Fedha pekee za mapato ya kikodi ambazo Serikali ya Muungano huzikusanya kwa niaba ya SMZ, ni fedha za makato ya Kodi (PAYE) za watumishi wa Serikali ya Muungano wanaofanyakazi Zanzibar, watumishi hawa ni kama Polisi, Wanajeshi nk. Fedha hizi hukusanywa kila mwezi na TRA makao makuu, hutunzwa kwenye akaunti ya hazina Benki Kuu ya Tanzania, na kisha hupelekwa hazina ya Zanzibar.

Fedha hizi hukusanywa kila mwezi, na zinapaswa kupelekwa Zanzibar kila mwezi ili kugharamia shughuli mbalimbali za SMZ. Kwa mwaka wa fedha wa 2016/17, matarajio ya makusanyo PAYE yalikuwa ni shilingi 21 bilioni. Kwa kuwa idadi ya watumishi hawa inafahamika, Wizara ya Fedha ya Zanzibar, wakati ikielezea utekelezaji wa Bajeti ya 2016/17, ilionyesha kuwa yalikusanywa yote kwa 100%.

5. Juni 30, 2017 akaunti ya Zanzibar BoT Ilikuwa na Shilingi Bilioni 14 tu.

Fedha za Zanzibar kwenye akaunti zake Benki Kuu (BOT) zinaweza kuonekana kwa urahisi kwenye Hesabu za Benki Kuu. Hesabu za BOT kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2017 hazionyeshi uwepo hizo shilingi 203.9 bilioni ambazo SMT wanadai kuikusanyia SMZ. Hata wakati wa kufunga hesabu za BOT kwa mwaka 2016/17 fedha pekee zilizokuwa kwenye akaunti hiyo zilikuwa ni shilingi Bilioni 14. Hivyo sio sahihi hata kidogo kwa Taarifa ya Naibu Waziri Fedha kuonyesha kuwa kulikuwa na ‘transfer to Zanzibar’ kutoka Makusanyo ya Mapato ya Serikali ya Muungano.

Serikali Ijibu Maswali Haya. Isituhadae!

Maelezo ya SMT bungeni ni kinyume na nyaraka za BOT, pamoja na taarifa za Wizara ya Fedha na Mipango ya Zanzibar. Ni vema sasa SMT ijibu chanzo cha mapato haya ya kikodi (203.9b) ni kipi? Kama fedha zilizokusanywa na TRA Zanzibar, zimeonywesha na SMZ kwenye BLW kuwa zimekusanywa, kubaki na kutumika Zanzibar, hizi SMT inazodai kuikusanyia Zanzibar na kukaa nazo kwa mwaka mzima ni zipi? Na ziko wapi? Fedha hizi zimekusanywa na kulipwa Zanzibar kupitia akaunti gani? Zanzibar wamepewa lini fedha hizi? Matumizi yake ni yapi kwa mujibu wa bajeti iliyopitishwa na BLZ? Je utaratibu wa makusanyo ya Zanzibar umebadilika na sasa Fedha za Zanzibar zinakaa Hazina ya Muungano? Kama utaratibu umebadilika, ulibadilika lini na je utaratibu mpya una ridhaa ya Baraza la Wawakilishi?

Kwa taarifa ile ya Serikali Bungeni, mpaka Juni 30, 2017, ni wazi kuwa SMT bado ilikuwa imezishikilia fedha za SMZ, ambazo kikawaida hutolewa kila mwezi ili kuwezesha Zanzibar kujiendesha. Tukiamini kuwa huu ndio ukweli, na kuwa bunge halijadanganywa, basi ni dhahiri kuwa tunapaswa kuamini kuwa Serikali ya Zanzibar ilikuwa inajiendesha kwa MIUJIZA, ikikusanya mapato HEWA na kufanya matumizi ya KUFIKIRIKA ya mishahara, ruzuku, pensheni kwa wazee na miradi ya maendeleo.

Maana ni jambo lisiloweza kuingia akilini kuwa Fedha zote zinazokusanywa kwa niaba ya Zanzibar Katika mwaka 2016/17 hazikutolewa kwenda Zanzibar na kubakia Bara mpaka baada ya mwaka kuisha. Pia taarifa za mwenendo wa Akaunti za SMZ zilizoko BOT ni uthibitisho wa dhahiri kuwa hakukuwa na fedha za SMZ, shilingi 203.9 bilioni zilizoshikiliwa na SMT wakati au mara baada ya mwaka wa fedha wa 2016/17 kuisha.

Kama SMT wanadai kubaki na fedha hizi kwa mwaka mzima wa fedha (2016/17), na kushindwa kuziwasilisha hesabu zake kwa CAG miezi mitatu baada ya mwaka wa fedha kufungwa (Septemba 2017), na hata kwenye Exit Meeting (Januari 2018), ni vema waonyeshe tu hata walikozitunza katika akaunti zao BOT.

Shilingi 1.5 trilioni ni karibu mara 2 ya bajeti yote ya Zanzibar, kupotea namna hii na maelezo ya kupotea kwake yawe ni uongo wa kuisingizia Zanzibar ni dharau kubwa kwa Zanzibar, ni kuidogosha Zanzibar, ni kitengeneza kero mpya ya muungano wetu kwa SMT kuitupia madudu yake SMZ, ni hadaa kwa umma, ni kutudharau Watanzania. Hatutakubali. Tutaendelea kuhoji ziliko shilingi 1.5 trilioni zetu mpaka tujue ziliko.

#1.5trilioniZipoWapi?

Masikini ya Mungu, Watanzania wamegoma kuamini kwamba Serikali yetu imeiba fedha mmebakia kupaniki tu!

Ingawaje mnatumia nguvu nyingi sana lkn hakuna anayewaamini, swali labda la kujiuliza ni kwa nini? Mbona ufisadi mwingine kama epa, escrow & Co. Watanzania walikuwa on board? Iweje sasa hivi wamewapotezea?

Ni kwa sababu tuna imani na Raisi wetu, tunaona matokeo ya fedha zetu kwani kazi zinafanyika, ukienda site reli inajengwa, TAZARA inakaribia kuisha, ATCL yetu inasimama, TTCL nayo iko poa, Askari wetu wanafanya kazi ajali zimepungua sana, usalama wetu uko vizuri, kipo kingine tunahitaji?
 
Masikini ya Mungu, Watanzania wamegoma kuamini kwamba Serikali yetu imeiba fedha mmebakia kupaniki tu!

Ingawaje mnatumia nguvu nyingi sana lkn hakuna anayewaamini, swali labda la kujiuliza ni kwa ninj?
CCM bila polisi 2020 chaliii!!
 
Back
Top Bottom