Kwa hiyo unasema kua katiba ilisajiliwa kinyemela bila kufuata utaratibu?Katiba za vyama vya hiari ikiwepo TFF husajiliwa na serikali (msajili)...
Kosa lililofanyika ni kwa serikali kupitia msajili wake kuisajili katiba mpya ya TFF (iliyobadilishwa kwa waraka sio mkutano mkuu kama katiba ya 2006 inavyotaka).
Waziri alitakiwa kumwagiza msajili kutengua usajili on premise kwamba alipotoshwa na TFF.....hapa ingekuwa on TFF kuprove kuwa hawakumdanganya Msajili kwamba mabadiliko ya katiba yalifuata taratibu husika
halafu ukimsikiliza Tenga, anang'aangania kua serikali kuwaambia watumie katiba ya mwaka 2006 ni kwamba tubarudi kule kule akisema kua kuanzia miaka ya 2008 mpka 2011 kuna mikutano mikuu imepitisha mambo mengi kwa hiyo eti haiwezi kutumika..
Kwa hiyo unasema kua katiba ilisajiliwa kinyemela bila kufuata utaratibu?
Ndolanga tulimsema tukaja kumpenda Tenga sasa naona Tenga anarudia ya NdolangaKosa kubwa alilofanya Tenga na timu yake ni kumfanyia fitina Wambura kila uchaguzi,Tangu ameingia madarakani kila Wambura akigombea uongozi wa soka popote walikuwa wanamwekea zengwe,tangu huko nyuma wangemwacha agombee ashindwe mwenyewe sidhani kama leo angelipua hilo bomu la katiba.Walidhani hata sasa watamwondoa but wakasahau kujipanga
acha tufungiwe kwani tuna faida gani katika soka hapa duniani?
Wadau,
Nimejaribu kufuatilia hili sakata la TFF, kati ya Wizara na TFF nimeona kuna mambo ya kujadili, ukimsikiliza Waziri anadai kua katiba mpya ya TFF imekiuka taratibu na kwa hiyo katiba hiyo ni batili. Ila ukimsiliza Tenga mwenyewe anasema kua maagizo aliyotoa wazir hayatekelezeki na akatoa onyo kua hili lizaweza kupelekea Tanzania kufungiwa na FiFa. Je kwa wale wchambuzi wa mambo hivi hapa nani mkweli kwenye hili Sakata?
soka la bongo uzuhi mtupu tunakomaa basi tu..